Zanzibar 2020 Wasifu: Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi, Rais ajaye wa Zanzibar

Zanzibar 2020 Wasifu: Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi, Rais ajaye wa Zanzibar

Kwa Mara ya kwanza raisi wa Zanzibar anakuwa na asili ya Tanzania bara yaani pwani, mpambano utakuwa mkali maalim vs mwinyi
Maalim nae asili yake sio pwani, vimiwani, bara wala afrika. Tukianza kubaguana hatutajenga nchi
 
Kumbe ni mndengereko, kweli vyeo vya juu mnapeana tuu ndugu kwa ndugu,

Acha akachape kazi kama baba ake hamna shaka raisi wa zanzibar mpya
 
Na kwa wale wasiomfahamu najua wapo vijana wetu (wangu) wa UVCCM hapa..Bwana Hussein Ali Hassan Mwinyi (MD) alikuwa mbunge wa Mkuranga Mwaka 2000 hadi 2005 ndio akahamia Zanzibar aandaliwe kuwa alivyo sasa yaani mgombea wa Zanzibar. Ni fahari kwa Mndengereko huyu kuibeba CCM yetu Mpya huko Zanzibar..naimani tutashinda kwa kishindo kama kawaida😛😛
Tusisahau Salumu Mwalimu, naibu katibu mkuu wa Chadema Znz, Mwaka 2015 aligombea ubunge jimbo la Kikwanjuni, Zanzibar, na mwaka 2018 akagombea tena ubunge jimbo la Kinondoni Tanganyika.

Ukiwa mzanzibari, unaruhusiwa kugombea Tanganyika, lakini ukiwa mtanganyika huruhusiwi kugombea Zanzibar.
Sie watanganyika hatuna ubaguzi.
 
Kwakweli Baba wa Taifa Mwl.Nyerere kuna sehemu alikosea kabisa...yaani mpaka sasa hamna mtoto ambae ni waziri au Rais aisee
 
pia baba yake Mzee Ruksa aliwahi kuwa Rais wa serikali ya watu was Zanzibar awamu ya tatu(3),unabisha !
 
Mzanzibari anaweza kuwa Mbunge Tanganyika lakini mtanganyika hawezi hata kupiga kura Zanzibar!!

Huu Muungano ni BIG SCAM!!
 
Hivi inakuaje raisi wa kuongoza Zanzibar aje apendekezwe na Watanzania bara?
Maana ukiangalia wajumbe wa NEC ya CCM wa bara ni wengi kuliko wa Zanzibar
 
Nasikia huyu bwana wazenji hawataki kabisa kumsikia......m

Zenji wanaenda nanMaalim Seif
 
Wazanzibari hawana maamuzi. Maamuzi yako Dodoma Iwe kwa CCM yenyewe au hata upinzani. Maamuzi ya wazanzibari hayaheshimiwi.

Rais ajaye lazima apimwe na akubalike Dodoma. Lazima awe tayari kuendeleza ukoloni Wa Tanganyika kea Zanzibar.

Hill liko wazi.

Ishu sio kukubalika Zanzibar, ishu ni yupi Anafaa kwa maslahi ya Tanganyika.

Sadakta.
 
Maali seif ndo chaguo letu. Hakuna cha mwinyi wala cha pekeku
Hii imekaa vyema sana.......usultani sio mzuri kabisa......anaenda kulinda maslahi ya muungano badala ya maslahi ya Zanzibar!!!!
 
Maali seif ndo chaguo letu. Hakuna cha mwinyi wala cha pekeku
Ushauri wa bure maana umri unakwenda kwa huyu jamaa na Sultani naye umri unakimbia vile vile.

Hii inchi inavisiwa vingi, jichangeni au vipi Sultani ajipapasepapase mnunue kisiwa kimoja wapo (Kuna baadhi katika bahari ya Hindi visivyo kaliwa nawatu). Alfu mnakusanyana wote, hata kama ni 2/3 ya watu wote, mnahamia hapo na kumchagua Maalim raisi wenu. Ila msijitangaze kama nchi huru kwenye hicho kisiwa maana kisheria kitakuwa ni ardhi ya Jamhuri, japo mnaimiliki nyie. Mkijitangaza, Mabeyo halali yenu.
Huu ndo ushauri wa bure. Hii ya kutegemea Maalim apewe Znz, ashinde asishinde ni ndoto tu wakati wa uhai wake na Sultani mwenyewe akiwa bado hai.
 
Ushauri wa bure maana umri unakwenda kwa huyu jamaa na Sultani naye umri unakimbia vile vile.

