Jicho la Tai
JF-Expert Member
- Oct 10, 2012
- 1,450
- 600
Katika zoezi ambalo linaendelea la Anwani za makazi, hata linalokuja la sensa, tunaiomba Serikali itumie watu wasio na ajira badala ya kuwatumia watumishi ambao tayari wana kipato.
Serikali inapaswa itumie watu wasio na ajira katika zoezi la anwani za makazi pia sensa ili kusaidia vijana wasio na ajira waweze kupata ajira za muda lakini pia itawawezesha kupata hata mitaji midogo kwa ajili ya kuanza biashara ndogondogo ama shughuli za kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.
Kuwapa ajira hizi watumishi kwa kigezo chochote kile itasababisha watu wa chini wasio na ajira wasiinuke lakini pia watumishi hawa wa umma wakienda kufanya hizi kazi utendaji wa serikali utapungua.
1. Kigezo cha Uzoefu: Watumishi hawana uzoefu na Anwani za makazi. Ndio maana kuna mafunzo yanatolewa kabla ya kazi, lakini pia wataalamu wa mambo wengi kwa sasa wako nje ya mfumo wa ajira (As we know mazoezi yote haya yanahitaji uelewa zaidi wa Technolojia)