Wasomi wa kitanzania wanashindwa kwenda nje ya nchi kutafuta fursa mbalimbali kwasababu ya hivi vitu viwili(TOEFL na IELTS)

Wasomi wa kitanzania wanashindwa kwenda nje ya nchi kutafuta fursa mbalimbali kwasababu ya hivi vitu viwili(TOEFL na IELTS)

Una hoja nzuri ila sio sahihi kwa 100%

Sio kila scholarship inahitaji TOEFL/ IELTS hii ninakuhakikishia jaribu kufuatilia vizuri.

Njia nyingine ni sio lazima kufanya hiyo mitihani huwa kuna recommendation letters unaandikiwa na professors huwa wanahitaji walau wawili pia ikithibitisha English ilikua medium of instruction ulipokuwa chuoni.

Hata Nigeria yenye watu milioni 200+ kuna vyuo wanahitaji wapate score ya. walau 80 kwenye TOEFL

Nigeria kwa makadirio ina diaspora wapatao milioni 15 huku wengi wakiwa USA.

Nilijifunza kwa wanigeria walichonacho ni uthubutu ambao watanzania wengi hawana. Wanayo kampeni yao waniita "JAPA"

Maana ya neno hilo japa ni kutokomea/kukimbia kutoka katika hali usiyohitaji kwenye hili wapo serious sana na wanashikana mikono sana tofauti na diaspora wengine.

Pia fursa za kwenda nje zipo nyingi na tofauti kama ,visa sponsored jobs, exchange programmes pia unaweza kwenda kama mtalii ukifika unabadilisha status ya visa unapata na work permit.

Nchi zingine ambazo wanashikana mikono sana ni Wakenya na Wasomali , hawa ukienda jimbo la Minnesota [USA] ni rahisi kukutana na mkenya au msomali kama unavyoweza kuwa Eastleigh hapo Kenya.

Tumemwambia ila yeye anataka aletewe TOEL maghettoni acha aendelee kusubiri. Labda Bunge lijalo litapitisha TOEFL iwe kila wilaya against matakwa ya wenye mitihani yao.
 
Ni ukweli kabisa usiopingika kwamba bara la Afrika kwa asili ni mahali pazuri sana pa kuishi hapa duniani, TATIZO KUBWA zaidi linalofanya bara hili la Afrika kuonekana kuwa ni mahali pabaya pasipofaa watu kuishi kwa amani ni kutokana na kuwepo kwa TAWALA MBAYA ZISIZOFAA kwenye hizi nchi zetu.
Tawala zilizopo ktk nchi za Afrika hazina mvuto kabisa wa kuweza kuwafanya watu kuwa na amani na furaha ya kuendelea kubaki ktk ardhi ya Afrika.
Tawala ni kuzisingia tu. All mental system ya mtu mweuse inaundergo evolution. Bado haiwezi kujisimamia.
 
Ukishindwa kufanya TOEFL kwa sababu hizi hata huko nje hujastahili kwenda.

You are simply not resourceful enough.

Kama umeshindwa kutoka Kigoma kuja Dar kufanya TOEFL, utawezaje kutoka Dar kwenda Los Angeles, USA?
Nilikwambia unikopeshe laki mbili hutaki?

Yaani wewe! Kazi kunisimanga tu!
 
ili kuepuka kufanya mitihani ya kozi hiZo kila baada ya miaka 2, nawashauri Watanzania kusoma Kozi ya Kiingereza ya Level ya juu (Advanced English Course, angalau kwa Level ya C1) ili upate cheti ambacho kinatambulika duniani kote, na cheti hiki utakitumia ktk maisha yako yote mpaka kifo.
Mkuu hii kozi hutolewa wapi ?
Je online naweza soma ?
Ni kiasi gani ada yake ?

Je hiko cheti kinaweza kuwa mbadala wa hio IETLS pale zinapotpka scholarship,namaanisha je nchi zinazotoa scholarship zinatambua hizo vyeti vya C1 kama ni mbadala wa hizo IETLS ?
 
Mkuu hii kozi hutolewa wapi ?
Je online naweza soma ?
Ni kiasi gani ada yake ?

Je hiko cheti kinaweza kuwa mbadala wa hio IETLS pale zinapotpka scholarship,namaanisha je nchi zinazotoa scholarship zinatambua hizo vyeti vya C1 kama ni mbadala wa hizo IETLS ?
Kozi hutolewa katika British Council iliyopo Chini ya Balozi za UK.
Cheti hicho pia ni mbadala IETLS, lakini pia ni mbadala wa TOEFL pamoja na mitihani mingine inayofanana na IETLS au TOEFL.
Kozi hizi ni za kusoma darasani, sina uhakika kama wameanza kutoa kozi hizi mitandaoni, nenda Ofisi za British Council au Ofisi za Ubalozi wa Uingereza.
 
Kinachokusumbua ni Africanism..natural jealous =poorest society.
Africanism gani! Mbona huko Afrika ya Kusini, Kati na Magharibi wamejaa nchi za ulaya kama kwao, masiki Tanzania hata ukiangalia tv ni nadra sana kuona habari hata za utalii toka Tanzania! Tunajificha kisa kutokujua lugha za nje, aibu zaidi ni pale Magufuli na ujumbe wake alipokwenda Zimbabwe na wakashindwa kuhutubia kutokana na ujumbe wote kutokujua kiingereza japo wameutunywi kwa suti kali!
 
Hapo vip!!
Kwa awali ya yote niandike kirefu cha TOEFL ni Test of English as a foreign language na IELTS International English language Testing system .

Ndugu zangu awali ya yote niseme tu nasikitika sana kuwepo na kuzaliwa katika nchi kama hii inaitwa Tanzania.

Lakini pia sisi sote ni mashuhuda ya uwepo mchache wa watanzania wanaofanya kazi nje ya nchi.

Hoja ya msingi nikwamba ili msomi wa kitanzanie apate scholarship ya kwenda nje ya nchi lazima afanye mitihani ya TOEFL na IELTS.

Tatizo kubwa ni mazingira ya upatikanaji wa hizi huduma,kwanza ni gharama sana kwa watanzania waliowengi,pili uwazi na upatikanaji wake ni hadimu,image kwa nyakati kama na miaka hii huduma nyeti kama hii inapatikana Dar es salaam tu.

Nahisi pia uwadimu wa huduma kama hizi ni kuwazuiya watanzania wasiende nje ya nchi kwa makusudi,kwasababu baadhi ya viongozi wa jinga wanaamini watu wengi wakiwa nje ya nchi watafunguka akili na kuleta challenge kwa serikali.

Naishauri serikali kwasababu imeshindwa kutoa ajira kwa vijanabna viongozi wa kitanzania na serikali kwa ujumla haina uwezo wa kuwapatia wananchi wake ajira basi hizi huduma za TOEFL na IELTS zitolewe bure kwa gharama ya serikali.Vijana wenzangu wasomi tukajiachie kwenye fursa mbali zilizopo katika nchi mbalimbali za ulaya na Amerika.

Tena huduma hii itolewe kwenye kila wilaya kwawasomi wanaotaka kwenda nje kutafuta ajira.

Black skin what is the problem?
Unajuta kuzaliwa TZ, na ukafikiri ili utoboe Nje lqzima ufanye hizo test! Bro maisha ya kufsnikiwa sio mono system, ni multi system, IPO mifumo mingi ya kutoka Nje,
Wapo watz wengi ulaya, wanapiga kazi Sana, na hawajawahi, hata kufika chuo kikuu!
 
Back
Top Bottom