Wasichana na wanawake tafuteni waume siyo wafanyakazi

Sahihi kabisa
 
Pole mkuu. Vijana wa hovyo humu JF hawapendi uhuru wa mwanamke. Hawapendi mwanamke ajieleze kile takacho bali kile watakacho,uzi wako umewachoma na kuwauma sana.

Tuvijana tuvivu tuvivu tunaona kama umetusimanga kwa vile unaishi london walitegemea utakua tiketi ya kuwavuta huko ulipo.

Tukikubali kupeana uhuru humu hizi judgements za ajabu ajabu zitapungua na kuisha. Anatokea mburura mmoja na kutoa mifano ya wazazi wake mara nyenyenyee eti yeye alilelewa na mke kabla hajapata kazi.


Maisha ya saiv ni kusaidiana na sio kutegemeana na kupunjana. Wakaka,wababa,wababu wanalalamika kuchunwa pesa kila leo ila hawapendi mwanamke mwenye pesa awe na uhuru wa pesa zake
Mimi sitaki kijana pia, vile vile acheni kutukana na kuhukumu sio sawa kabisa.
 
Zanzibar2014 ni member mpya Jamani mkaribisheni basi amejoin jana ila mshaanza kumchangamsha pia muelekezeni na ku reply.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] umfundishe wewe kureply
 
Kwa kweli mdogo wangu uko sahihi kabisa, mimi nawashangaa kabisa na tabia zao za ajabu. Waona ni utu kutukana na kuhukumu mtu. Nahisi stressi za maisha na kutojielewa pia.
 
Mfano huyo mwanaume akipoteza kazi, ndoa itaendelea kuwepo?
 
Hapo ni kulingana na uvumilivu wa mwanamke husika. Mkuu kuna wanawake waliwaacha waume zao baada ya kutoswa kwenye vyeti feki na walikua wametoka mbali mfano wa mleta mada na mkewe,wazazi wa mleta. Wengine walikua na ajira,biashara walizotafutiwa na waume zao.
Mfano huyo mwanaume akipoteza kazi, ndoa itaendelea kuwepo?
 
Nimekuelewa mdogo wangu, unamtizama na mwanaume husika. Kuwa haya ni maisha, muhimu tu asiwe mvivu atatafuta kazi nyengine. Tatizo mdogo wangu akiwa mvivu.
 
Mimi sitaki kijana pia, vile vile acheni kutukana na kuhukumu sio sawa kabisa.
Punguza munkari na kujishuku, hamna mtu ametukana mtu hapa, ni mawazo huru na maoni huru, maoni ya mtu yakiwa ni tofauti na uliyonayo kichwani usitafsiri kama tusi au kusakamwa.

Mfungua uzi kaleta mada yake huru, hajashinikizwa na mtu au hajaja kujibu uzi wa mtu mwingine,

Uzi za wanaotaka wenza ni nyingi hivyo basi huna haja ya kuhofia kila usomacho.

Naona sehemu nyingi unaandika watu wanatukana na kukashifu binafsi sijaona matusi wala kashfa sijui unatafsiri namna gani, inaonekana hujiamini kwa namna fulani, mtu asiyejiamini siku zote hudhani ni yeye tu anaonewa na kutukanwa na kusemwa, badili mtazamo wako sasa.
 
Soma messegi zangu nilizosema nimetukanwa na kuhukumiwa kwanza. Na wengine ni waongo kwenye macho yangu. Sijapata kuona, mimi sisemi tu tizama kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…