Pre GE2025 Wasira ametudanganya. Samia Kajiteua mwenyewe akisaidiwa na Kikwete sababu hatujui wana CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Makamba? Nitakua mtu wa mwisho kuamini hilo kaka. Makamba katolewa kwenye cabinet kimkakati, sio bahati mbaya. Mpina pia nina wasiwasi, wanaweza kua wanataka atoke au atolewe kabisa kibabe BUT kauri na misimamo ya Mpina kwa Watanzania ni habari nyingine, halafu Mpina anatokea kanda ya ziwa, eneo lenye wapiga KURA wengi kuliko kanda yoyote bongo. Ukitaka kushinda uchaguzi kirahisi, jenga jina kule, tafuta kukubalika kule, kanda zingine zina wapiga kura wachache na zingine ni ngome za ccm for years, hawahitaji kufanya kampeni. Watu kama wangoni kwamfano, utawaambia nini na ccm yao? Mikoa ya pwani je? Something, kanda ya ziwa kama ilivo nyanda za juu kusini (though hawa nao wapo wachache ) siasa zao zinabadirika badirika, ukiwaletea za kuleta, unakula za uso. As we speak, kabla ya November Sugu alikua na uhakika wa kushinda ubunge Mbeya, sasa hivi baada ya watia Nia kwa nafasi ya uenyekiti wa Chadema na kila mtu kua na upande either wa Mbowe au Lissu, tayari Sugu hana uhakika wa kushinda Mbeya. Again baada ya uchaguzi hu tena, Iringa nayo haitabiriki, kabla ya November 2024, ccm walikua na uhakika wa kushinda, now sidhani, upepo umekwisha badirika. Mikoa ya pwani wala
 
Hivi mnategemea ccm na wana ccm waseme ukweli upi?
Kwa kuwa si wanyoofu, wana wa giza na hadaa wanaipuuza kweli na kuwarubuni Wadanganyika.
 
Huyu Mzee amelikaribia kaburi badala ya kutengeneza mambo yake na Mungu,ndio kwanza anakimbilia kwa shetani.
 
Ikiwa hakuna mtu alisimama na kupinga hapo mkutanoni basi Ina maana wote waliridhia matokeo ya uchaguzi.
Hata lusinde aliposema wanaounga mkono hoja yake wasimame, karibu ukumbi mzima walisimama. Bendera fata upepo, sina hakika kama hata wanajua wanahitaji nini.
 
Chadomo na Suku gang hii inawahusu 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DFSQVJktKNH/?img_index=1&igsh=OTh1dnczOHMxZzl1
 
Nafahamu Lissu anakubalika sana kanda ya Ziwa , na mikoa ya Umasai Kilimanjaro, Arusha, Manyara hasa wafugaji
 

View: https://x.com/Hakingowi/status/1883511122378014837?t=qEoibmhfgDIBLzk72EfZXw&s=19
 
Ajenda ya kumpitisha mgombea wa kinyang'anyiro cha nafasi ya urais na ile ya mgombea mwenza kwa chama chochote kile ni mahususi sana, na tena huwa inahitaji uwepo wa mkutano wake mkuu wa kipekee kutokana na kalenda ya vikao vya chama ndani ya mwaka wa uchaguzi.

Licha ya uwepo wa utitiri wa ajenda za kikao cha Mkutano Mkuu, ajenda ya kupitisha jina la mgombea wa nafasi ya urais huwa ni ajenda kubwa kuliko zote. Kutokana na unyeti wake, haitazamiwi kwa vyovyote vile uwepo wa mizengwe yenye kupelekea hali ya ukakasi ili kupitisha jina la mpeperusha bendera akiwa na jukumu kubwa la kuinadi ilani ya chama. Mchakato mzima ni lazina uendane na masharti ya katiba ya chama, kanuni muhimu, na kwa kuzingatia taratibu nyingine muhimu.

Mkutano huu mkuu hufanyika mara baada ya tume ya uchaguzi kufungua rasmi zoezi la shughuli za uchaguzi katika mwaka husika. Mkutano Mkuu wa CCM wa tarehe 18 & 19 Januari 2025 ulikuwa na ajenda moja kuu ya kumpitisha Makamu M/Kiti Taifa.

Sasa hili la kumteua mgombea wa nafasi ya urais kutokana na ajenda ya mengineyo (yaani AOB) siyo tu ilikuwa ni uhuni uliofanyika hadharani bali pia ni kituko cha mwaka. Hii ni aibu kubwa kwa Mwenyekiti wa kikao, na hata kwa wajumbe wote walioshiriki na kuridhia uamuzi ule. Kuchomekea jina la mpeperusha bendera ni kitendo cha kihuni, na pia ni fedheha kubwa wa kuhalalisha haramu ionekane kuwa halali.
 
Washazoea kuiba uchaguzi, na juzi uliona Jinsi Kikwete na Mama walivyoiba uchaguzi wa Mgombea wa Uraisi, Kikwete huwa na maslai gani na hii nchi kila mara anatuletea Raisi kutoka mfukoni mwake, au yeye ndo MMILIKI WA TANZANIA
 
Hangaika na Saccos yako ya CDM ya CCM waachie CCM wenyewe, mkutano mkuu wa CCM ndio ulioamua na ndio wenye mandate.
Mtukufu sapoka kuhusu utaratibu kanuni za kudumu za...
 
Kilichofanyika Dodoma hakieleweki kamwe, ...ccm wajitafakari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…