Wasomi jifunzeni kwa dada Mwasu, dereva wa bajaji msomi mwenye shahada mbili

Wasomi jifunzeni kwa dada Mwasu, dereva wa bajaji msomi mwenye shahada mbili

Kuna jambo anatuficha , kafanya kazi za NGOs tangu 2009

Kama mshahara ulikua mdogo ada ya kusoma masters na pesa ya kujikimu alipata wapi ?

Kwa position alizotaja kufanyia kazi napata mashaka na huo mshahara aliotaja

Namalizia , kuna jambo anatuficha

Lakini kuhusu biashara nadhani ni suala la kuyumba kiuchumi tu limetokea maana inaonekana tayari alikua na biashara kubwa ya nguo
You think something.
 
Hivi kweli UWEZO WETU , wasomi kiwango hata cha diploma, hatuwez kubuni bali kuvamia idea iliyobuniwa na std seveni,? " hii inasikitisha Sana Sana, ina maana IRR(internal rate of return) kwa serikali KUWEKEZA kwenye elimu linakomea kumonitor kutoa tu mikopo, baada ya kumaliza tu biashara imeisha, kuna haja ya mfumo yetu iliangalie hili, kama Kweli msomi nguri kama Huyo anafaa ku-compete Sokoni na wale less than std seven?. Mr.einstern, amewahi sema,"UKIOONA MWANAFUNZI wako hajaelewa, jua wewe una mbinu kidogo na uelewa mdogo kumuelimisha MWANAFUNZI". Naona hili si tatizo la Wanafunzi bali mfumo, kwani same class mmoja anaajiliwa Kampuni A, anafanya vizur, mwingine analaumiwa kwasabab tu mazingira yake sio rafik. !! ".Stefan's Law of black body, alisema, temperature flow from high concentration to low temperatures under certirice per bus" aliimanisha, kuwa joto litatoka palipo na joto kubwa kwenda palipo na joto kidogo, hivyo chenye joto kubwa kitapoteza HARAKA joto lake, ,namuona msomi Huyu akipoteza uwezo wake wa KUFIKIRI kwani anaokutana nao kwenye maeneo yake ya kazi ni std seven (low temperature) kifikra, hivyo atajikuta anafanana nao, Na kuwaza level moja. Siku tukioona msomi mmoja kuwa kundi lisilo lake ni tatizo la sote basi TUTAWAZA SAWA.. iam not voting this kind of entrepreneur as appropriate to be promoted as a legacy to the rest of university graduates.View attachment 1660403View attachment 1660406
Umejitahidi kutoa maoni yako kwa faida ya wengi
 
Kuna jambo anatuficha , kafanya kazi za NGOs tangu 2009

Kama mshahara ulikua mdogo ada ya kusoma masters na pesa ya kujikimu alipata wapi ?

Kwa position alizotaja kufanyia kazi napata mashaka na huo mshahara aliotaja

Namalizia , kuna jambo anatuficha

Lakini kuhusu biashara nadhani ni suala la kuyumba kiuchumi tu limetokea maana inaonekana tayari alikua na biashara kubwa ya nguo

Kila mtu anaangalia life kwa angle yake mkuu

Kuna NGO zipo zinazowalipa interns wao laki mbili plus sehemu ya kulala, chakula na huduma za afya. Hiyo ya 390000 kwa mtu experienced nadhani inategemeana na ukubwa wa NGO yenyewe
 
View attachment 1660302

Tofauti na mawazo ya wengi kuwa ukisoma hadi chuo kikuu lazima uajiriwe, Mwasu Mavere ameonyesha upande mwingine wa shilingi, kwamba unaweza kujiajiri na kufanikiwa zaidi. Licha ya kuwa na shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), yeye ameamua kuwa dereva wa pikipiki ya miguu mitatu (bajaji) akisafirisha abiria katikati ya makao makuu ya nchi, Dodoma.

Dada Mwasu anasema wasomi wengi wanatembea na bahasha miaka hadi mitatu bila kupata kazi, kumbe wangeuza hata karanga zingewaingizia kipato badala ya kuzunguka na vyeti. Hata hivyo, anasema mfanyabiashara msomi ni tofauti na asiyesoma, kwa kuwa ile elimu aliyonayo msomi anaitumia kufanya vizuri kwenye biashara zake. “Kuna wasomi wengi wanaendesha bajaji na bodaboda na wapo wengine wengi mtaani wanatafuta kazi, hawajajua kuwa kuna kazi ya kuendesha bajaji na kujipatia fedha kama walioajiriwa, hivyo niwatake waache kuchagua kazi,” alisema Mwasu alipozungumza na Mwananchi.

Mwasu alianza shughuli za usafirishaji abiria Desemba 2018 katika eneo la eneo la Royal Village, Dodoma lakini baada ya muda alihamia katikati ya mji ili kupata abiria wa pande zote. Anasema wasomi wengi wanatembea na bahasha miaka hadi mitatu bila kupata kazi, kumbe wangeuza hata karanga zingewaingizia kipato badala ya kuzunguka na vyeti.

Hata hivyo, anasema mfanyabiashara msomi ni tofauti na asiyesoma, kwa kuwa ile elimu aliyonayo msomi anaitumia kufanya vizuri kwenye biashara zake. “Kuna wasomi wengi wanaendesha bajaji na bodaboda na wapo wengine wengi mtaani wanatafuta kazi, hawajajua kuwa kuna kazi ya kuendesha bajaji na kujipatia fedha kama walioajiriwa, hivyo niwatake waache kuchagua kazi,” alisema Mwasu alipozungumza na Mwananchi.

