Mimi ni mfugaji wa kuku,mbuzi na kwa uchache sana Ng'ombe hivyo huwa natambea maeneo na maeneo nakutana na kila aina ya mbegu za mifugo tajwa hapo juu.
Mara kadhaa nimekuwa nikishuhudia hii tabia ya kusafiri na kuku mara moja nimewahi safiri na msukuma na mbwa wa4 wadogo miaka na miaka bado hatubadiriki kabisa.Tunachosha angesema mgogo au mzaramo tungesema anatutania.
Sikatai kabisa kuwa kusafirisha mifugo tajwa hapo juu kuwa ni kosa lakini nakataa namna mifugo hiyo hasa kuku inavyosafirishwa kwenye gari la abiria.
Mtu anapanda gari mfano geita kwenda kahama ana vifaranga vya kuku 2 au kimoja ni kwamba huko kahama kabisa huwezi pata kifaranga cha sh 6000 hadi 10000 kama kweli wewe ni mdau wa ufugaji?
Mbaya zaidi unapanda na msukuma siti moja kutoka kahama hadi mpanda ana kuku wake ni safari ya siku nzima hii ni haki kweli?
Mambo mengine mnatufanya tuonekane wasukuma wote ni watu wasiojielewa mbaya zaidi ukiambiwa kwa lugha ya staha unajibu kwa sauti kuubwa halafu wasukuma wenzetu wasiojielewa kama wewe wanadikia utafikri umeomba lifti.
Wito kwa wenye magari angalieni namna nzuri za kusafirisha kuku sio tuwe tuna kaa na mtu aliyepakata kuku safari nzima akinya halufu yetu sote asee haifai
Hii ni kero
View attachment 3565962