Pre GE2025 Wasira awatetemesha akina Tundu Lissu na Wenzake: "Kauli Mbiu ya "No Reform, No Election" Haina Maana Kwa Sasa"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Stevin Wasira, amesema kauli mbiu ya "No Reform, No Election" haina maana yoyote kwa sasa, akisisitiza kuwa muda wa kufanya mabadiliko ya kisheria umekwisha kutokana na uchaguzi mkuu kukaribia.
View attachment 3213528
Akizungumza leo, Januari 23, 2025, jijini Dodoma, Wasira alieleza kuwa badala ya kushikilia kauli hiyo, CHADEMA wanapaswa kushiriki uchaguzi na kuhakikisha wanakubaliana na maridhiano yaliyopo.

"Kauli ya 'No Reform, No Election' haina nafasi kwa sasa. Rais Samia Suluhu Hassan na CCM wameonyesha utayari wa mazungumzo, na bunge linakaribia kuvunjwa, hivyo hakuna muda wa kufanya mabadiliko ya kisheria yanayohitaji muda mrefu," alisema Wasira.

Aliongeza kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu, unaotarajiwa kuchagua Rais, Wabunge, na Madiwani, unapaswa kuwa nafasi ya vyama vyote kushindana kwa hoja badala ya kutafuta visingizio.

Wasira aliwataka viongozi wa CHADEMA kutumia nafasi za mazungumzo zilizopo badala ya kusimamia misimamo isiyotekelezeka kwa wakati huu. "Ni muhimu kushiriki uchaguzi na kuwa sehemu ya demokrasia badala ya kupoteza muda na kauli ambazo hazina tija kwa wananchi," alisisitiza.

..badala ya kufanya uchaguzi kwa kutumia sheria mbovu kwanini tusiuahirishe mpaka 2016 ili tufanye marekebisho ktk Tume ya Uchaguzi?

..hii nchi ni yetu sote. Raisi apewe ushauri mzuri kwa maslahi ya taifa letu.
 
Hao wanaokaribishwa kutoa ushauri akina LIssu. Mawazo yao yapo Ubeligiji
 
..sote tunajua Lissu anakwenda Ubelgiji kutibiwa.

..kwanini CCM mnachukia Lissu akipata matibabu?
CCM ndio imepewa dhamana ya Watanzania wote. Ndio maana Lissu anapewa misaada yote anayoihitaji na Serikali ya CCM. So hakuna anayemchukia LIsuu
 
..hoja iliyopo mezani ni marekebisho ya Katiba yatakayowezesha kuundwa kwa Tume Huru kabla ya uchaguzi mkuu.
Tayari Sheria ya uchaguzi imesharekebishwa. Unataka utengenezwe kwa manufaa ya Lissu pekee yake? 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Hao wanaokaribishwa kutoa ushauri akina LIssu. Mawazo yao yapo Ubeligiji

..CCM mmeshauriwa kuhusu Tume Huru toka mwaka 1991 wakati Jaji Mkuu Francis Nyalali alipowasilisha taarifa ya Tume ya vyama vingi.

..Tangu Mama Samia aingie madarakani amekuwa akitahadharishwa, akishauriwa, akililiwa, akibembelezwa, ili arekebishe Tume ya Uchaguzi.

..Sasa leo hii Makamu wa Mwenyekiti wa CCM akijitokeza na kusema hakuna muda wa kurekebisha Tume hakuna anayeweza kumtilia maanani. Wenye akili timamu wataona kwamba Mzee Wassira analeta dharau, na kiburi.
 
Wapi amesema hivyo? Mzee au unajitungia taarifa wewe mwenyewe? 🤣 🤣 🤣 🤣
Marekebisho ya sheria za uchaguzi Mbowe na Lissu waliingia mitini. Sheria za uchaguzi zilishapitishwa na zinafanya kazi.

Sasa nakuuliza Unataka marekebisho ya Sheria hizo yawe kwaajili ya CHADEMA pekee na siyo Tanzania?
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Stevin Wasira, amesema kauli mbiu ya "No Reform, No Election" haina maana yoyote kwa sasa, akisisitiza kuwa muda wa kufanya mabadiliko ya kisheria umekwisha kutokana na uchaguzi mkuu kukaribia.
View attachment 3213528
Akizungumza leo, Januari 23, 2025, jijini Dodoma, Wasira alieleza kuwa badala ya kushikilia kauli hiyo, CHADEMA wanapaswa kushiriki uchaguzi na kuhakikisha wanakubaliana na maridhiano yaliyopo.

"Kauli ya 'No Reform, No Election' haina nafasi kwa sasa. Rais Samia Suluhu Hassan na CCM wameonyesha utayari wa mazungumzo, na bunge linakaribia kuvunjwa, hivyo hakuna muda wa kufanya mabadiliko ya kisheria yanayohitaji muda mrefu," alisema Wasira.

Aliongeza kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu, unaotarajiwa kuchagua Rais, Wabunge, na Madiwani, unapaswa kuwa nafasi ya vyama vyote kushindana kwa hoja badala ya kutafuta visingizio.

Wasira aliwataka viongozi wa CHADEMA kutumia nafasi za mazungumzo zilizopo badala ya kusimamia misimamo isiyotekelezeka kwa wakati huu. "Ni muhimu kushiriki uchaguzi na kuwa sehemu ya demokrasia badala ya kupoteza muda na kauli ambazo hazina tija kwa wananchi," alisisitiza.
TAL njoo huku babu anakuita😂
 
NINA UMRI WA BABAAKO, HUENDA CLASSMATE
Tayari unaonekana hujapevuka kiakili. Nimekuuliza swali dogo tu umeanza kuhaha. 🤣 🤣 🤣 🤣
Narudia, Umri wako ni miaka Mingapi?
 
Back
Top Bottom