Wasifu wa Rais Samia Suluhu Hassan

Wasifu wa Rais Samia Suluhu Hassan

Mkuu Kalamu uwezo wako wa kiuchambuzi ni mkubwa zaidi ya ulichokiandika hapa......

Mh.Rais SSH kwao ni Kizimkazi....amepita katika machujio ya kizalendo kufikia hapo alipo.....wamakunduchi ni wahadimu Kutoka huku bara... wamakunduchi wanajulikana kwa umakini wao na kuupenda uafrika.....wamakunduchi wanajulikana kwa UKOMREDI wao juu ya CCM......

Mh.Rais SSH ameshawahi kuwa mkurugenzi wa NGO's Zanzibar.....ameshawahi kuwa waziri wa utalii.....ameshawahi kuwa waziri wa muungano wa JMT......unadhani ni kwa bahati mbaya?!!!

Huyu mama yetu ni zaidi ya umuonavyo na umjuavyo....ni komredi haswa....kwake Tanzania kwanza kabla ya nafsi yake......

Wanaomjua watakuwa wanaisoma comment hii kwa furaha kubwa.....

#Aishi Milele Chifu Hangaya amen[emoji120]
Nimekusoma kwa makini na heshima kubwa.
Ngoja niishie hapo kwa sasa.
Niseme tu kwamba hizo sifa ulizoweka hapo zinajadilika, na siyo kigezo tosha cha kuwa hapo alipo sasa.
 
Siyo mimi, nilijazia tu kinachowezekana kufanywa kwa uelewa nilionao juu ya hayo mliyojibishana wenyewe.
Hakuna mtu anayeweza kwenda kuchimbua hilo kaburi kwa sababu hiyo, labda tuongee kwa kufurahisha baraza kidhahania tu hapa.
 
Hakuna mtu anayeweza kwenda kuchimbua hilo kaburi kwa sababu hiyo, labda tuongee kwa kufurahisha baraza kidhahania tu hapa.
Binafsi hayo siyajui mkuu 'Kiranga', mchango wangu uliishia kwenye hiyo DNA kama wenyewe wakitaka kufanya hivyo.
 
Baba yake ni marehemu Mzee Suluhu Hassan.

Kaka yake ni Rashid Suluhu Hassan.

Dada yake ni Mgeni Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa makala hii ya BBC.

'Rais Samia alipenda kusoma, baba yetu alimhimiza afaulu’. Familia yake yaeleza​

  • Halima Nyanza
  • BBC Swahili
20 Aprili 2021
---

Akiwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya urais nchini Tanzania, Watanzania wamekuwa na hisia na mitazamo mbalimbali juu yake.

Lakini familia yake na watu wake wa karibu wanamfahamu vizuri kuliko ilivyo kwa watu wengine .

Rashid Suluhu Hassan ni kaka wa Rais Samia anasema jitihada anazozionesha hii leo , alianza tangu akiwa mdogo.

''Alikuwa mtu ambaye ana ari ya kusoma, bidii ya kusoma, alikuwa anapenda kuambiwa soma uwe kama mtu fulani, unamuona kaka yako hapa kwasababu Baba yetu alikuwa mwalimu, hivyo openness alikuwa nayo tangu zamani sana kwa hiyo watoto wake alikuwa akiwaachia nafasi''. Alisema Bw. Rashid.

Kaka yake anasema hakuna yeyote kwenye familia aliyewahi kuwa na ndoto kuwa siku moja atakuwa kiongozi...

''Hakuna mtu alijua.. kama ingewezekana kumfufua marehemu Mzee Suluhu sasa hivi akaamka ukamwambia leo Samia ni rais atakushangaa sana''. Alisema Bw. Rashid

Mgeni Suluhu Hassan ni dada wa Rais Samia anasema hakutarajia mdogo wake kushika nafasi ya juu kabisa ya uongozi nchini Tanzania.

Lakini pia hakushangazwa pia kutokana na rekodi yake ya kushika nafasi mbalimbali akipanda hatua kwa hatua.

