Huyu bwana watu hawajuitu. Huyu ni jembe kweli kweli. Watanzania wanapoona nchi yetu imeongeza kasi ya ukusanyaji mapato, pamoja na Kusimamia Miradi yote ya kimkakati basi Dkt Mpango Anahusika.
Hivyo nimpongeze Mama Yetu Samia kwa kutambua mchango wa Dkt Mpango na kweli Atamsaidia sana kwenye kusimamia Utekelezaji wa malengo yote Tuliyojiwekea kama nchi.
Kama angekuwa na mtazamo unaousema hapa Dr. Mpango angefanywa kuwa waziri mkuu. Nafasi ya makamu wa Rais si ya utendaji sana kuliko Waziri Mkuu.
Tuna haja ya katiba mpya kujua majukumu ya watu hawa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu. Kama Rais ni mtendaji mkuu wa serikali, hakuna haja ya Waziri Mkuu. Mfumo sahihi ulikuwa ni kuwa na Rais kama kiongozi wa nchi, na waziri mkuu kama kiongozi wa serikali ya Tanzania Bara na huyu Rais wa Zanzibar kama waziri mkuu huko!! Sasa huko visiwani hata kuna waziri kiongozi na makamu wawili wa Rais. Tuna kazi sana!!