Show imefunika vibaya mno, watu hawakumbuki kabisa kama jana tu ilikuwa Simba day! Kila kitu kilikuwa super mwake mwake babake!! Yanga inatisha kwenye show za kibabe, dunia nzima imeona na kushangaa jinsi Yanga inavyoshinda kila kitu hadi matamasha na mafataki!!
Vitu vilivyowauma sana makolo ambavyo hawana ni wananchi kuvaa uzi mpya uwanja mzima jana zilikuwa kauka nikuvae jezi za zamani mashabiki wa Simba hawana hela ya jezi, makombe matatu makali, mashabiki kujaza viwanja viwili ni maajabu, nongwa za Manara kutambulisha dada zake wa ikwiriri, mrembo Mobeto kuvalishwa jezi na Ki Aziz , kiongozi mkubwa sana kupewa kadi, gari kali la Kitenge, show bab kubwa ya Marioo na Harmonize na ile show kabambe ya half time, mpira kama Real Madrid msako mkali mwanzo mwisho timu ina muunganiko, goli la dhahabu la Mudathir, chenga hatari za Pacome na penati ya karne ya Ki Aziz kipa kaenda sokoni na mengineyo.
Makolo muwe mnaanza tamasha lenu kila siku sisi uto tunamalizia na kuwapoteza!!