Wasukuma mulimhola: Mmetisha kujaza Tanzania kila mahali!

Wanaongoza kwa kumiliki mifugo mingi nchini, pia ndio wazalishaji namba moja wa mpunga.. asilimia kubwa ya mashine za kukoboa mpunga zinamilikiwa na wao.. ukifika machimboni wao pia ndio mabingwa wa kuzamia mashimo marefu (rongobesi)
Ufugaji wa kijinga tuu,wanatakiwa kuougwa marufuku
 
Huko katavi wanyama wameamua kuwapisha wakae wao....😊😊
 
ni kweli, uchagani na umasaini hutaona wasukuma wamejazana huko na ndio maana jamii za wafugaji ni kama zimegawana nchi hii kanda ya ziwa, magharibi, kati na kusini wasukuma wana move sana huko na kanda ya kaskazini na mashariki wamasai wanafanya movement, hawakutani malishoni pamoja na kuwa kuna jamii zingine za wafugaji kama wao wanachuliana poa na kuwaona ni sehemu yao wanaendana pamoja hata katika mila zao
 
Yanatualibia = Yanatuharibia
Yamelogwa = yamerogwa

Ni lini Wasukuma walilazimisha Kisukuma?
Unamkosoa Nani kwa elimu gani uliyonayo zaidi ya kukalilishwa ubao Kama wewe ni mwerevu tuambie umegundua teknolojia gani mpaka huna chakunilekebisha we ni lofa tu
 
Sasa wewe umejifunga hapo kijiji kwenu tuu, tembea uone hawa ngosha walivyosambaa TZ na wao wanaoñgea kisukuma tuu kwa sauti kubwa kila mahali.
Ngosha wanajiamini sana hata katikati ya Dar tunapiga Kisukuma tu! Nilikutana na mdada mmoja anafanya kazi kwenye NGO moja Dar eti anaogopa kuongea Kisukuma ataonekana mshamba nikamwangaliaaaaa! Nikajisemea nimekutana na hamnazo!
 
Kweli wasukuma kabila kubwa, kila sehemu ya Tanzania wapo wengi na wanachapa kazi kwelikweli. Nimewakubali sana.
Karibuni kwenye huu uzi tuwapongeze.
Sasa wewe wenzio tunashangaa wapemba wapo milio moja tu, ila nchi zote za westerners wamejaa kuanzia UK ndio kama kwao na EU yoote nenda America Canada wamejaa na kama umetokea bara hawa ndio wapokezi wako.. wewe unasifia kujazana bongo?? Kuna baadhi ya maeneo ni ukame huwezi wakuta watu waliotoka mfano Mbea nk ila wasukuma ni Wapagazi tunashukuru Mafia ndio wakulima wetu,
 
Siri ya wasukuma ni kuoa zaidi ya mke mmoja wao hawana mke mmoja mpaka kifo kiwatenganishe

Wanamimina tu mbegu hakuna uzazi wa mpango wala family planing

Na wanalea na kukuza

Hii ishu ya mke mmoja ni uvivu wa kufanya kazi

Tofauti ya wasukuma na wapemba ni lafudhi tu ila vilivyobaki sawa
 
Hivi ndivyo wanaume tunavyotakiwa kuwa, ni kutimiza malengo ya kuletwa duniani.
 
Issue sio kuzaliana kama kumbikumbi,tunataka watuzalie cream na sio mambumbumbu.
 
wameingia Zanzibar na kisiwa cha mafia kuwasaidia wazee wa vijiweni kazi. Kwa hapa mafia, ujio wao umeleta faida sana kwenye kuzalisha vyakula. Wabarikiwe waongezeke zaidi
 
Issue sio kuzaliana kama kumbikumbi,tunataka watuzalie cream na sio mambumbumbu.
Kwa nini wewe usijifungie chumbani na mkeo mzalishe hiyo cream unayohitaji badala yake umezalisha machangu wanaosumbua watu "nitumie na yakutolea" na masharobaro wanaoshinda betting point na kukaba watu mtaani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…