Wasioishiwa pumzi ya kuupinga ufisadi tunakutana hapa!

Yaani una shangaa kabisa kwamba mtu anasema kwamba hata kama ni mwizi tuna mtaka huyohuyo!! Yaani unajua kabisa ni fisi ila unataka umpe banda la nyama kweli!

ACT pekee ndio ina hoja muimu wengine wote wana tukanana tu

Tunampenda hivyo hivyo
 

Attachments

  • 1444819427572.jpg
    70.5 KB · Views: 96
Lowasa sio fisadi



mimi nataraji kuwa kama mwalimu angekuwepo leo hii kuna watu wangechezea bakora ile mbaya.
 

Huyo huyo mwaribifu anatufaaaaaaaa
 
Huyo huyo mwaribifu anatufaaaaaaaa

Tatizo unaonekana umekariri na kufikiri hii ni Bongo Star Search. Uzuri unawakilisha asilimia ndogo ya wapiga kura. Ila asante kwa kutushtua kuwa elimu ya raia muhimu!
 
Dah! Kwanini nimechela kuiona thread hii!!

Posha!!!! Inanihusu hii, Mimi kwa sasa sina kadi ya chama chochote (tangu niichane chane kadi ya CDM) lkn nawaunga mkono ACT.

Na ungana na wale wote wanaopinga ufisadi nchini, ktk hili sintabadilika mpaka naingia kaburini.
 

Wawezaje kukanusha ukweli usiojificha????
 
Wawezaje kukanusha ukweli usiojificha????

Hilo tope walilojipaka kina lissu,Mbowe,Msigwa na Mnyika litawatafuna kama jamaa anayegombea kupitia UKAWA leo hii.wao wanadhani litapita tu na sisi tutaeachekelea
 
Mabadiliko ya KWELI yataanzia Bungeni na siyo IKULU. Kama kuna mtu anadhani Lowassa ataleta mabadiliko basi ni au hajui nini maana ya Bunge au anajua (kama mimi) ila tu tunataka kumtumia Lowassa kuongeza nguvu ya kupata wabunge wengi zaidi wa upinzani.
Dr Slaa alisaidia sana mwaka 2010 kwa kugombea Urais. Umaarufu wake wakati ule ulikuwa chachu ya Chadema kuvuta Wabunge wengi. Lowassa na ugonjwa wake, na ufisadi wake, kaweza kuwaunganisha UKAWA dakika za mwisho. Lipumba alikuwa atoe pigo la mwisho la UKAWA ila kuja kwa Lowassa, kulisaidia sana.
Lowassa unaweza ukamchukua kwa mabaya yake yote ila dakika za mwisho, amini usiamini ndiye kasaidia upinzani usisambaratike. Delila angelifanya vitu vyake dakika ya mwisho , tungelia na kusaga meno.

Maadamu Lowassa simpendi, sasa kwa nini namshangilia? Jibu ni rahisi: Asaidie kuwaunga UKAWA kupata wapinzani wengi. Mungu Ibariki Tanzania.

Sasa tujikite kuongeza wabunge wa upinzani tuachane na hii failed project ya 2015! Naamini tupo pamoja katika malengo ila approach ndo tumetofautiana!
 
Chadema iliongezaje viti vya serikali za mitaa?

Tusitafute justification za ufisadi uliofanyika Ukawa...watu wamechukua mpunga wakaja na matokeo ya utafiti feki kuwa Slaa kachuja ha ha ha...

Ungeniambia mabadiliko ya kweli yanaanzia kwenye mitaa na udiwani labda ungekuwa na mantiki.

CCM/TANU haikupewa nchi wakiwa kama genge bali kama taasisi inayojitambua.
 
meningitis kelele peke yake hazitoshi bali hizo ni kampeni nje ya uwanja wa siasa za kuwachafua watu. kama kweli hii ni thread ya wapinga ufisadi na wachukia ufisadi basi na iwe darasa mahsusi kwa wote kwanza wafahamu nini maana halisi ya ufisadi na unabebwa vipi kwenye katiba na sheria za nchi. wajifunze nini hatua za kuchukua kuwezesha kuukomesha na nini mpiga kelele anacho kama ushahidi usio na shaka utakaotuwezesha kuwafungulia mashtaka mafisadi na serikali ishinde kesi. kwa kuanza kuchezesha mpira mimi nitazungumzia ufisadi uliofanyika wakati wa zoezi ove la uuzwaji nyumba za serikali ambapo ndani yake viongozi waligawa nyumba hizo kwa ndugu na vimada.huu ndio ufisadi wa mwanzo kujadiliwa ili sasa yale magazeti ya rai na mtanzania yaliyoanika ushahidi wa dhahiri dhidi ya vitendo hivyo yatusaidie kama sehemu ya ushahidi wa kuwafikisha wote waliohusika kwa namna moja ama nyingine katika ufisadi huu. baada ya hapo tujadili fisadi nyinginezo kama richmond, epa, escrow; meli ya samaki, twiga waliotoroshwa pamoja na vijisenti vya waziri mmoja
 

