Wasichana na wanawake tafuteni waume siyo wafanyakazi

Wasichana na wanawake tafuteni waume siyo wafanyakazi

Hapo ni kulingana na uvumilivu wa mwanamke husika. Mkuu kuna wanawake waliwaacha waume zao baada ya kutoswa kwenye vyeti feki na walikua wametoka mbali mfano wa mleta mada na mkewe,wazazi wa mleta. Wengine walikua na ajira,biashara walizotafutiwa na waume zao.
Kwa mazingira hayo, kilichooa hapo ni ajira na si mapenzi; chukulia mfano uko kwenye ndoa, mara ghafla ukapata ajali na ukawa kipofu; hapo si mtakimbiana?
 
Nimekuelewa mdogo wangu, unamtizama na mwanaume husika. Kuwa haya ni maisha, muhimu tu asiwe mvivu atatafuta kazi nyengine. Tatizo mdogo wangu akiwa mvivu.
Unaweza ukapaboresha kwa kusema, nataka mwanaume mwenye maono ya kuona mbali
 
Katika vitu vinanishangaza ni wanawake wa kileo kutafuta wafanyakazi na wafanyabiashara baada ya kutafuta wanaume wa kuwaoa.

Inakuwaje mwanamke unaweka sharti la dini kwenye ndoa na sharti la mume au mke kuwa na kazi?

Dini sio ndoa Kama dini ni ndoa mngetongozwa uko msikitini na Makanisani kwanini hampati waume uko msikitini na Makanisani?

Au kwanini hampati waume uko makazini kwenu wakati mkija mitandaoni mnaanza kusumbua watu kwa vigezo kibao?

Natoa ushuhuda, mimi baba yangu na mama yangu wameoana mwaka 1985 na baba yangu hakuwa na kazi alikuwa kamaliza kidato cha nne lakini waliishi mpaka baba akaja kuwa mwandisi baadaye mwaka 1995 wakati huo tulishazaliwa sisi watoto wake.

Pia natoa mfano wangu mimi wakati namaliza chuo nilikuwa sina kazi mwaka, nilikuwa napanga chumba kimoja kinondoni lakini nilioa na baada ya kuoa nikaanza biashara na kupiga pesa mpaka leo nina familia na nyumba yangu ya kuishi na ndoa yangu ina amani sana.

Kama mke wangu angetaka mtu mwenye kazi na masharti kibao leo angekuwa hajaolewa.

Nawashauri wanawake waache kuweka masharti mengi kwa wanaume, kwenye ndoa hakuitaji masharti muhimu upendo hayo mambo ya dini, sijui kazi, kama unataka wa dini yako kamtafute msikitini au kanisani.

Na kama unataka mtu mwenye kazi mpate hapo hapo unapofanya kazi!
Mkuu hizi mbwembwe na masharti ya kuwa na kazi and so on kwa wanawake ni umri kati ya 18 - 29. Huu muda ndio wanakuwaga na masharti kibao wako radhi hata kuwa vimada cha msingi ni pochi yako tu.

Shughuli yao inaishaga wakiwa na 30 na kuendelea, hapo huwaga hawachaguagi wanajua jua limeshazama (Umri umeenda) wanaweza wakakosa kabisa.
Umri huo huwa yeyote alie mbele yao huwa hawakatai.
 
Pole mkuu. Vijana wa hovyo humu JF hawapendi uhuru wa mwanamke. Hawapendi mwanamke ajieleze kile takacho bali kile watakacho,uzi wako umewachoma na kuwauma sana.

Tuvijana tuvivu tuvivu tunaona kama umetusimanga kwa vile unaishi london walitegemea utakua tiketi ya kuwavuta huko ulipo.

Tukikubali kupeana uhuru humu hizi judgements za ajabu ajabu zitapungua na kuisha. Anatokea mburura mmoja na kutoa mifano ya wazazi wake mara nyenyenyee eti yeye alilelewa na mke kabla hajapata kazi.


Maisha ya saiv ni kusaidiana na sio kutegemeana na kupunjana. Wakaka,wababa,wababu wanalalamika kuchunwa pesa kila leo ila hawapendi mwanamke mwenye pesa awe na uhuru wa pesa zake
Sidhani kama umemuelewa mtoa mada, hajamaanisha uolewe na marioo au kibenten hapana, alichomaanisha ni kuwa uolewe au kuoa kwa sababu ya upendo, mengine ni nyongeza.
 
Kizazi hiki Cha kudanga ni hatari Sana kwenye mustakabali wa ndoa..wanawake waelewa ktk hili wachache Sana..Sio Kila mwanaume anakuwa tayari amejikamilisha ndio aingie kuoa..Mwanaume akiwa na vision ya Nini anataka kufanya na anajibidisha inatosha.Mengine Mungu atafungua mbele ya safari .

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom