Wasimamizi Yanga Day Ovyo Kabisa

Wasimamizi Yanga Day Ovyo Kabisa

Umesema mwenyewe kuwa haya mambo yanajadiliwa kishabiki.

Naamini ukitoa ushabiki, huwezi zungumza haya mambo uliyozungumza mkuu.
Shabiki wa simba anaipindea show ya yanga vivyo hivyo kwa shabiki wa yanga.
Ni waelewa wachache ambao wako nje ya box la ushabiki, wengi mmexamia humo.
 
Manara yupo yanga sababu ya gsm na ni balozi wa bidhaa zao halafu huwezi kumfananisha huyo meneja na mtu maarufu kama haji manara
Haji manara akisema jambo linakuwa na uzito mkubwa kuliko angesema mtu mwingine wa kawaida
Mtu wakawaida anakuwaje?
 
Wenye timu yetu wala hata hatujakasirika. Mimi nilifurahi sana mechi kuisha saa 5 usiku kwa sababu nilijitwalia zangu katoto ka mwaka 2006 kama soma VETA na Mimi nikaonjamo..
 
Tayari tumewazoea, ila hatukujua kama hamjabadilika.

Hakuna tamasha la Siku ya mwananchi liliwahi tamatika bila vituko, malalamiko au majonzzi katika miaka ya hivi karibuni. Mwanzo tuliamini bado ni wachanga katika matukio makubwa kama haya. Ila umefanya matukio kama haya zaidi ya mara tano kwanini hakuna mabadiliko?

Leo sasa, ukitoa tamasha kuendeshwa kiswahili swahili(very unprofessional) kuna mambo mengi ni ngumu kuelewa.

1. Suala la ratiba, hii ni kichekesho watu wameanza kuingia saa tatu, unakuja kuwatoa saa tano dakika 20 usiku? Siku ya jumapili na kesho ni shule na makazini?

2. Hivi Haji Manara na kundi lake ni kitu gani walikua wanafanya pale? Mazoea au Jeuri, wamevunja protocal nyingi plus unnecessary drama hadi kero.

3. Show kuwa chini ya kiwango, hivi Harmonize amefanyaa show bure? Sijaona zaidi ya washa tochiii.. Marioo nao ni wale wale poor, very poor.

4. Yuko wapi Ali Kwamwe? Heshimuni sana jitihada za huyu kijana.

Na mengine mengi.

Kipi kimekufurahisha au kukukera siku ya leo?
Umeandika ya kweli hakika, ila mimi hili la huyu bwana mdogo Kamwe ndilo limenisikitisha sana.

Yanga na hasa ndugu Hersi (nimesitisha kukuita "injinia" au kuweka "Eng") jitahidini sana kuondoa huo uswahili swahili uliopo hapo.
 
Usitegemee makubwa toka kwa Yanga, ile ni timu ya Kiswahili na ndiyo maana mambo yao ni ya Kiswahili swahili tu siku zote.

Hii ni changamoto kubwa sana upande wao.

Labda kuna siku watamka. Nje ya hapo tutaenda kutia aibu huko mbeleni kama taifa, maana tayari wameanza kufuatiliwa na watu wa mataifa tofauti tofauti.
 
Harmonize & Manara waliingia wakiwa wamelewa ... Na uchawa wa Kitenge na Zembwela ukaharibu kila kitu .

Ni changamoto sana.

Kwenda kwenye tamasha kama hili umelewa sijui ni dharau, kiburi ila wanawaangusha sana Wananchi
 
Hata mimi kiukweli sijafurahishwa na mambo kadhaa kwenye tamasha la jana;

1. Kupangwa siku ya Jumapili, badala ya Jumamosi! Na hii ni kutokana na ukweli kwamba baadhi ya mashabiki wanatokea Mikoani, na usikute ni wafanyakazi! Sasa unarudi vipi Mkoani na kuwahi kazini?

2. Mchezo wa kuhitimisha tamasha kuanza saa tatu usiku! Wakati mwingine nashauri mchezo uanze kati ya saa 11 - 1 jioni, ili watu waondoke mapema kurudi majumbani kwao. Sidhani kama kulikuwa na sababu ya msingi ya kuanza saa tatu usiku.

3. Hajji Manara adhibitiwe. Huyu kiumbe akiendelee kuachwa afanye anavyotaka; bila shaka kuna siku watu watasusa kuhudhuria hilo tamasha. Haiwezekani mtu mmoja ajione ana haki ya kufanya chochote anachojisikia hata kama ni kitu cha kipuuzi! kwenye kundi la watu elfu 60+.

Umenena vyema. Kudos Mkuu
 
Gsm wanamuogopa manara wanajua wakimchinjia baharini ataitisha press na kuanza kuwaanika km alivyomfanyia mo dewji.

Inakuwa kama ile hadithi ' nani wa kumfunga paka kengele? Wanakosa ujasiri wa kumwambia hahitajiki yanga
Na tokea arudi hana alichoongeza zaidi ya drama tu!

Watamuogopa hadi lini?

Sipo kuharibu ugali wa Manara, ila wakati wa kudeal naye ni sasa kabla hajajiona ni kila kitu pale Yanga.

Huyu jamaa ukimpa freedom tu, anafanya anachotaka na ana ushezi mwingi sana.
 
upande wa protocol alikuwa hovyo

hivi Mangungu alitambulishwa ?

Yes Mangungu alitambulishwa.

kuhusu protocol jamaa alijitahidi sana kwa kufuata itifaki na bila kuacha mtu au taasisi muhimu.
 
Back
Top Bottom