Wasira: Urais 2025, chanzo upotosha uwekezaji bandari

Wasira: Urais 2025, chanzo upotosha uwekezaji bandari

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Ni haki yao hao wanaoutaka uraisi kujipanga. Mbona inajulikana wazi kuwa mama anamalizia miaka iliyoachwa na hayati kikatiba. Na kama ningepewa nafasi ya kumshauri mama, basi ningemshauri kwamba mambo ya 2025 aachane nayo kabisa. Maana hao anaowashutumu Tyson wamefanikiwa sana kumharibia mama.
 
Ni haki yao hao wanaoutaka uraisi kujipanga. Mbona inajulikana wazi kuwa mama anamalizia miaka iliyoachwa na hayati kikatiba. Na kama ningepewa nafasi ya kumshauri mama, basi ningemshauri kwamba mambo ya 2025 aachane nayo kabisa. Maana hao anaowashutumu Tyson wamefanikiwa sana kumharibia mama.
Ni nani aliyekuambia wewe "mama anamalizia..."? Usije ukawa wewe ni wakala tu wa kueneza upotoshaji huo, ili watu wasistuke.
Kama kazi hiyo ndiyo unayoifanya hapa, itakuwa imekushinda kabisa.

Ruto wa Kenya amekwishatoa mfano kwa wengine, kwamba inawezekana kabisa ukapambana kivyako, nje ya mfumo uliopo na ukafanikiwa kunyang'anya mfupa wanaoutafuna hao walioushikilia.

Watu hao hapa kwetu bila shaka na wao wanataka kufuata njia hizo hizo alizotumia Ruto.
 
Sukuma gang wanapush sana hii ajenda ya DPW. Mzee Wasira kaona mbali sana.
Hizi Propaganda za divid and rule. Nyiwe Wenyewe mlimtuhumu Kagsh mskma kuwa alilamba Sukari na hamkutaja amelambaje tena Saizi mnahusisha na Sukuma Gang. Muache Tabia za Kuwachonganisha Wananchi.
Nb: Umepewa room ya kutoa Maoni eneo lenye Changamoto ila Wewe kutwa kutukana na Kugombanisha Makabiri/Dini.
Tuone aibu Tanzania inauhitaji Mkubwa wa Wawekezaji eneo la Uchumi na Biashara, so ni Muhimu kushauri kuliko kutukana Wawekezaji kwa sababu zako za kisiasa.
Nasikia: Kuna Mataifa nao walikuwa wanataka na Baada ya Kukosa wakanunua visemeo vya Kuchonganisha Wanachi na Mwekezaji.
 
Wasira is a spent force, Hata wapiga kura wake waliona Bora Esther kuliko huyo anayesinzia masaa kumi na nane.
Wasira atakua amefikisha miaka 85: MTU wa umri huo unadhani ataongoza watu kwenda wapi zaidi ya makaburini? Angetumia muda huu kufahamiana na vitukuu na kuandika wosia.
 
Ni nani aliyekuambia wewe "mama anamalizia..."? Usije ukawa wewe ni wakala tu wa kueneza upotoshaji huo, ili watu wasistuke.
Kama kazi hiyo ndiyo unayoifanya hapa, itakuwa imekushinda kabisa.

Ruto wa Kenya amekwishatoa mfano kwa wengine, kwamba inawezekana kabisa ukapambana kivyako, nje ya mfumo uliopo na ukafanikiwa kunyang'anya mfupa...
Mama anamalizia awamu ya 5 kikatiba. Hajawahi kuutafuta uraisi. Ila katiba imemleta kwenye uraisi. Mimi nilishangaa mlivyoanza kupindua awamu ya 5 na kutangaza awamu ya 6 lengo la mapinduzi ya awamu lilikuwa nini? Amalizie tu awamu ya 5. Na baada ya hapo mizani sawa ndani ya chama kutafuta mgombea wa uraisi na mama akipenda kuwa mmoja wao basi anaruhusiwa kuwa miongoni mwa wagombea.
 
Yupo sahihi kabisa na ninaafiki na mtazami wake.

Mzee wetu na apewe maua yake manake nimechoka na hawa wapiga debe , machawa wanaotaka kulazimisha na kupotosha kuwa hili suala ni la Kipinzani, ati ni la CHADEMA? Mimi ni CCM ninaemwagika damu ya kijani na nyeusi, na ninawajua wana CCM wenzangu, lukuki, wanao ona Mkataba huu una kasoro. Yaani haulubaliki.

Hakika mzee Wasira yupo sawa,walakini, wanaopinga ni kuwa, hawakubali mbinu hizi za kujipatia vitita vya kampeni za CCM 2025.
 
Mama anamalizia awamu ya 5 kikatiba. Hajawahi kuutafuta uraisi. Ila katiba imemleta kwenye uraisi. Mimi nilishangaa mlivyoanza kupindua awamu ya 5 na kutangaza awamu ya 6 lengo la mapinduzi ya awamu lilikuwa nini? Amalizie tu awamu ya 5. Na baada ya hapo mizani sawa ndani ya chama kutafuta mgombea wa uraisi na mama akipenda kuwa mmoja wao basi anaruhusiwa kuwa miongoni mwa wagombea.
Wewe nawe hueleweki, kwa vile upeo ni mdogo.
Ni nani aliyetangaza kuanza kwa "Awamu ya sita", unamjua?
Sasa hapa unabwabwaja kitu gani hasa?
 
Moto anaowapelekea ni balaa!.
20230723_170717.jpg
20230723_170712.jpg
 
Nimeipitia CV ya Mzee Wassira, kumbe na yeye ni Mchumi !!! Tena Mchumi wa basics na applied! Maelezo haya ni kwa mujibu wa Wikipedia
===

Amesomea Marekani Tena Mjini/Jijini Washington DC.

DPW inasemwa ya waarabu lakini umiliki wa DPW unaweza kuwa zaidi ya Waarabu. Wenzetu wa Magharibi waliwekeza/kwa jasho la Watanzania!!! Mpaka miaka ya 90 watanzania wengi walikuwa wanasomeshwa kwa pesa za walipa Kodi wa Tanzania.
 
Naamini kabisa waccm hasa wenye nafasi za juu katika serikali hii,hawaukubali mkataba huu,ila wana hofu wakijitokeza watapoteza nafasi walizonazo. Mama kama wanavyokuita kuwa makini sana .
 
Back
Top Bottom