Wasomi wa vyuo siku hizi hamna kitu, wanafuata mkumbo tu

Wasomi wa vyuo siku hizi hamna kitu, wanafuata mkumbo tu

Ferruccio Lamborghini

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2020
Posts
1,667
Reaction score
2,595
Yaani ovyo tu, wengi wanaenda kusoma vyuoni kwa ajili ya kufuata mkumbo tu ili jamii iwachukulie kama vile wamesoma sana.

Ila huko chuoni aisee, ukiwaona utachoka. Yaan kichwani hakuna kitu😬 kuna mmoja alisoma IT nilimpa kazi ya kunipigia Windows 10 kwenye PC yangu,akabaki ananikodolea macho tu kama mhamiaji haramu anayekaguliwa na afisa uhamiaji.

Nikasema hapa hakuna kitu,.

Hivi nyie vijana mnaenda chuo kufanya nini?

Kama huamini nachokisema hapa ukionana na mtu yeyote wa chuo jaribu kumdodosa kwa vijiswali vya hapa na pale kuhusu kozi anayosomea huko chuo.

Watu wanachezea tu ada za wazazi ma walezi😰
 
Yaani ovyo tu, wengi wanaenda kusoma vyuoni kwa ajili ya kufuata mkumbo tu ili jamaa iwachukulie kama vile wamesoma sana.
Ila huko chuoni aisee, ukiwaona utachoka. Yaan kichwani hakuna kitu[emoji51] kuna mmoja alisoma IT nilimpa kazi ya kunipigia Windows 10 kwenye PC yangu,akabaki ananikodolea macho tu kama mhamiaji haramu anayekaguliwa na afisa uhamiaji.
Nikasema hapa hakuna kitu,.
Hivi nyie vijana mnaenda chuo kufanya nini?
Kwa hiyo huyu moja wa IT ndo ana hakilisha wasomi wote au?
 
Tatizo hata walimu wetu wamekuwa na changamoto, theory nyingi, practical chache
 
Halafu wanasema Ajira hakuna! Nani awaachie afisi na hizo Degree za mchongo.
 
IMG_20220219_211637.jpg
 
Kupiga window chini ndiyo kipimo ulichoona kinafaa kuwapima wananavyuo?..
Mbona unatumia kipimo cha kienyeji sana kukejeli elimu?
 
Binafsi nimekuwemo kwenye panels kadhaa za usaili unauliza swali jepesi tu kama TELL US ABOUT YOURSELF kwa Kimombo...the so called graduate anakula tu ulimi mwishowe mnaishia kumlima
 
Binafsi nimekuwemo kwenye panels kadhaa za usaili unauliza swali jepesi tu kama TELL US ABOUT YOURSELF kwa Kimombo...the so called graduate anakula tu ulimi mwishowe mnaishia kumlima
Saili za siku hizi hili swali sijakutana nalo
 
Mimi sijasoma IT ila windows installation ni kitu nakijua yangu nipo form four.

Hivyo hiki siwezi kukifanya kigezo cha kuelimika.

Nilifanya field Halmashauri fulani hivi kuna binti ni IT na yeye alikua field, akashindwa kuconnect laptop na hotspot. Nikamsaidia.

Na haikufanya nione IT ni nyepesi
 
Wasomi wa sasa wapo vizuri sana, ni vile mmepitwa na wakati na mmejaa chuki.
 
Halafu wanasema Ajira hakuna! Nani awaachie afisi na hizo Degree za mchongo.
Sio degree za mchongo jamani, hali ndiyo illivyo hata msiwalaumu.
Unaweza kuta hata huyo mwalimu aliyemfundisha hajui kuinstall hiyo window 10.
Ni juhudi binafsi za mwanafunzi zitamfanya ajue vitu.
 
Aliyekwambia kusoma IT ni kupiga window peke yake ni nani?

Kingine we hiyo S/W ulikuwa umenunua au ndo habari zenu unaenda na computer eti nipigie window alafu hujui hiyo window anatoa wapi.

Lengo halikuwa kufanya michambo sema tu ulivyoweka hoja zako mpaka kufikia hitimisho lako ndio mambo yamenichosha zaidi.

Swali jepesi kwako,wewe mwenzetu umesoma mpaka darasa la ngapi kwanza?
 
Yaani ovyo tu, wengi wanaenda kusoma vyuoni kwa ajili ya kufuata mkumbo tu ili jamii iwachukulie kama vile wamesoma sana.
Ila huko chuoni aisee, ukiwaona utachoka. Yaan kichwani hakuna kitu😬 kuna mmoja alisoma IT nilimpa kazi ya kunipigia Windows 10 kwenye PC yangu,akabaki ananikodolea macho tu kama mhamiaji haramu anayekaguliwa na afisa uhamiaji.
Nikasema hapa hakuna kitu,.
Hivi nyie vijana mnaenda chuo kufanya nini?
Kama huamini nachokisema hapa ukionana na mtu yeyote wa chuo jaribu kumdodosa kwa vijiswali vya hapa na pale kuhusu kozi anayosomea huko chuo.
Watu wanachezea tu ada za wazazi ma walezi😰
Wewe haukusoma kwenye hivyo vyuo?
Kupiga Windows kwenye PC ndio kufanyaje?
 
Back
Top Bottom