Hii inchi inavisiwa vingi, jichangeni au vipi Sultani ajipapasepapase mnunue kisiwa kimoja wapo (Kuna baadhi katika bahari ya Hindi visivyo kaliwa nawatu). Alfu mnakusanyana wote, hata kama ni 2/3 ya watu wote, mnahamia hapo na kumchagua Maalim raisi wenu. Ila msijitangaze kama nchi huru kwenye hicho kisiwa maana kisheria kitakuwa ni ardhi ya Jamhuri, japo mnaimiliki nyie. Mkijitangaza, Mabeyo halali yenu.
Huu ndo ushauri wa bure. Hii ya kutegemea Maalim apewe Znz, ashinde asishinde ni ndoto tu wakati wa uhai wake na Sultani mwenyewe akiwa bado hai.

Ndiyo maagizo ya Kardinali wako, Pengo hayo ??
 
MKIKOSEA MTAKUMBUKA HII SIKU
CONGS KUFUNGUA RUKSA WANANCHI AMA WANACHAMA HUSIKA KUANZA KUGOMBANIA CCM TKT KADHAA

NAPENDA NIWAMBIE WAAZI SIJIPONGEZI AMUAMINI ANGALIENI TABIRI ZANGU SIMBA NA YANGA

ANGALIENI SIKU CORONA INAINGIA NILIANDIKA NN NA MDAGANI MTASIKIA AIPO KABISA

LEO NAOMBA NIWEKEWAZI OCTOBER CCM. MKIKOSEA BASI HIKI KILIO MTANIKUMBUKA MAISHA

KWAMDAHUU ANAEFAAA ZNZ N HUSSEIN MWINYI TUMECHOKA SANA NNA MAJINA YA AJABU AJABU

HUSSEIN MWINYI AMEONYESHA UADILIFU HEKIMA. NA HESHIMA KUBWA KWA TAIFA KWA POSN ALIZOPEWA

SIDHANI SASA TUNAHITAJI KUFANYA TRIAL N ERROR PALE IKULU ZZNZ

NAWATAKIA KILA LA HERI KWA HILI
NAAMINI TUTAKUMBUSHANA SIKU IKIFIKA

STY BLSD
KWA MANUFAA YA WANZNZ WOTE

HUSSEIN MWINYI ATAKIBADILISHA KILE KISIWA NA KUWA KISIWA BORA KABISA KWENYE HII DUNIA

GODBLESS U ALL


Chini ya CCM hata atokee malaika hakuna jipya zaidi ya kuongezeka udhalimu . Alikuwepo baba yake na hakuna jipya zaidi ya maudhi

Tuna msubiri Popo bawa lakini uelewa kwa dhuluma zilizofanywa na CCM na serikali zake si rahisi kujivua gamba
 
Hakuna cha Makame Mbarawa wala nani. Huyu ndiye atayeiingiza Zanzibar kwenye karne ya 21.
View attachment 1502736
Wasifu wake ni huu hapa:

Dk Hussein Mwinyi ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa katika Serikali ya Awamu ya Tano, ameteuliwa katika baraza la mwanzo la mawaziri la Rais John Magufuli. Kiongozi huyu pia ni mbunge wa jimbo la Kwahani lililoko Unguja, Zanzibar.

Dk Hussein Mwinyi Alizaliwa Desemba 23, 1966 kwenye kisiwa cha Unguja, Zanzibar. Dk Mwinyi ni mtoto wa Mzee Ali Hassan Mwinyi (Rais wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) na mama Sitti Mwinyi ambaye amekuwa (First Lady) katika awamu ya pili.

Kwa sababu ya kazi za baba yake mzazi, Dk Mwinyi alianza elimu ya Msingi jijini Dar es Salaam kati ya mwaka 1972 – 1976 akisoma katika Shule ya Msingi Oysterbay. Mwaka 1984 hadi 1985 wazazi wake walimhamishia Misri ambako aliendelea na masomo ya elimu ya msingi hadi kuhitimu katika Shule ya Msingi “Manor House Junior”.

Shule hii ilikuwa na hadhi ya “Middle School za Tanzania” kwa wakati huo. Hussein Mwinyi alipelekwa Misri kwa sababu baba yake (Ali Hassan Mwinyi) alihamishiwa nchini Misri kikazi kama balozi wa Tanzania nchini Misri wakati huo.

