Wasomi wa vyuo siku hizi hamna kitu, wanafuata mkumbo tu

Wasomi wa vyuo siku hizi hamna kitu, wanafuata mkumbo tu

Wanakesha Instagram Facebook na kuweka status nyingi WhatsApp kuna wawili walikuja field hapa ni aibu inabidi wizarani ijitafakari uelewa wa wahitimu hawa wa siku za karibuni ni shida vitu vidogo tu hawavijui.
 
sio wote mzee ila kuna mmoja nilikuwa najadiliana naye jinsi serikali ya magufuli ilivyoshindwa kiuchumi kwa kigezo kidogo tu cha kushindwa kutekeleza budjet majibu aliyoyatoa hata maiti siwezi kuisimulia


na kuna mwingine tulikuwa tukijadiliana naye madhara ya serikali kuchapisha pesa kiholela alichonijibu siwezi hata kuusimulia mti wa mpapai
 
Yaani ovyo tu, wengi wanaenda kusoma vyuoni kwa ajili ya kufuata mkumbo tu ili jamii iwachukulie kama vile wamesoma sana.

Ila huko chuoni aisee, ukiwaona utachoka. Yaan kichwani hakuna kitu😬 kuna mmoja alisoma IT nilimpa kazi ya kunipigia Windows 10 kwenye PC yangu,akabaki ananikodolea macho tu kama mhamiaji haramu anayekaguliwa na afisa uhamiaji.

Nikasema hapa hakuna kitu,.

Hivi nyie vijana mnaenda chuo kufanya nini?

Kama huamini nachokisema hapa ukionana na mtu yeyote wa chuo jaribu kumdodosa kwa vijiswali vya hapa na pale kuhusu kozi anayosomea huko chuo.

Watu wanachezea tu ada za wazazi ma walezi😰
Ndio hao unakuja kuwakuta Tanroads Wana design barabara kama za hapo Tazara na Ubungo 😬😬
 
Back
Top Bottom