Bufa
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 12,599
- 26,263
Una hoja nzuri ila sio sahihi kwa 100%
Sio kila scholarship inahitaji TOEFL/ IELTS hii ninakuhakikishia jaribu kufuatilia vizuri.
Njia nyingine ni sio lazima kufanya hiyo mitihani huwa kuna recommendation letters unaandikiwa na professors huwa wanahitaji walau wawili pia ikithibitisha English ilikua medium of instruction ulipokuwa chuoni.
Hata Nigeria yenye watu milioni 200+ kuna vyuo wanahitaji wapate score ya. walau 80 kwenye TOEFL
Nigeria kwa makadirio ina diaspora wapatao milioni 15 huku wengi wakiwa USA.
Nilijifunza kwa wanigeria walichonacho ni uthubutu ambao watanzania wengi hawana. Wanayo kampeni yao waniita "JAPA"
Maana ya neno hilo japa ni kutokomea/kukimbia kutoka katika hali usiyohitaji kwenye hili wapo serious sana na wanashikana mikono sana tofauti na diaspora wengine.
Pia fursa za kwenda nje zipo nyingi na tofauti kama ,visa sponsored jobs, exchange programmes pia unaweza kwenda kama mtalii ukifika unabadilisha status ya visa unapata na work permit.
Nchi zingine ambazo wanashikana mikono sana ni Wakenya na Wasomali , hawa ukienda jimbo la Minnesota [USA] ni rahisi kukutana na mkenya au msomali kama unavyoweza kuwa Eastleigh hapo Kenya.
Tumemwambia ila yeye anataka aletewe TOEL maghettoni acha aendelee kusubiri. Labda Bunge lijalo litapitisha TOEFL iwe kila wilaya against matakwa ya wenye mitihani yao.