Wasifu wa Rais Samia Suluhu Hassan

  • Certificate to Advanced Diploma?
 
Institute,Institute,Institute? Kuna shule kweli hapo?
Watajaribu kurembe mwandiko lakini kiuhalisia pale hakuna shule yoyote na hata kwenye hizo institute bado hakuwa na cha kusema, halafu ile juzi wakati anazungumzia habari ya safari zake akadai "wenye akili ya kawaida ndo wanaolalamika" 😄

Angelikuwa na elimu japo kidogo basi ingetusaidia kama taifa maana kwasasa haelewi asimame na lipi au lipi matokeo yake kaachia watu wajiamulie kila wanalotaka kwa manufaa yao, yeye kazi yake ni kupiga saini tu.
 
Ni kazi iliyolingana na uwezo wake wa kisomo, siyo urais.
Anaupiga mwingi sana na elimu yake inayodharaulika humu ndani. Anao uwezo mkubwa wa kuwasiliana na watu wa mataifa mbalimbali, ni msikilizaji mzuri na anayekubalika kimataifa.

Elimu kuna wakati inakuwa ni mbwembwe tu za kishamba, Steve Harvey hana degree ya aina yoyote ni tajiri mkubwa USA.

Cristiano Ronaldo hana hata diploma, ni tajiri mkubwa anayelisha mamilioni ya watu na kusomesha wasio na uwezo duniani pote.

Punguzeni huu ushamba wa kupapatikia elimu.
 
Elimu yenyewe ya ovyo
Imekua diluted sana hadi haina ladha
 
Utaumia sana, Sasa shule yako hapo wewe mwenye shule inakusaidia nini kama unaongozwa na asie na shule.
Kwamba kila mwenye shule ni lazima atawale? Hivi hizi hoja nyingine huwa mnatoa wapi aiseeh.

Tunajua kwamba tunaongozwa na asiye na shule kwasasa (kama ulivyodai) ila yupo pale kwa mujibu na sio kwa ridhaa ya watz, hakuna Mtz anaejielewa ambaye angekubaliana na hilo swala, maana ndiyo linalotutesa mpaka sasa.
 
Kufananisha swala la kuongoza nchi na swala la kupata utajiri bila kisomo ndio ushamba wenyewe huo.

Kuna vitu vinahitaji elimu bila kupepesa macho, leo hii umpe Msukuma urais kisa anamiliki mali?
 

Lkn Harvey ni Comedian na Ronaldo ni footballer na wamelipwa na kutajirika kwa kazi zao, sijaona ulitaka kumaanisha nini, kwamba unalinganisha Steve Harvey failure yake kwenye Elimu na kushindwa kumaliza Chuo na Raisi wetu au ?

Nijuavyo mimi Ronaldo au Harvey hawaongozi nchi ni watu binafsi, raisi yuko responsible na maisha ya watu zaidi ya milioni 45, hivyo hiyo siyo kamali ni maisha ya watu , na ni sawa kabisa watu hao kuhoji uwezo ikiwa ni pamoja na Elimu ya anayewaongoza!
 
Makapi ya mwendazake bwana.
Jamaa yao aliunga unga masomo wanasema ni msomi kuliko Mama. Kama kweli alikuwa mkemia huko kwenye ualimu alifuata nini?
Kama kweli alikuwa mwanasayansi kwenye siasa alifuata nini? Na ni vipi elimu yake ya kemia imemsaidia?
 
Kufananisha swala la kuongoza nchi na swala la kupata utajiri bila kisomo ndio ushamba wenyewe huo.

Kuna vitu vinahitaji elimu bila kupepesa macho, leo hii umpe Msukuma urais kisa anamiliki mali?
Angekuwa hana elimu asingeweza kuimaliza miradi yote aliyoachiwa na hayati JPM na kuanzisha mingine.

Nimewaongelea hao mastaa wasio na elimu lakini wana pesa nyingi katika kuonyesha ushamba unaotesa watanzania wengi wa kuabudu uprofesa na sifa nyingine za kitaaluma.