Hussein Mwinyi alirejea Tanzania na kuendelea na masomo ya sekondari katika Shule ya Sekondari Azania ambako alisoma kidato cha kwanza hadi cha nne mwaka 1982 – 1984. Alipohitimu kidato cha nne alifaulu na kupangiwa Shule ya Sekondari Tambaza kusoma kidato cha tano na cha sita, hata hivyo aliishia kusoma kidato cha tano peke yake mwaka 1984/1985, mwaka huo huo 1985 alienda nchini Uturuki kusomea utabibu wa binadamu. Alianza masomo ya udaktari nchini Uturuki mwaka 1985 kwenye Shule ya Utabibu ya Chuo Kikuu cha Marmara na kuhitimu Shahada ya Utabibu wa Binadamu mwaka 1992.

Kwa sababu hakumaliza kidato cha sita, alipokuwa huko ughaibuni alipitia masomo ya mwaka mmoja ya kujiandaa na udahili wa Chuo Kikuu “Pre University Studies”. Wakti huo Chuo cha Marmara kilikuwa kinapokea hata wanafunzi wa kidato cha nne kuanza kusomea shahada ya utabibu, lakini lazima wapitie mwaka mmoja wa maandalizi kama alivyofanya Mwinyi. (Sikufanikiwa kupata mawasiliano na chuo hiki ili kujiridhisha ikiwa hadi sasa wanatumia utaratibu huo)

Mwaka 1993, Mwinyi alikwenda nchini Uingereza kujiendeleza zaidi kielimu, aliendelea na masomo ya juu ya utabibu katika Hospitali ya Hammersmith ambako alihitimu shahada ya uzamili ya utabibu mwaka 1994 na kuunganisha shahada ya uzamivu ya udaktari hapohapo Hammersmith ambayo aliihitimu mwaka 1997.

Dk Mwinyi amemuoa Mariam Herman na wana watoto wanne; Ibrahim, Jamila, Tariq na Sitti.

Dk Mwinyi hakuishia tu kuwa daktari wa mdomoni, amefanya kazi za kidaktari. Alipohitimu shahada ya kwanza ya utabibu alirejea Tanzania na kufanya kazi kwa mwaka mmoja katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Na hata baada ya ya kuhitimu shahada ya uzamivu nchini Uingereza, alirejea nchini kwa mara nyingine na kufanya kazi katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Herbert Kairuki (HKMU) kwa miaka miwili hadi mwaka 1999.

Kiongozi huyu alijitosa kwenye siasa mwaka 1999 akiliwania Jimbo la Mkuranga mkoani Pwani (Bara) na kushinda. Alipokuwa mbunge, Rais Benjamin Mkapa alimteua kuwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, alikaa katika wadhifa huo hadi mwaka 2005.

Kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 Dk Mwinyi alijitosa tena jimboni, lakini safari hii siyo Mkuranga. Ilikuwa ni jimbo la Kwahani, Zanzibar – ambako alipambana na kuwashinda wagombea sita kutoka vyama vingine akipata kura 6,239 sawa na asilimia 85.6 akifuatiwa na Mussa Haji Khamis wa CUF aliyeambulia kura 921 sawa na asilimia 12.6. Baada ya kuwa mbunge kwa mara ya pili, Serikali ya Awamu ya Nne chini ya uongozi wa Jakaya Kikwete na Dk Mwinyi ilimteua kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais na alidumu hadi mwaka 2008 alipohamishiwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa alikokaa hadi mwaka 2010.

Mwinyi alirejea tena na kugombea ubunge katika jimbo la Kwahani mwaka 2010, akashindana na yuleyule hasimu wake wa mwaka 2005, Haji wa CUF, mara hii vyama vingine havikuweka wagombea na Dk Mwinyi hakupata shida kushinda kwa kura 5,277 sawa na asilimia 83.0 dhidi ya kura 1,085 sawa na asilimia 17.0 za CUF. Mara baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 Rais Kikwete akamteua Mwinyi kuwa Waziri wa Ulinzi kabla ya kumrejesha Wizara ya Afya mwaka 2012 na miezi 19 baadaye (yaani Januari, 2014) kwa mara nyingine tena akamteua kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, nafasi aliyodumu hadi mwaka 2015.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Dk Mwinyi alirudi tena katika jimbo la Kwahani, hii ikiwa ni mara ya nne akisaka nafasi ya kuwawakilisha wananchi, akafanikiwa kumshinda Khalid Rajab Mgana wa CUF na kuchaguliwa kuwa mbunge kwa kipindi cha nne. Rais JPM amemteua Mwinyi kuwa Waziri wa Ulinzi na Kujenga Taifa na hivyo kumuongezea rekodi ya kuongoza wizara hiyo kwa kitambo cha kutosha.

Mwaka 2015 Dk Mwinyi alitajwa sana kama mmoja wa wanasiasa wanaoweza kuvaa viatu vya JK ikiwa CCM ingeamua mrithi huyo atokee upande wa Zanzibar, hata hivyo yeye mwenyewe hakuwa na nia na hakuchukua hata fomu kwa ajili ya kuwania kiti hicho.

