Wasomi jifunzeni kwa dada Mwasu, dereva wa bajaji msomi mwenye shahada mbili

You think something.
 
Umejitahidi kutoa maoni yako kwa faida ya wengi
 

Kila mtu anaangalia life kwa angle yake mkuu

Kuna NGO zipo zinazowalipa interns wao laki mbili plus sehemu ya kulala, chakula na huduma za afya. Hiyo ya 390000 kwa mtu experienced nadhani inategemeana na ukubwa wa NGO yenyewe
 
Usitake kuhalalisha mambo ya hovyo bwn! Unataka kunambia huyo angejua kama ataishia kuwa dereva wa bajaji angejihangaisha kuzitafuta hizo degree 2? Kama hatuwezi kuajiri watu wetu kwa nafasi zinazoendana na elimu zao, kwa nini kuwaingiza kwenye gharama na upotevu wa muda kuwapa hiyo elimu kubwa?

Tukubali tu kuwa tumeshafeli!!!!
 
Ujinga huu nao niwakujivunia?? Master unaenda kuendesha bajaji?? Kweli? Elimu yetu ni ya hovyo sana, badala ya kwenda kutatua changamoto za kijamii na kuja na kitu kipya kama msomi, unakwenda kuendesha bajaji na na yule wa shule msingi atafanya kazi gani?
 
mwaka 2011 aliamua kujiendeleza katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) huku akiendelea kufanya kazi. Alihitimu mwaka 2013 shahada ya uzamili katika utawa (Masters of public adminstration).
Kam ameshindwa kutumia elimu yake kufanya mambo yanayoendana na elimu yake Basi sawa, tunasema elimu yetu haina msaada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na hili gazeti la mwananchi wanafeli sana, badala ya kutuletea emerging youth billionaires watu wawe inspired, tunarudishana kwenye udereva wa bajaji
Na wasiojua kiswahili wapitie hapa kuhusu hii !🙄
 

Attachments

  • 1609073285193.png
    359.9 KB · Views: 3
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…