Wasichana wa kazi wa ndani

Vipi wee Rick Blair.Sasa kama mimi ninayefanya kazi serikalini,Umeshasema ninalipwa sh 200,000 kwa mwezi.Sasa nikimlipa housegirl 150,000 kwa mwezi,Ina maana umeme,maji, nauli,Chakula,Nitalipia na Nini.Tuiombe Serikali ifanye minimum salary serikalini na kwingine kuwa 500,000 ili wazo lako lifanye kazi
 
Anajishaua tu mtoa mada , usikute kwao alilelewa na house girl anayelipwa elfu 15 kwa mwezi afua kaja JF yupo nyuma ya keyboard anatype upuuzi tu hapa.
Watu wengine bwana; kweli shule haiondoi Ujinga. First nimelelewa na housewife mom who did most of the work and tuvokua tukawa tunamsaidia while baba was the breadwinner so hatukujishaua kuleta mdada wa kazi ili umlipe iyo 15k that's why I said km we maskini pia acha kuajiri watu fanya kazi mwenyewe
 
Nimesema km huwez kumudu usiwe naye km mtoto tu. Usizae km huwezi kulea
 
Wanaharakati za wanawake na wasichana utasikia wanakwambia binti akijihusisha na mahusiano katika umri mdogo atajiharibia ndoto zake na kuweka rehani future yake.

Ila kuwa house girl somehow haiharibu ndoto zake. Cha ajabu idadi ya mabinti wanaoharibiwa maisha baada ya kuletwa mjini wakiwa wadogo majority chini ya miaka 16 idadi inaongezeka. Wengi wanakuja kuishi then huondoka kwa kukorofishana na akina mama wenye nyumba.
 
Mtu anakula bure, analala bure, halipii maji ,halipii umeme ,matibabu pia wakati mwingine huwa ni kwa bosi aliyemuajiri , sasa kwa nini alipwe pesa yote hiyo?

Haya makelele yote unayotupigia hapa Bora urudi shule ukafundishwe kuandika.
 
Ndo maana nikasema fanya kazi Mwenyewe mkuu; unaingiza 100k kwa mwez unaleta msichana wa kazi wa nn??😝😝😝 ni sawa sawa utake tv na umeme huna
Nyumbani kulikuwa na housegirls wamepokea sana hizo 20k kwa kipindi hicho na wengine kupelekwa kwenye ushonaji upishi na mpaka leo wengine wanaenda home kusalimia
 
Maybe your dad had money. Let's say uwe na mume anapokea mshahara mdogo , ndo utabaki nyumbani eti kisa kulea watoto? Maisha ya sikuhizi Kama mke anaujuzi, na yeye pia anaenda kutafuta kipato . Hatupo NYC tupo daslamu mama. Nakataa , maskini pia anaweza kuwa kaajiriwa na mshahara wa 350K na Ana dada wa kazi wa 50k vizuri tu.
 
Mara nyingi wanaoropokwa kuhusu mabintinwa kazi hawajawahi kuishi nao wanazungumza kinadharia tu ingia site mzee umemtoa kanda ya ziwa anakaa wiki anaondoka anatoroka au anasingizia kafiwa ..utaufyata kupiga debe walipwe laki 2 ..sio shida kwa mwenye pesa kuilipa pesa hiyo illa ss unga mwana maisha yetu tunayajua wenyewe na mabinti wetu wa kazi
 
hao mabinti wengi unakuta waliacha shule au hawapati kazi rasmi, wengine wametoroka nyumbani.... wanalazimika tu kufanya kazi hiyo

kuna binti mmoja nakumbuka alitoroka kwao umasaini, alikua analazimishwa kuolewa kwenye umri wa 14, akawa hana namna zaidi ya kufanya kazi za uhouse girl
 
Still narudia usizae pia km huna uwezo; hii mentality ya kukazania kuzaa au kuingia kw ndoa ni kukariri na tunarithisha umaskini tu. Na My Dad wasn't rich Bali middle income tu. Na why people hawachangii kuhusu unyanysaji wa hawa watu but kulilia hela tu?? Heri aliyesema tuishi nao km familia tu
 
Issue ya malipo kwa house girl ni pasua kichwa kwa Watanzania, sijui ni kutokana na kukariri au la ila nina hakika hata ukiamua kufanya survey basi asilimia 85+ ya watumishi unaowahoji watakwambia wanalipwa 50k kwa mwezi, na waliobaki ndio hela hiyo plus kidogo kana kwamba kuna bei elekezi yake

Kwenye suala la wafanyakazi wa ndani sijui tumerogwa na nani, hapa narejea mfano aliowahi kuutoa Marehemu Mufuruki kuwa hajui watanzania tumelogezewa nini kutumia mkaa

Unaweza kuta mtanzania tajiri kabisa ana majiko ya gesi, umeme etc ndani lakini bado atatumia mikaa pamoja na kufahamu fika jinsi upatikanaji wake unavyohatarisha mazingira
 
Anajishaua tu mtoa mada , usikute kwao alilelewa na house girl anayelipwa elfu 15 kwa mwezi afua kaja JF yupo nyuma ya keyboard anatype upuuzi tu hapa.
Anachoongea ni sahihi, two wrongs dont make a right tunapaswa tubadilike na kuondoa makosa waliyofanya watangulizi wetu

Lets be honest, 50k kwa mwezi?
 
Kaa utulie then andika vyema.

Yani ukae kwangu nakulipia kila kitu huna gharama ya ziada then nikulipe 200k. Huo mshahara wangu ni kiasi gani?
 
Anachoongea ni sahihi, two wrongs dont make a right tunapaswa tubadilike na kuondoa makosa waliyofanya watangulizi wetu

Lets be honest, 50k kwa mwezi?
Anaongea upuuzi tu.

Serikali imepanga kima cha chini 60k kwa wanaolala kwa mwajiri na 100k kwa wanaoondoka.

MAbalozi na wanadiplomasia 200k.

Yeye anajua kuliko serikali?
 
Akafanye kazi bar au akafanye kazi za ndani? ushawaona wale wa viwandani? Hakuna mtu anaenjoy mshahara wake kama house maid basi tu wapo chenga chenga sana, kikubwa asinyanyaswe na kupewa kazi nyingi kwa mshahara mduchu
 
Anaongea upuuzi tu.

Serikali imepanga kima cha chini 60k kwa wanaolala kwa mwajiri na 100k kwa wanaoondoka.

MAbalozi na wanadiplomasia 200k.

Yeye anajua kuliko serikali?
Serikali ni watu , na watu kama mimi na wewe, changamoto ni kuwa wanachoamua sasa kinaweza hata chukua miaka 10+ kisibadilishwe ilhali hali imebadilika sana

60k ni chache sana ila ndio uhalisia huo, maana hata wale wanaofanya kazi kwenye migahawa maeneo ya mijini malipo huwa kidogo sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…