Wasichana na wanawake tafuteni waume siyo wafanyakazi

Wasichana na wanawake tafuteni waume siyo wafanyakazi

Mwanamke akitoa mawazo mnakimbilia neno feminism. Mwanaume akitoa wazo mnakimbilia kusema ukidume duh
Feminism inawaharibu sana pia mna ubinafsi sana.

Hv kama mnataka haki sawa, kwanini msipange matumizi ya mishahara yenu na waume zenu. Mishahara yenu inawanufaisha ninyi peke yenu lakini mnalilia haki sawa
 
Tatizo linaanzia kwenu mkuu hamna misimamo dhabiti. mkianza kufukuzia penzi mnagawa sana pesa bila kuweka mipango sawa na mkiingia kwenye ndoa bado mnalambisha asali kisha mbeleni ndo ghafla mnaanza taka kubadili gia hapo ndipo mnapoanza kuzitambua rangi halisi za wake zenu
Nikwasababu mawazo ya wanawake wa kisasa yamejaa ubinafsi
 
Tatizo linaanzia kwenu mkuu hamna misimamo dhabiti. mkianza kufukuzia penzi mnagawa sana pesa bila kuweka mipango sawa na mkiingia kwenye ndoa bado mnalambisha asali kisha mbeleni ndo ghafla mnaanza taka kubadili gia hapo ndipo mnapoanza kuzitambua rangi halisi za wake zenu
Hapa sitii neno maana umesema ukweli.

Tatizo pia la wanawake wa kileo, bila pesa utasugua sana benchi na wanaume tumeanza kutumia hisia katika maamuzi badala ya akili
 
Katika vitu vinanishangaza ni wanawake wa kileo kutafuta wafanyakazi na wafanyabiashara baada ya kutafuta wanaume wa kuwaoa.

Inakuwaje mwanamke unaweka sharti la dini kwenye ndoa na sharti la mume au mke kuwa na kazi?

Dini sio ndoa Kama dini ni ndoa mngetongozwa uko msikitini na Makanisani kwanini hampati waume uko msikitini na Makanisani?

Au kwanini hampati waume uko makazini kwenu wakati mkija mitandaoni mnaanza kusumbua watu kwa vigezo kibao?

Natoa ushuhuda, mimi baba yangu na mama yangu wameoana mwaka 1985 na baba yangu hakuwa na kazi alikuwa kamaliza kidato cha nne lakini waliishi mpaka baba akaja kuwa mwandisi baadaye mwaka 1995 wakati huo tulishazaliwa sisi watoto wake.

Pia natoa mfano wangu mimi wakati namaliza chuo nilikuwa sina kazi mwaka, nilikuwa napanga chumba kimoja kinondoni lakini nilioa na baada ya kuoa nikaanza biashara na kupiga pesa mpaka leo nina familia na nyumba yangu ya kuishi na ndoa yangu ina amani sana.

Kama mke wangu angetaka mtu mwenye kazi na masharti kibao leo angekuwa hajaolewa.

Nawashauri wanawake waache kuweka masharti mengi kwa wanaume, kwenye ndoa hakuitaji masharti muhimu upendo hayo mambo ya dini, sijui kazi, kama unataka wa dini yako kamtafute msikitini au kanisani.

Na kama unataka mtu mwenye kazi mpate hapo hapo unapofanya kazi!
Hhhhhhmmmmm 🙏🙏
 
Mapenzi ni fumbo, utakapopata shikilia hapohapo. Wanaume wenyewe siku hizi wanaoa sura na makalio, wale tuliambia mke tabia tuko palee Ila msituite nyau.
 
Umeongea neno. Wanawake wanajionaga wazuri sana na wakiona una date na mtu kapuku wataku simanga hadi ujute. Wakute kwenye thirties sasa
Poleni kaka zangu nasema kaka zangu wengine humu ni waume za watu.

Najua sio sawa kuwa mnasimangwa, ndio maana mimi kwenye profile yangu nimesema mume wangu awe anafanya kazi au biashara.

Sikusema kazi gani kuwa nathamini kazi zote, muhimu ni ya halali lakini sitaki mume mvivu kuwa mimi sio mvivu na nafanya kazi pia.
 
Mapenzi ni fumbo, utakapopata shikilia hapohapo. Wanaume wenyewe siku hizi wanaoa sura na makalio, wale tuliambia mke tabia tuko palee Ila msituite nyau.
Kweli dada yangu, uko sawa kabisa.
Mimi niko makini mnooo, ahsante saaana 🙏🙏
 
Sio tabia njema kusimanga kazi kuwa kazi ni kazi tu, muhimu ni ya halali na mwenzako asiwe mvivu. 🙏
We dada sijui mama una matatizo ya akili? Nimesimanga kazi ya mtu? Hivi mods kuna uwezo wa kublock mtu asiwe ana reply post zako. We mama tafuta wachumba huko uk mimi niache eboo
 
Back
Top Bottom