PostGE2025 Wasifu (CV) wa Naibu Waziri wa Elimu, Wanu Hafidh Ameir sijauelewa kabisa

PostGE2025 Wasifu (CV) wa Naibu Waziri wa Elimu, Wanu Hafidh Ameir sijauelewa kabisa

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Like maza like douta! Elimu ya kuunga unga mwanzo mwisho! halafu mama yake anamzawadia Wizara nyeti ya Elimu kwa nchi isiyo ya asili yake!! Aisee Gen Z mnatakiwa kuchukua hatua hiyo D9. Huku tunakoenda, ni kama dharau na masihara kwa Tanganyika yamepitiliza.
Mihemko imeanza kukutoa akili. Hivi huyu anayezungumza haya ni wewe? Unazungumzia nchi isiyo ya asili yake? Haya maskhara yamepitiliza .
 
Ataendaje? Unaelekea hujui kitu.
We kunguru umetokea wapi!?
Kama wewe ni miongoni mwa waosha miguu ya walaji basi pole.
Kama ni miongoni mwa walaji, ule vya mwisho mwisho...129 twaja!
 
We kunguru umetokea wapi!?
Kama wewe ni miongoni mwa waosha miguu ya walaji basi pole.
Kama ni miongoni mwa walaji, ule vya mwisho mwisho...129 twaja!
Na we ng'ombe unasema nini? Kama wewe kweli unajiamini tukutane siku hiyo!
 
Wanu Hafidh Ameir (born 9 February 1982) is a Tanzanian CCM politician and a member of the Zanzibar House of Representatives in the National Assembly of Tanzania since 2005. Her mother Samia Suluhu Hassan became President of Tanzania in 2021.

She graduated in law in 2018 from the online Open University of Tanzania
========
Wasifu wa Wanu Hafidh Ameir Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia

Taarifa Za Msingi
• Jina Kamili: Wanu Hafidh Ameir
• Tarehe ya Kuzaliwa: 09 Februari 1982
• Chama cha Kisiasa: CCM (Chama Cha Mapinduzi)

Elimu
• Shule ya Msingi: Mwanakwerekwe B Primary School (1990–1996)

• Sekondari: Kawanda Secondary School, O-Level (1997–2000)

• Sekondari ya A-Level: Kawanda Secondary School (2001–2002)

• Shahada ya Cheo cha Kazi (Certificate): Info-Serve Institute (2005–2006), kusaidia kazi za kisheria (“Legal Assistance”)

• Diploma: Centre for Foreign Relations, kozi ya Uhusiano wa Kimataifa na Utawala wa Diplomasia (2007–2008)

Historia ya Kazi
• Msaidizi wa Utawala (Administrative Officer), Wizara ya Utalii, Biashara na Uwekezaji, Zanzibar (SMZ) – mwaka 2010.

Uzoefu wa Kisiasa
• Mwanachama wa Kamati ya Utekelezaji ya CCM (CCM National Executive Committee) tangu 2010.
• Mwenyekiti wa CCM vijana, Unguja Kusini (2008–2012).

Mafunzo & Kozi Za Ziada
• Mafunzo ya ukuaji wa maendeleo (“Growth for Development”) – Uingereza, 2014.
• Cheti cha Uandishi wa Sheria (“Legal Drafting”) – Zanzibar Law Resource Centre, 2013.
• Mafunzo ya Uongozi (“Leadership Development”) – Chuo cha Wawakilishi, 2013.
• Kozi ya Kompyuta – Karume Technical Institute, 2003–2004.

Chanzo: Kulingana na Tovuti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar:
Naibu waziri haramu wa elimu ana elimu mbalimbali yaani ana elimu ya hapa na pale🤔🤔
 
Mihemko imeanza kukutoa akili. Hivi huyu anayezungumza haya ni wewe? Unazungumzia nchi isiyo ya asili yake? Haya maskhara yamepitiliza .
Sasa nyinyi Wazanzibari si mna serikali yenu! Huku Tanganyika mnafuata nini? Au mnafikiri kama huu Muungano wenu wa changu changu, chako changu Watanganyika tunaufurahia!
 
Haki ya Mungu munafanana tokea sura hadi ukilaza, ikitokea kweli ni kilaza.
Ni kilaza.Mimi nilipata division one form four na six.University nilipata first class 4,8 GPA. Kazini nimepata kwa akili zangu si kwa connection. Ni tofauti kabisa na yeye.
 
Ni kilaza.Mimi nilipata division one form four na six.University nilipata first class 4,8 GPA. Kazini nimepata kwa akili zangu si kwa connection. Ni tofauti kabisa na yeye.
Elimu ya Tz ni duni sana sijui huwa mnabrag kitu gani
 
Sasa nyinyi Wazanzibari si mna serikali yenu! Huku Tanganyika mnafuata nini? Au mnafikiri kama huu Muungano wenu wa changu changu, chako changu Watanganyika tunaufurahia!
Mkuu nilidhani sio wewe, ila kwakuwa ndiwe, tafakari haya: Huu muungano, kama unavyojua, chimbuko lake ni Nyerere ambaye nadhani unamjua sina haja ya kukupa wazifu wake. Yeye ndiye mbunifu wa huu muungano bila ya ridhaa ya Wazanzibari walio wengi. Nadhani unakumbukumbu kwamba muungano huu haukuridhiwa huku Zanzibar. Ni yeye kwa kutishwa na kivuli chake akataka, eti, kuidhibiti Zanzibar.

Sasa ukiniuliza sisi Wazanzibari tunafuata nini huko Tanganyika, ni vema nami nikakuuliza nyinyi mulifuata nini Zanzibar wakati ule?.

Ukiniuliza kufurahia changu changu na changu chako kuwa jee Watanganyika wanafurahia, mimi nikuambie tu, swala hilo jawabu lake unalijua wewe Mtanganyika, mimi halinihusu kwasababu ni Mzanzibari. Sasa naomba nikuulize wewe Mtanganyika unalifurahia hilo?

Mkuu, tupo JF - home of great thinkers. Tafakari hilo, usiongozwe na mihemko.

Zawadini.
 
Ni kilaza.Mimi nilipata division one form four na six.University nilipata first class 4,8 GPA. Kazini nimepata kwa akili zangu si kwa connection. Ni tofauti kabisa na yeye.
Ni kilaza. Hata kusema uongo hujui! Inahitaji akili kubwa kusema uongo ukafanana na kweli. Hili la Division one form four na six ushahidi uko wapi? Unajidanganya kwa ukilaza wako. Kuhusu First Class ya 4.8 ukaipatie wapi ? Au ni ile ya kule Mwanza iliyokuwa kabla ikitoa diploma ya uandishi wa habari? Nakukumbusha tu unazungumza na mtu mzima. Tuendelee.
 
Kwa hiyo unataka nikupe details ? Unataka unipe kazi au? Basi nikutajie Head mistress wangu O level ni Mama ........Na wa A level ni.....Mama..
 
Duh this is totally absurd now. Untolerable indeed. Total reshaping is needed here.
 
Kwa hiyo unataka nikupe details ? Unataka unipe kazi au? Basi nikutajie Head mistress wangu O level ni Mama ........Na wa A level ni.....Mama..
Endelea kujidanganya! Majisifu mengi ila hamna kitu inapokuja uhalisia. Nakujueni vizuri. Kajifunze kwanza kusema uongo halafu uje tujadili kwasababu msema pweke hakosi.
 
Back
Top Bottom