Zanzibar 2020 Wasifu: Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi, Rais ajaye wa Zanzibar

Zanzibar 2020 Wasifu: Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi, Rais ajaye wa Zanzibar

DK. HUSSEIN MWINYI MGOMBEA NYOTA (Star Candidate)

Na, Deogratias Mutungi

Wapiga kura upenda kumpata mgombea ambaye wanakuwa na imani naye na wanajitambulisha naye katika masuala ya uadilifu na kuwa makini katika kuongoza.

Wagombea nyota siyo zawadi kutoka kwa Mungu bali ni matokeo ya malezi katika familia, nje ya familia, shuleni, taasisi za umma na katika chama cha siasa. Hivyo taswira ya mgombea nyota ni kielelezo cha chama chake. Vile vile jambo la kuzingatia ni la uongozi na viongozi waasisi wa taifa hili na hivyo kuna urithi wa mila na desturi za uongozi ambazo zimetokana na uongozi na viongozi madhubuti wan chi hii. Si rahisi kusema mtu Fulani kujaliwa bila kujali mchango wa watu na asasi mbalimbali ambazo zinachngia kumjenga mtu.

Mgombea nyota ni binadamu kama binadamu wengine, Ana uwezo wake na mapungufu yake, kilicho kikubwa zaidi ni namna ya kudhibiti madhara, kuendeleza na kukuza uwezo wake, Mkakati madhubuti wa ujumla humwongezea uwezo mgombea nyota kumiliki kumiliki eneo kubwa zaidi kuliko kama kusingekuwepo na mkakati, Kwa mantiki yenye mashiko Dk. Mwinyi ananusuru ushindi wa Chama Cha Mapinduzi hata kabla ya mechi yenyewe rasmi kuanza (Uchaguzi)

Nyota ya Dk. Mwinyi inangara sana kuliko ya wagombea wenzake ambao wamechukua fomu, unaweza ukalinganisha Nyota ya Dk.Mwinyi na Baraka Hussein Obama rais wa zamani wa Marekani ilivyokuwa wakati akiomba Wamarekani wampe fursa ya kuwa Rais, kwa hoja hii hamna ubishi wa aina yoyote, Japokuwa kwa sasa zimeibuka hoja mfu zikijengwa kuwa Dk. Mwinyi haijui Zanzibar vizuri kuliko wagombea wenzake bila shaka hoja hizi ni porojo za kisiasa na zinalengo la kupotosha ukweli, inawezekana wanaojenga hoja za namna hii ni mamluki na vijeba wa siasa na wasio itakia mema Zanzibar na Wazanzibar wote kwa ujumla ni kheri kuwapuuza kuliko kuwapa ujiko husio na maana yoyote.

Aidha Hoja zinazojengwa na baadhi ya wanasiasa na wananchi wa kawaida kwa kile wanachokiita “Kwa nini watoto wa marais wasitaafu” Hoja hii inayojengwa kwa mantiki kuwa kwa nini watoto wa viongozi ambao wazee wao wamewai kuwa marais wa Zanzibar ndo wanataka kupewa nchi? Hoja hapa sisi watoto wa viongozi wastaafu bali uwezo wa vijana hao, Yapo maswali ya kujiuliza juu ya watoto hawa je niwaadilifu kiasi gani? Wanao uwezo wa kuongoza? Je wameguswa na changamoto za Wanzanzibar jibu kama ni ndio sioni mantiki ya kuwa nanga kwa hoja hii dhaifu, hatuwezi kumkosa kiongozi bora, shupavu na imara eti kwa sababu mzee wake amewahi kuwa rais wa nchi dhana hii kikatiba haipo na wala haina mashiko yoyote yale.

Kwa ufupi Dk. Hussen Mwinyi ni Star Candidate anayestahili kupewa fursa ya kuwaongoza Wanzibar kuliko mgombea mwingine wa aina yoyote kati ya 31 waliojitokeza kuchukua fomu ndani ya Chama Cha Mapinduzi, Kamwe uwezi kumlinganisha Dk.Mwinyi na Prof. Makame Mbarawa katika utendaji na “Ustar Candidate”
 
Deogratias Mutungi,

Star candidate ni mwenye nyota kichwani,paji la uso,mabegani au ni mtu alietumikia Taifa na vitu vikaonekana jamii ikakubali ktokana na ubunifu na ustadi wa hali ya juu ama nini mana ya star candidate mimi sjakuelewa..mkitaka kumnadi mtu kisiasa tumieni mifano ya mambo tija aliyofanya mtu sio tantalila hizi!!
 
Baada ya 10 ndiye atakayechukua visiwa vay Zanzibar

kapita kwenye 5 bora tena kawa wa kwanza
 
Wanzibari wakiona busara huyu atawafaa sana
 
MKIKOSEA MTAKUMBUKA HII SIKU
CONGS KUFUNGUA RUKSA WANANCHI AMA WANACHAMA HUSIKA KUANZA KUGOMBANIA CCM TKT KADHAA

NAPENDA NIWAMBIE WAAZI SIJIPONGEZI AMUAMINI ANGALIENI TABIRI ZANGU SIMBA NA YANGA

ANGALIENI SIKU CORONA INAINGIA NILIANDIKA NN NA MDAGANI MTASIKIA AIPO KABISA

LEO NAOMBA NIWEKEWAZI OCTOBER CCM. MKIKOSEA BASI HIKI KILIO MTANIKUMBUKA MAISHA

KWAMDAHUU ANAEFAAA ZNZ N HUSSEIN MWINYI TUMECHOKA SANA NNA MAJINA YA AJABU AJABU

HUSSEIN MWINYI AMEONYESHA UADILIFU HEKIMA. NA HESHIMA KUBWA KWA TAIFA KWA POSN ALIZOPEWA

SIDHANI SASA TUNAHITAJI KUFANYA TRIAL N ERROR PALE IKULU ZZNZ

NAWATAKIA KILA LA HERI KWA HILI
NAAMINI TUTAKUMBUSHANA SIKU IKIFIKA

STY BLSD
KWA MANUFAA YA WANZNZ WOTE

HUSSEIN MWINYI ATAKIBADILISHA KILE KISIWA NA KUWA KISIWA BORA KABISA KWENYE HII DUNIA

GODBLESS U ALL

Kweli mkuu.
 
Back
Top Bottom