Baba yake ni marehemu Mzee Suluhu Hassan.
Kaka yake ni Rashid Suluhu Hassan.
Dada yake ni Mgeni Suluhu Hassan.
Kwa mujibu wa makala hii ya BBC.
---
Akiwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya urais nchini Tanzania, Watanzania wamekuwa na hisia na mitazamo mbalimbali juu yake.
Lakini familia yake na watu wake wa karibu wanamfahamu vizuri kuliko ilivyo kwa watu wengine .
Rashid Suluhu Hassan ni kaka wa Rais Samia anasema jitihada anazozionesha hii leo , alianza tangu akiwa mdogo.
''Alikuwa mtu ambaye ana ari ya kusoma, bidii ya kusoma, alikuwa anapenda kuambiwa soma uwe kama mtu fulani, unamuona kaka yako hapa kwasababu Baba yetu alikuwa mwalimu, hivyo openness alikuwa nayo tangu zamani sana kwa hiyo watoto wake alikuwa akiwaachia nafasi''. Alisema Bw. Rashid.
Kaka yake anasema hakuna yeyote kwenye familia aliyewahi kuwa na ndoto kuwa siku moja atakuwa kiongozi...
''Hakuna mtu alijua.. kama ingewezekana kumfufua marehemu Mzee Suluhu sasa hivi akaamka ukamwambia leo Samia ni rais atakushangaa sana''. Alisema Bw. Rashid
Mgeni Suluhu Hassan ni dada wa Rais Samia anasema hakutarajia mdogo wake kushika nafasi ya juu kabisa ya uongozi nchini Tanzania.
Lakini pia hakushangazwa pia kutokana na rekodi yake ya kushika nafasi mbalimbali akipanda hatua kwa hatua.
''Kapita kwenye nyanja nyingi akianza tangu chini kabisa, mpaka akawa mbunge, kaliongoza bunge la katiba pia, anaweza na anajitahidi kuweza na ataweza''.
Tumsaidie na kumshauri vizuri.'' alisema Bi.Mgeni
Chanzo cha picha, Ikulu Tanzania
Chanzo: BBC
Akiwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya urais nchini Tanzania, Watanzania wamekuwa na hisia na mitazamo mbalimbali juu yake. Lakini familia yake na watu wake wa karibu wanamfahamu vizuri
www.bbc.com