Mwasu alianza shughuli za usafirishaji abiria Desemba 2018 katika eneo la eneo la Royal Village, Dodoma lakini baada ya muda alihamia katikati ya mji ili kupata abiria wa pande zote. “Elimu yangu ni masters, lakini mshahara mdogo niliokuwa nalipwa ndio uliosababisha nikaamua kuacha kazi na kujishughulisha na biashara mbalimbali ikiwemo kuuza nguo na hatimaye nikaanza kuendesha bajaji,” anasema.

Mwasu, mama wa watoto wawili anasema mshahara aliokuwa analipwa ambao haukukidhi mahitaji yake wala kuendana na kiwango chake cha elimu, ulisababisha akaichukia ajira akaamua kujiajiri mwenyewe.Alisema mwaka 2009 alihitimu shahada ya sociology and political science nchini Kenya na baada ya hapo alirudi nchini na kufanya kazi katika NGOs mbalimbali.

Ilifopika mwaka 2011 aliamua kujiendeleza katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) huku akiendelea kufanya kazi. Alihitimu mwaka 2013 shahada ya uzamili katika utawa (Masters of public adminstration). Alisema wakati anafanya kazi kwenye shirika lisilo la kiserikali la Afnet alikuwa programme officer na field officer baada ya muda akahamia katika shirika jingine la Ngonedo ambapo alikuwa monitoring and evaluation officer (ufuatiliaji na tathmini).

Mwasu alisema katika kipindi alichofanya kazi hakuwa na mshahara uliokuwa unazidi Sh390,000 kwa mwezi, ambao amesema haukuwa unakidhi mahitaji yake. Alisema kipindi hicho anafanya kazi alikuwa na mtoto mdogo, hivyo kutokana na mahitaji yake kuwa mengi na mshahara mdogo alipomaliza shahada ya uzamili aliamua kuacha kazi na kuanzisha biashara mbalimbali ikiwemo kuuza nguo. “Hela hiyo haikuwa inakidhi mahitaji yangu, mwisho wa siku nikaona ili nisiingie kwenye vishawishi vya kuiba fedha ofisini ili kukidhi mahitaji, bora niache kazi, niliona ni bora kujiajiri mwenyewe kuliko kuajiriwa kwani nilichokuwa ninalipwa hakilingani na elimu yangu.

“Wakati huo nafanya kazi, nilikuwa nakusanya hela kidogo kidogo na kuna siku nilienda field, pesa niliyolipwa na zile akiba zangu nikaamua kuanzisha biashara kwa mtaji wa Sh400,000. Nilikwenda Kariakoo (Dar es Salaam na kuchukua mzigo wa nguo na kuja kuuza Dodoma.” Alisema Mwasu, biashara yake ilikuwa vizuri na alikuwa anaingiza fedha kuliko zile alizokuwa analipwa wakati ameajiriwa.

Biashara hiyo aliifanya kwa muda mrefu hadi akawa anasafiri kwenda China pamoja na wafanyabiashara wengine kuchukua mzingo wa nguo na kuuza nchini. “Katika biashara kuna kuinuka, lakini pia unaweza kushuka. Biashara yangu ilikuja kuwa mbovu nikawa napata hasara, si kila siku ni kupata faida, hasara kwa mfanyabiashara haikwepeki nawakati huo tayari nilikuwa nishapata mtoto wa pili. “Licha ya hasara hiyo, sikukata tamaa badala yake nikaamua kubadilisha kazi ya kufanya. Niliamua kuachana na biashara kabisa na kuwa dereva bajaj,” alisema.

Endelea kufahamu Kilichomfanya aendeshe bajaji na Manufaa yake pamoja na Changamoto aipatayo kupitia link >>> Mwasu, dereva wa bajaj mwenye shahada mbili

View attachment 1660415
Usitake kuhalalisha mambo ya hovyo bwn! Unataka kunambia huyo angejua kama ataishia kuwa dereva wa bajaji angejihangaisha kuzitafuta hizo degree 2? Kama hatuwezi kuajiri watu wetu kwa nafasi zinazoendana na elimu zao, kwa nini kuwaingiza kwenye gharama na upotevu wa muda kuwapa hiyo elimu kubwa?

Tukubali tu kuwa tumeshafeli!!!!
 
Ujinga huu nao niwakujivunia?? Master unaenda kuendesha bajaji?? Kweli? Elimu yetu ni ya hovyo sana, badala ya kwenda kutatua changamoto za kijamii na kuja na kitu kipya kama msomi, unakwenda kuendesha bajaji na na yule wa shule msingi atafanya kazi gani?
 
mwaka 2011 aliamua kujiendeleza katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) huku akiendelea kufanya kazi. Alihitimu mwaka 2013 shahada ya uzamili katika utawa (Masters of public adminstration).
Kam ameshindwa kutumia elimu yake kufanya mambo yanayoendana na elimu yake Basi sawa, tunasema elimu yetu haina msaada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na hili gazeti la mwananchi wanafeli sana, badala ya kutuletea emerging youth billionaires watu wawe inspired, tunarudishana kwenye udereva wa bajaji
Na wasiojua kiswahili wapitie hapa kuhusu hii !🙄
 

Attachments

  • 1609073285193.png
    1609073285193.png
    359.9 KB · Views: 3
Back
Top Bottom