Wasimamizi Yanga Day Ovyo Kabisa

Wasimamizi Yanga Day Ovyo Kabisa

Ndugu mshabiki,ulienda uwanjani kwa raha zako,umefurahi kwa raha zako,ilipofikia hatua ukakereka ungeondoka kwa raha zako na ungebakia na raha zako.

Halafu nyakati zijazo mnakuja kuuliza kwanini mashabiki ni wazito kwenda viwanjani kusapport timu zao.

Huu ndio wakati sahihi wa kurekebisha makosa au mapungufu yaliyojitokeza.
 
Hata mimi kiukweli sijafurahishwa na mambo kadhaa kwenye tamasha la jana;

1. Kupangwa siku ya Jumapili, badala ya Jumamosi! Na hii ni kutokana na ukweli kwamba baadhi ya mashabiki wanatokea Mikoani, na usikute ni wafanyakazi! Sasa unarudi vipi Mkoani na kuwahi kazini?

2. Mchezo wa kuhitimisha tamasha kuanza saa tatu usiku! Wakati mwingine nashauri mchezo uanze kati ya saa 11 - 1 jioni, ili watu waondoke mapema kurudi majumbani kwao. Sidhani kama kulikuwa na sababu ya msingi ya kuanza saa tatu usiku.

3. Hajji Manara adhibitiwe. Huyu kiumbe akiendelee kuachwa afanye anavyotaka; bila shaka kuna siku watu watasusa kuhudhuria hilo tamasha. Haiwezekani mtu mmoja ajione ana haki ya kufanya chochote anachojisikia hata kama ni kitu cha kipuuzi! kwenye kundi la watu elfu 60+.
Baada ya Mzee Kikwete , Sunday Manara ,Mzee Magoma anaefuata ni wewe.

Naona sasa angalau wenye akili mmekuwa wanne pale Yanga .

Mkuu , kwenye ukweli huwa unanyoosha . Huna kabaya .
 
Watamuogopa hadi lini?

Sipo kuharibu ugali wa Manara, ila wakati wa kudeal naye ni sasa kabla hajajiona ni kila kitu pale Yanga.

Huyu jamaa ukimpa freedom tu, anafanya anachotaka na ana ushezi mwingi sana.
Na Manara hashauriki hata kidogo. Alishajiona anajua kila kitu na hakuna wa kumuuliza Wala kumpangia chochote
 
Mkoo busy kuongelea matukio ya Yanga Day ila baada ya tarehe nane mtaanza kuongelea matukio yenu. Huku mkikumbushia bil 20 na kuanza kuyatafuta maduka.
 
Mechi ilitangazwa itakuwa saa mbili usiku, sasa hapo kwa akili za kawaida mechi itaisha saa ngapi?

Well. Mechi imeanza saa ngapi Mkuu?

Au ndio tumeamua kutetea kila kitu kwa maslahi ya Club? [emoji1]
 
Wenye timu yetu wala hata hatujakasirika. Mimi nilifurahi sana mechi kuisha saa 5 usiku kwa sababu nilijitwalia zangu katoto ka mwaka 2006 kama soma VETA na Mimi nikaonjamo..

Sema hii Klabu masuala ya kula nyapu mmeweka kipaumbele sana.

Ndio maana hata tukio la Mobetto lilipewa nguvu sana.

By the way, sidhani kama unaweza eleza kama hilo jambo lako kama ni faida kwa umma( Wananchiiii).
 
Mkoo busy kuongelea matukio ya Yanga Day ila baada ya tarehe nane mtaanza kuongelea matukio yenu. Huku mkikumbushia bil 20 na kuanza kuyatafuta maduka.

Tunazungumza mambo ambayo yametokea sasa, hayo mengine yana wakati wake.

Muda sahihi ukifika tutazungumza tu. Mazuri kwa mabaya. Pongezi na malalamiko.
 
Well. Mechi imeanza saa ngapi Mkuu?

Au ndio tumeamua kutetea kila kitu kwa maslahi ya Club? [emoji1]
Mm cjui mechi imeanza saa ngap mana hua sifatilii, ila kama mechi mkitangaziwa inaanza saa mbili usiku c unajua kabisa hapo itaisha saa ngapi au?
 
Tunazungumza mambo ambayo yametokea sasa, hayo mengine yana wakati wake.

Muda sahihi ukifika tutazungumza tu. Mazuri kwa mabaya. Pongezi na malalamiko.
Kipi umekiona ww cha ajbu mpaka mnakuza.Subiria baada ya tarehe nane nazani mtapata vya kuongea vitakavyokuwa vinawahusu nyinyi.
 
Ilitangazwa itaanza saa mbili ikaanza zaidi ya sasa tatu usiku. Saa Moja na zaidi mbele. Je ni sawa?
Ratiba
20240806_130444.jpg
 
Mm cjui mechi imeanza saa ngap mana hua sifatilii, ila kama mechi mkitangaziwa inaanza saa mbili usiku c unajua kabisa hapo itaisha saa ngapi au?

Mechi ilipaswa kuanza saa mbili kamili, lakini imekuja kuanza saa tatu na nusu ambapo kwa muda huo mechi ingekuwa ukingoni ukingoni Mkuu.
 
Mkoo busy kuongelea matukio ya Yanga Day ila baada ya tarehe nane mtaanza kuongelea matukio yenu. Huku mkikumbushia bil 20 na kuanza kuyatafuta maduka.
Kwamba mashabiki wa Yanga hamuoni tatizo kabisa??

Hivyo, kila anayekosoa tamasha lanovyo la Yanga na upumbavu wa Kalikonji Manara hapa ni Simb?

Yaani Kalikonji Manara ni Yanga damu kuliko mashabiki wa Yanga tunaoshauri hapa??
 
Mechi ilipaswa kuanza saa mbili kamili, lakini imekuja kuanza saa tatu na nusu ambapo kwa muda huo mechi ingekuwa ukingoni ukingoni Mkuu.
Mbona kwenye ratiba iliyowekwa juu inaonesha kuwa mechi ni saa mbili na nusu hadi saa tatu na dakika 15 ndio muda wa kuanza?
 
Back
Top Bottom