Hashpower7113
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 1,353
- 2,142
Katika kitabu kitakatifu cha Biblia, Marko 10: 25 inasema: Ni rahisi ngamia kupenya katika tundu ya sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.
Wanachokielewa wengi, wakiwemo baadhi ya watumishi wa Mungu, ni kwamba ngamia anayezungumziwa hapa ni yule mnyama mwenye nundu kubwa mgongoni, pengine hata wewe kwa miaka mingi umekuwa ukijua hivyo.
Hata hivyo, ngamia iliyomaanishwa hapa, ni kamba! Ndiyo, kamba! Zile kamba nene zinazotumika kuvuta kwa mfano meli iliyozama na kadhalika. Makosa ya tafsiri hii yanaanzia kwenye kufasiri kifungu hiki cha Biblia kutoka kwenye Kiingereza kuja kwenye Kiswahili. Kwa Kiingereza, Mark 10:25 inasomeka hivi: It is easier for a camel to go through the eye of a needle than for a rich person to enter the kingdom of God.
Ukichukua kamusi yako, angalia maana ya neno camel, ya kwanza utaona ni ngamia mnyama lakini kuna maana ya pili ambayo ni hii: Camel: An apparatus for raising a sunken ship, consisting of one or more watertight chests to provide buoyancy. Kwa tafsiri nyepesi, ni kamba nene zinazotumika kuvuta meli iliyozama...
Kwa commoni sense ya kawaida tu, ngamia mnyama anawezaje kufananishwa na kupenya kwenye tundu la sindano? Hakuna uhusiano wowote, lakini kuna uhusiano wa kamba nene kupenya kwenye tundu la sindano kwa sababu kamba nyembamba (uzi) unapenya kirahisi!
Kwa hiyo tunahitimisha kwa kusema, ngamia/camel inayomaanishwa kwenye bible ni kamba. I stand to be corrected!