Elimu yake ni ya kawaida sana lakini vipi kuhusu wasaidizi wake? na wao hawana elimu. Profesa wa Elimu yule mrombo nae hana elimu?, Ndalichako hana elimu?.

Tuache kuendekeza mada za kipuuzi kama hizi. Wasiokuwa watanzania wanapopitia JF na kukutana na utoto kama huu wanatudharau na kutupuuza sana.
 
Kuna mawaziri na manaibu ni maprofesa na madokta na wamepewa nafasi ya kufanya kazi pasipo kuingiliwa wala kufuatwafuatwa.

PHD ya JPM na yenyewe ilikosolewa na Ben Saanane na wajuaji wengine wa humu jukwaani. Tumuache SSH apige kazi kwani anaiweza sana na amerudisha heshima yetu kimataifa, Ameweza kwa vitendo kuzitetea rasilimali zetu kwa kiwango cha juu sana.
 
Wao wapite tu wajionee ili hata kama kuna kasoro fulani wanaziona kwenye nchi yetu kwa sasa, wasianze ku-guess bila majibu.

Baada ya hii mada , watakuwa na conclusion ya HAKUNA ELIMU.
 

JPM alisomea UDSM na records zipo kama ina mushkeli UDSM wangeshasema huyo Saanane ndo nani hapo UDSM ? Isitoshe kuhusu hao Maprofesa inategemea Bosi wao yukoje, kwa mfumo wa Tanzania hakuna kitu kama kufanya kazi pasipo kuingiliwa kila kitu kinategemea na Raisi aliyeko madarakani hakuna kitu Profesa au expert yoyote atafanya kama raisi siyo, wakati wa JPM watu walipiga kazi tuliona Maprofesa wa Sheria, Kemia wakipigania nchi hata Barrick kukubali kutulipa 300 Million USD, Wahandisi walijenga flyovers wengine walishughulikia Bwawa la Nyerere, reli ya tazara ilitumika kusafirishia mizigo ktk Dar mpaka Site Rufiji kabla ya hapo tazara ilishakufa, reli ya Dar- Moshi-Arusha ilishafufuliwa na kuanza kazi, treni ilifika Arusha yote haya tuliyaona yakifanywa na Wataalamu wetu na mengine mengi tu kama nyumba kujengwa na wahandishi wa Serikali mfano hosteli ya wanafunzi UDSM, mashine za kuhudumia wagonjwa Muhimbili zilifanya kazi na hata Umi Mwalimu ni shahidi na anamkumbuka Magu kila uchwao kwamba walifanya kazi vizuri, Maziwa yote yaliotuzunguka yalijengewa Meli mpaka Ziwa Nyasa na Wataalamu wa Tanzania walitumika, orodha ni ndefu sana , …
 
Hoja mezani ni elimu ya SSH nikasema hao wasaidizi wake ni maprofesa tena walikuwa sehemu ya awamu ya tano.

Angekuwa hafanyi kazi kwa kuzingatia weledi makusanyo TRA yangeshuka, mabenki yangeshindwa kutoa mikopo kwa wananchi.

Angekuwa hana elimu hiyo miradi ya ujenzi wa reli ingesimama mpaka muda huu lakini ndio kwanza SGR inakwenda kumalizika.

Hizi nongwa zote sababu SSH ni mwanamke halafu mzenji, hatukutegemea JPM kama angefariki hivyo hata urais wa Samia kwa mujibu wa katiba unaonekana kama ni wa bahati mbaya. Kuna watu walishajiweka katika nafasi za kiutawala kuanzia awamu ya tano hao hawawezi kukubaliana na ukweli kuwa mambo yamebadilika na ni kwa mapenzi ya Mungu mwenyewe sio ya binadamu.
 

Ana mwaka 1 madarakani kila kitu bado ni masalia ya Uongozi wa Magu, uraisi wake utaanza kuonekana kuanzia 2024/25, hakuna kitu kipya alichokianzisha uniondoa madarasa ya mkopo wa World Bank na imf!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…