Ndani ya CCM Dk Mwinyi anashikilia nyadhifa mbalimbali, Mwaka 2000 aligombea na kushinda ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), akashinda tena mwaka 2007 na kushinda na tangu wakati huo aliteuliwa kuingia kwenye Kamati Kuu ya CCM hadi hivi sasa.

Dk Mwinyi ni mmoja kati ya mawaziri wenye rekodi za kuwa shahada tatu za ubobezi wa taaluma na elimu ya juu katika fani moja. Amesoma kwa uhakika na ni mtu mwenye uwezo wa kutumia stadi za ubobezi wake kujenga weledi wa jumla unaomfanya atoe uongozi wa kudumu hadi hivi, nina hakika kuwa ubobezi wake utaendelea kumbeba hata kwenye uteuzi wa sasa.

Jambo la pili ni uzoefu wa kibunge wa miaka 20 unaoambatana na uzoefu wa uwaziri kwa miaka 15. Mwinyi ana rekodi nyingine tena, ni kati ya wabunge walioweza kukaa bungeni kwa vipindi vitatu mfululizo (2000 – 2020). Huyu ni mmoja kati ya viongozi wa zama za sasa waliokaa muda mrefu kwenye utumishi wa ngazi ya juu na ikumbukwe kwamba muda wote huo amekuwa kwenye nafasi za uwaziri. Uzoefu wake wa pamoja unamtofautisha na mawaziri wengine wengi wanaojifunza kazi na huwenda ukamjengea kujiamini zaidi na kufanya vizuri zaidi.

LIVE - Uchaguzi 2020: Yanayojiri katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM. Dkt. Hussein Ally Hassan Mwinyi ateuliwa Kugombea Urais Zanzibar kupitia CCM
GENERAL
SalutationHon.
Member picture
1042.jpg
First Name: Dr. Hussein
Middle Name:Ali
Last Name:Mwinyi
Member Type:Elected Member
Constituent:Kwahani
Political Party:Chama Cha Mapinduzi
Office Location:P.O. Box 9120, Dar es Salaam
Office Phone: +255 754 279 343/+255 754 995 555Office Fax:
Office E-mail: hmwinyi@parliament.go.tz
Member Status: Active
Date of Birth 23 December 1966
EDUCATION
School Name/LocationCourse/Degree/Award
Start Date
End Date
Level
Manor House Junior School, Cairo, Egypt
CPEE​
1977​
1981​
Primary School​
Oysterbay Primary School
CPEE​
1972​
1976​
Primary School​
Azania Secondary School
CSEE​
1982​
1984​
Secondary School​
Tambaza High School
ACSEE​
1984​
1985​
Secondary School​
Marmara University Medical School, Istanbul Turkey
Doctor of Medicine​
1985​
1991​
Certificate​
Hammersmith Hospital, London, UK
Masters (Medicine)​
1991​
1997​
Masters Degree​
Hammersmith Hospital, London, UK
PhD​
1994​
1997​
PhD​
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name
Position
From
To
Ministry of Defence and National ServiceMinister
2014-01-20​
2015​
Ministry Of HealthMinister
2012​
2014-01-20​
Vice-President's Office - Union AffairsMinister
2006​
2/8/2008​
Ministry of HealthDeputy Minister
2000​
2005​
Ministry of Defence and National ServiceMinister
2/13/2008​
To Date​
Hubert Kairuki Memorial UniversityLecturer
1998​
2000​
Hubert Kairuki Memorial UniversitySpecialist Doctor
1998​
1999​
Ministry of Health - Muhimbili HospitalRegistrar
1994​
1995​
Ministry of Health - Muhimbili HospitalDoctor
1993​
1993​
Marmara UniversityIntern
1991​
1992​
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location
Position​
From​
To​
Chama Cha Mapinduzi, CCMMember - National General Council
2005​
Todate​
The Parliament of TanzaniaMember - Kwahani Constituency
2005​
2015​
Chama Cha Mapinduzi, CCMMember - Kwahani /Mkuranga Political Committee
2000​
To Date​
The Parliament of TanzaniaMember - Mkuranga Constituency
2000​
2005​


NITAMKUBALI SANA KAMA ATAKUWA NI KIONGOZI WA KWANZA WA CCM KUKUBALI KUSHINDWA ; TENA HADHARANI
 
Dodoma ndio machinjio ya wazanzibar????haaaa CCM tunaendeleza usultani kwenye koloni letu zanzibar
 
Back
Top Bottom