Ni kweli Luteni, kuna thread moja hapa sikumbuki ilikuwa ni ya nini, Mwanakijiji alisema amefika stage anahisi kama tunamwonea rais. Niko na feeling hiyo hiyo mimi pia, frankly ninahisi kana kwamba tunamuonea mr president. Kuna vitu kwa kweli anaviongea halafu masikio yangu yanagoma kupokea kwamba no hajasema pamoja na kwamba ni kwenye luninga na ninamwona kwa macho yangu. Wale madaktari wa Cuba i doubt majibu yao kwa kweli.
Unajuwa nimefika mahali ninashindwa kuimagine hivi Kikwete asiyekuwa na serikali (mawaziri, makatibu wakuu na wengineo),washauri lukuki, usalama wa taifa, jeshi, chama tawala na mengineyo yasiyo na idadi anafananaje? Huyu mtu ana hizi organs zote nilizotaja na nisizotaja kumfanya ajuwe exactly what's going on na ni kipi cha kusema na kufanya ili nchi hii iende mbele lakini still kila siku ni kutusononesha tu tuliomchagua. Kwa wale tunaoamini Mungu kama mimi nadhani ipo haja ya kumwomba Mungu sana katika hili jambo, its more than serious.