Wapi amesema hivyo? Mzee au unajitungia taarifa wewe mwenyewe? 🤣 🤣 🤣 🤣
Marekebisho ya sheria za uchaguzi Mbowe na Lissu waliingia mitini. Sheria za uchaguzi zilishapitishwa na zinafanya kazi.
Sasa nakuuliza Unataka marekebisho ya Sheria hizo yawe kwaajili ya CHADEMA pekee na siyo Tanzania?
..Kwanza Chadema, Mbowe, Lissu, hawakukimbia kushiriki mchakato wa kurekebisha sheria za uchaguzi.
..Kilichotokea ni serikali na Bunge kupuuza maoni ya wadau ambayo yangepelekea marekebisho ya maana ktk Tume ya uchaguzi, na mifumo inayosimamia uchaguzi.
..Marekebisho yamefanyika lakini hayajakidhi matarajio ya vyama vya siasa, viongozi wa dini, asasi za kiraia, na wananchi mbalimbali waliojitokeza kutoa maoni kwa Kamati ya Bunge.
..Hata hayo marekebisho yasiyokidhi viwango ambayo Bunge limepitisha serikali bado haitaki kuyatekeleza.
..Kwa mfano, Bunge limepitisha sheria chaguzi zote zisimamiwe na Tume, serikali imepuuza na Tamisemi wakasimamia uchaguzi wa serikali za mitaa.
..Mfano mwingine, Bunge limepitisha sheria kuanzisha Tume Huru, lakini serikali imegoma kuteua Tume hiyo, makamishna wa Tume ya zamani bado wako ofisini.
..Hii nchi ni yetu sote. Rais Samia ashauriwe vizuri katika suala hili na atende HAKI.