Nashauri asigombee.Nilikuwa napekua makabrasha nikakumbana na kijihabari kwamba Samia alikuwa sekretari wa NGO.
Kiukweli nilifadhaika. Sikutarajia kama angeweza kuwa na kisomo cha hadhi ya NGO.
Na hapa sitaki kubeza. Wala sina lengo la kutweza. Nataka kuondosha mashaka yangu.
Binafsi sijawahi kuona CV ya samia. Nimefukua kila mahali lakini sijaipata.
Naamini baadhi yenu mna CV yake humu. Lakini sijui kwanini mmeificha?
Kuna wanawake wa shoka wako CCM wana CV zina ujazo kweli kweli — Kama Asha Rose Migiro.
Ukizisoma mpaka unatoka udenda wa hamasa.
Lakini hii CV ya samia sijui wameifukia kwenye shimo gani. Hata uitafute vipi huipati.
Hivi ni kweli alikuwa sekretari wa NGO?
Yeyote atakaehusika kuhujumu upatikanaji wa KATIBA mpya itokanayo na Rasimu ya Judge Warioba ndo adui no moja wa Watanzania.
Amen.