Wasichana wa kazi wa ndani

Sawa boss mshaara tsh 200000/= namkata tsh 30000 kulala kwangu kama kodi,.elfu 3 kila siku kwa kula milo 3=120000/=,inabaki 50 haki yake,.bado sokoni anaenda yeye so chances za kujikuna buku buku zipo
Narudia; fanya kazi mwenyewe tu hata iyo 50k yako iokoe
 
Beki tatu kapata simu😂😂😂😂. Hotelini tu, service akilipwa atmost ni 180,000 na anatoa mashuka mikono wazi, na kusafisha vyoo.
Hatukulipi hyo hela wewe na dada zako. Ni mwenda wa 50-60. Sawa mwaya😂
 
Watu wa usafi kwenye makampuni,walinzi kampuni za kibongo wanalipwa laki moja hadi na elf 30 Kila kitu juu yako nauli, chakula,kodi Tena baada ya siku 40 au wanakopwa mwezi mmoja.
Ndo housemaid alipwe laki 2 kula kulala kila kitu kwa boss si Kila mtu atatamani awe housegirl
 
Mtu anakula bure, analala bure, halipii maji ,halipii umeme ,matibabu pia wakati mwingine huwa ni kwa bosi aliyemuajiri , sasa kwa nini alipwe pesa yote hiyo?

Haya makelele yote unayotupigia hapa Bora urudi shule ukafundishwe kuandika.

Anapokea retained earning kabisa[emoji23]
 
Wapo mabinti wngne wanakuja mpka na watoto wao waliotelekezewa , unamsaidia mpka kununua nguo za mtoto ,mafuta na matibabu ya mtoto , tena hyo 50 k ni nyingi sana.
 
wasichana wa kazi iwe marufuku kulipwa at the very most minimum ya 200k kwa mwezi na wale wa kwenda na kurudi at least 150k and I thk minimum salary is around iyo kwa serikali;
Soma kima cha chini cha serikali wafanyakazi za ndani kwa watu local ni 60,000/- Ila kwa watu kutoka nje ubalozini mpaka ikulu na wapi huko anakunja zaidi ya 600k mfanyakazi wa ndani, wale unaowaona ikulu pale wanapangapanga maji mezani
 
Madogo kwa minajili gani?

Kuna watu wanafanya kazi sehemu kubwa analipwa laki 5 na anajitegemea kila kitu. Mwisho wa mwezi hana duchu mfukoni.

House girl halipi kodi, hanunui chakula, hatumii nauli, halipi pango n.k....
 
Nadhani wakati anaandika hakufikiria kwa mañana zaidi kwa nn asiwee dalali wa kuwakuwadia wadada wa kazi huko Arabuni na India walipwe pesa anayoitaka
 
Naungana nawe kuhusu unyanyasaji ukomeshwe, kuhusu malipo ya elfu 50 ni halali kabisa.
Ebu angalia, kwa kawaida mtu kwa siku anakula 4000 nazungumzia kipato cha kati kwa wengi wetu Tz.
Ukichukua hiyo 4000 mara 30 unapata 12,000.
Chukua malazi + maji+sabuni kwa siku 1000 kwa mwezi 30,000.
Jumlisha sasa mshahara 50000+120000+30000= 200000

Kuna watu wanalipwa laki 2 kwenye makampuni na wanajitegemea hawawezi kuwa na balance ya elfu 50 kwa mwezi,
Usifanye mchezo na maisha mtoa mada.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…