PreGE2025 Wasira: Deni la taifa, trilioni 97 hajakopa Rais Samia peke yake, tulikopa tangu enzi za Nyerere

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kukopa Siyo kosa ila ukikopa hizo Hela ulizokopa na kuzitapanya ndiyo huleta mjadala.

Kukopa Siyo dhambi, ila ukikopa bila ya kuwa na sababu za msingi zinazokulazimisha kukopa, huo ni uzwazwa.

Kukopa kwa niaba ya Nchi ni jambo linalohitaji hekima na utu, Lakini unapokopa kwa niaba ya Nchi na huo mkopo ukatumika kiubadhirifu, hiyo ni kufuru.
Utakopaje bila sababu za msingi?
 
Sasa atu changulie, deni la kila moja na kitu kilichofanywa na Muhusika.
Nyerere....
Mwinyi....
Mkapa....
Kikwete.....
Magufuli
Awamu ya Sita.......

Halafu Kazi iendelea dipi weldi ikiwemo, Adinani,- Tiscn

Halafu ipitieli ilikuwaje na Seth

Kwa sasa tuache hapo
Takwimu zipo mbona? In fact Nyerere ndio alikuwa na madeni mengi japo mengi yalisamehewa awamu ya MKAPA.
 
Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Stephen Wasira amesema nchi inakopa kwa ajili ya kufanya mambo tukayoishi nayo na faida zake zitakuwepo kwa miaka mingi kwa kizazi cha sasa na hata kijacho.

Amesema deni lililopo la Sh. trioni 97 sio kwamba lote limekopwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan bali limekuwepo tangu enzi za Rais wa kwanza, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Pia soma Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Wasira ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na wanachama pamoja na viongozi wa CCM Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu katika kikao cha ndani kikiwa sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo yenye lengo la kukagua uhai wa Chama, utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kusikiliza kero za wananchi.

“Tunakopa ili kufanya jambo ambalo tutaishi nalo na faida zake kwa miaka mingi kizazi hiki na hata kizazi kijacho na lile deni sio kwamba amekopa Rais Samia trilioni 97 sio kweli, lile deni linaongezeka na madeni mengine ya zamani ambayo tulishakopa tangu enzi za Nyerere, alichukua miaka 40 kuanza kulipa nayo yamo katika hesabu," amesema.

View attachment 3286751
Anaona fahari kuishi na madeni kizazi na kizazi
 
Lakini Kwa Sasa wamekuja wale machawa ambao kazi Yao ni kuonesha Kwa vitendo eg Baba Levo na Masanja wao wanazunhuka huko na kule kwenye miradi kuonesha,Bora hao kuliko wale wengine.
Nafuu ya hao,kiukweli watanzania waliowengi wanataka kuona matokeo kwa macho na sio maandishi ya mahesabu ya matrilion na asilimia ngapi zimeongezeka mwaka huu.
Kwaio kina Masanja wanaonyesha kile wengi wanataka kuona.
 
Takwimu zipo mbona? In fact Nyerere ndio alikuwa na madeni mengi japo mengi yalisamehewa awamu ya MKAPA.
Weka takwimu sio maneno au siasa
Kwamba hizo trillioni 97
Ngapi za Nyerere na hazijalipwa kama zipo au ndio kutaka kumtupia Marehemu mizigo ya watu walio hai sababu hakuna wa kumsemea
 
Kukopa Siyo kosa ila ukikopa hizo Hela ulizokopa na kuzitapanya ndiyo huleta mjadala.

Kukopa Siyo dhambi, ila ukikopa bila ya kuwa na sababu za msingi zinazokulazimisha kukopa, huo ni uzwazwa.

Kukopa kwa niaba ya Nchi ni jambo linalohitaji hekima na utu, Lakini unapokopa kwa niaba ya Nchi na huo mkopo ukatumika kiubadhirifu, hiyo ni kufuru.
Hawa wajinga sababu yao kubwa ya kukopa sio uhitaji bali ni “ Deni linavumilika”!! This is utter stupidity.
 
Weka takwimu sio maneno au siasa
Kwamba hizo trillioni 97
Ngapi za Nyerere na hazijalipwa kama zipo au ndio kutaka kumtupia Marehemu mizigo ya watu walio hai sababu hakuna wa kumsemea
Sio rahisi kihivyo na lengo ni nini?
 
Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Stephen Wasira amesema nchi inakopa kwa ajili ya kufanya mambo tukayoishi nayo na faida zake zitakuwepo kwa miaka mingi kwa kizazi cha sasa na hata kijacho.

Amesema deni lililopo la Sh. trioni 97 sio kwamba lote limekopwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan bali limekuwepo tangu enzi za Rais wa kwanza, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Pia soma Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Wasira ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na wanachama pamoja na viongozi wa CCM Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu katika kikao cha ndani kikiwa sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo yenye lengo la kukagua uhai wa Chama, utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kusikiliza kero za wananchi.

“Tunakopa ili kufanya jambo ambalo tutaishi nalo na faida zake kwa miaka mingi kizazi hiki na hata kizazi kijacho na lile deni sio kwamba amekopa Rais Samia trilioni 97 sio kweli, lile deni linaongezeka na madeni mengine ya zamani ambayo tulishakopa tangu enzi za Nyerere, alichukua miaka 40 kuanza kulipa nayo yamo katika hesabu," amesema.

View attachment 3286751
Huyo mnayemtetea amekopa kiasi kikubwa kuliko wote waliopita. Amekopa pesa zote kwa miaka mitatu na nusu. Hatuna shida na kukopa bali tunataka kujua zimekwenda wapi? Maana hatuoni kilicho kikubwa kilichofanyika.
 
Ndugai alisema jinsi wanavyokopa kwa speed wanayokopa ipo siku nchi hii itapigwa mnada. Wakamfukuza uspika. Tuna dictator ambaye hataki kuambiwa ukweli.
 
Back
Top Bottom