ESCROW ndio ilisaidia CHADEMA kupata viti vingi kwenye serikali za mitaa baada ya hapo Watanzania tukasahau ndio maana hadi muda huu watu wanazungumzia ufisadi wa UZWAJI WA NYUMBA ZA SERIKALI NA RICHMOND TU.
 
kabla hamjakanusha ukweli mnaodai usiojificha kwanza muwatake wale wote waliopata mgao wa escrow kutoka kwa harbinder singh pale standard chartered waanze kukanusha tuhuma zilizozagaa awali kabisa kila kona ya nchi mpaka nje ya nchi. mkishindwa kuwataka wafanye hivyo na wakishindwa kutoa maelezo sadifu basi tutakuwa tumetenda haki kama tukiwaongeza kwenye list ya wazushi na warongo
Wawezaje kukanusha ukweli usiojificha????
 
jingalao huu ujinga mlioufanya wa kumlisha marehemu baba wa taifa maneno ambayo kamwe hakuyatamka na hayapo kabisa katika kumbukumbu zake zote utawatokea puani pale TCRA watakapowataka mupeleke uthibitisho


mimi nataraji kuwa kama mwalimu angekuwepo leo hii kuna watu wangechezea bakora ile mbaya.
 

Mkuu nimeupenda ushauri wako kuhusu kuwa na common understanding ya nani hasa ni fisadi au ufisadi ni kitu gani.
Hilo litaboreshwa kadri siku zinavyoenda.

Naamini tukiwa na uelewa wa pamoja tutakuwa na uwezo wa kutofautisha fisadi anayekataliwa na magwiji wa ufisadi nakukubaliwa na waliojiita wapinga ufisadi versus yule anayekubaliwa na magwiji wa ufisadi na kupingwa na wanaojiita wapinga ufisadi.

Mkuu jisikie huru kushusha nondo zote ili kila anayetajwa humu iwe halali yake kweli.Jitahidi kama mimi ninavyojaribu hapa kutokuwa biased.

''be as wise as the serpent you encounter''
 

Naona mkuu unakuja kwenye njia sahihi.
Kwenye uchaguzi huu hatukutakiwa kupotezwa kwenye ajenda ya msingi ya kuwakataa kwa sababu ni mafisadi.

Nilitegemea Chadema na pengine Ccm iteue wagombea wake kwa kuzingatia uadilifu hasa hasa eneo la ufisadi.

Nilitegemea mwaka huu wa uchaguzi kuwa ni hukumu kuu ya wote wanaotuhumiwa kuwa mafisadi.

Sasa kuna mtu ghafla ghafla katutoa kwenye ajenda hiyo na kuifanya kutojadilika au kuifanya ya kawaida sana.

Sijayasikia haya mawe ya escrow,nyumba,epa,richmond yakivuma mara baada ya julai 28.

Madhara ya jambo hili sio madogo,sasa hivi hakuna anayemkumbuka 'tumbili' ambaye amefunguliwa kesi.

Mafisadi wamepata nguvu baada ya kuwa mapilot wa ndege iliyokuwa ituvushe dhidi ya ufisadi.

Ndio maana nakuja na hoja hii ya kutokuishiwa pumzi kamwe kwani kwa kufanya hivyo ni kukaribisha mikandamizo zaidi kutoka kwa mafisadi.

Na siku moja wajukuu watakuwa wanapiga viboko makaburi yetu.
 
Mleta mada hata wewe kwenye eneo lako la kazi utakua unafanya ufisadi indirectly
 
Ndiyo maana nilikuambia kuwa CCM walishammaliza Dr Slaa kwani sifa pekee aliyokuwa anajulikana nayo ni UFISADI.

Waliruhusu makusudi Ufisadi usemwe wazi na mzigo wote akabebeshwa Lowassa wakati siyo kweli.

Ukiniambia Escrow Lowassa alilamba ngapi? Ntailipia kadi yangu ya CCM. Ukiniambia fedha zilizopotea Wizara ya Magufuli Lowassa alikula ngapi? Tatizo lenu ni kutufanya hatuna akili kwa kutulisha upuuzi wenu kuwa Fisadi ni Lowassa peke yake. Nchi ni giza, miaka 10 ya Kikwete bado anaiacha nchi giza. Lawama apewe Lowassa aliyeondoka miaka 8 iliyopita.

Slaa alishapoteza umaarufu wake kwa namna moja au nyingine. Asingeliweza kushindana na CCM hata kidogo. Na ili kuonyesha hilo, serikali za Mitaa, Chadema walifanya vibaya sana. Hata wewe umelijua hilo na umeliandika hapa kwenye BOLD. Sasa ili kutibu hilo tatizo, LOWASSA kaja na kibao kimegeuka. Mnahemewa Kisogoni kwa mara ya kwanza.

Hata kwa Mbinde, safari hii lazima Lowassa awachukue.

https://www.youtube.com/watch?v=mnAlHuGWOFg

 
Dr Slaa aingie kwenye list of shame maana amekubali kutumia na wazazi wa UFISADI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…