''Kapita kwenye nyanja nyingi akianza tangu chini kabisa, mpaka akawa mbunge, kaliongoza bunge la katiba pia, anaweza na anajitahidi kuweza na ataweza''.

Tumsaidie na kumshauri vizuri.'' alisema Bi.Mgeni

Chanzo cha picha, Ikulu Tanzania

Chanzo: BBC

BBC ndiyo watupe uasili wa Rais wetu wa Tanzania aibu hizi.
 
Nimekusoma kwa makini na heshima kubwa.
Ngoja niishie hapo kwa sasa.
Niseme tu kwamba hizo sifa ulizoweka hapo zinajadilika, na siyo kigezo tosha cha kuwa hapo alipo sasa.
Niko bize na matayarisho ya fainali ili kuhakikisha kuwa Tanzania siyo "kichwa cha mwendawazimu tena", nitarudi baada ya fainali.
 
Niko bize na matayarisho ya fainali ili kuhakikisha kuwa Tanzania siyo "kichwa cha mwendawazimu tena", nitarudi baada ya fainali.
Mbona utakuwa umechelewa mkuu! AU nimesoma visivyo? Mtayarishaji ni lazima uwepo wakati wa "fainali" kuhakikisha kila kilichotayarishwa kinakwenda kama kilivyokusudiwa.

Nchi hii tumewahi kuwa na mipango mizuri sana, lakini tumekuwa mafundi wa kupindisha, ndiyo maana tunakwenda zigzag namna hii kwa sasa.
 
.......unataka tukawafukue makaburini muwahoji?!!!
hatuwezi kufukua makaburi, yeye mwenyewe asimame ahesabiwe, unless ukweli hata yeye haujui

niliomba kuhuisha passport mwaka juzi, nikatoa kadi ya NIDA ikawa haitoshi, nikaingizwa kwenye chumba cha maofisa wa uhamiaji ofisi ya Wilaya, nikahojiwa chimbuko langu, kabila, ubini, mila na desturi, nikaitiwa jamaa anaelijua kabila langu na vijiji vyetu kunihakiki, akaridhika

mimi ni raia namba milioni 58 nukta 7822, chimbuko langu na uraia wangu umehojiwa mbele ya vyombo vya umma. Kwa nini raia namba moja chimbuko lake na uraia uwe kitendawili mbele za umma?
 
Mbona utakuwa umechelewa mkuu! AU nimesoma visivyo? Mtayarishaji ni lazima uwepo wakati wa "fainali" kuhakikisha kila kilichotayarishwa kinakwenda kama kilivyokusudiwa.

Nchi hii tumewahi kuwa na mipango mizuri sana, lakini tumekuwa mafundi wa kupindisha, ndiyo maana tunakwenda zigzag namna hii kwa sasa.
Problem ya Tanzania iko kwenye katiba hasa huko CCM kuhusu utaratibu wa kumpata mgombea mwenza ambaye hupangwa na kamati ya CCM baada mgombe a kufuzu. Mgombea Mweza hupat free ride bila kuchujwa na wananchi. Kwa mfano ukiwa na Mgombea ambey ni 80% halafu akapatikana mgombea mwenza ambaye ni 15% basi tiketi hiyo itapita, sasa tatizo ni pale yule 80% mgombea akifariki basi huyu 15% ndiye anshika madarak. Very tricky!

Nitajibu kwa makini baada ya fainali; niko bize na fainali za CAF.
 
Siri gani na wazee wako makaburini?!!! Wakafukuliwe wahojiwe?!! [emoji15][emoji1787][emoji1787]
Kwani wapi uliona siri ya serikali ikahojiwa kwa nini imekuwa siri na ndo waliomficha babu yetu mzazi wa namba moja wetu nao hawataki tuwahoji ...,..mpaka Leo hii hakuna sehemu wameandikwa wala kuonyeshwa Baba wala Baba wadogo wala akina Baba wakubwa wa namba moja wetu,yaani ni km vile kizazi choote cha babu yetu kilikumbwa na gharika au kuzama majini na kufutika choote
 
Naona mods wameamua kuunganisha Uzi na mwingine ilhali haifanani hata maudhui
 
Back
Top Bottom