Wasukuma ndivyo mlivyo au huyu ananiigizia

Wasukuma ndivyo mlivyo au huyu ananiigizia

Nitafute juuu ya huyo msukuma wako kiufupi mwambie akutolee posa akuoe
 
No reform no election

Habari zenu wana jf… hongereni kwa ibada kwa mlioenda na wengineo ambao mpo sehemu za starehe nawasalimia

Nataka nijue wasukuma ni watu wa haina hii au huyu wangu nimemuokota tu

Nipo na huyu mkaka almost 9 months lakini ila Naona kama hatuna chemistry au mimi ndio nina mawenge

1: Sio muongeaji yaani ukimwambia kitu anakujibu Sawa nimekuelewa😕 yaani unajitumisha sms ndefu halafu ni ile labda inahitaji majibizano yeye anajibu Sawa nimekuelewa
Ukimuuliza maana ake nini anacopy lile swali ulomuuliza analirudia kwako
Na ukilalamika utasikia anakwambia “umeanza” yaani hapo kamaliza aendelei 🤣

2: Hanaga story mpk wewe uanzishe kwaiyo mnaweza kujikuta ni hello, hello. Mzima .. mzima sijui wewe basi usiku mwema..

3: Kuongea na simu hapendi yaani ukiongea nae ni sekunde tena mara chache sana.. namuuliza una shida gani anasema I hate calls 😳😳 hapa ananishangaza


4: Analazimisha SANA NIkaishi nae ( ni long distance relationship) while hajanioa wala kunitolea mahali.. namueleza mimi nafanya kazi nikiacha inakuaje majibu yake wewe njoo tutafuta ingine

Kinachonifanya nibaki nae ni kwa kuwa yaani ni mpole, hawezi kuniongelesha vibay labda kunikejeri.. ana ule upendo mnapokuwa pamoja ana kujali.. kiufupi ana ile kukuthamini na kujishusha kidogo tu utasikia am sorry 😢

Ukweli wa Mungu huyu ndio mwanaume naempenda kutoka Rohoni ila mambo yake yanafanyaga nikaage mbali nae kila siku anatoa ahadi atabadilika lakini Hakuna mabadiliko

Mpk najiuliza kwani wasukuma wapo hivyo au huyu wangu ana matatizo yake

Ila nampenda Msukuma wangu sana tu
Sasa unalalamika nini, si unataka mpenzi na nani aliyekuambia Wasukuma ni wanaume sahihi kwenye mapenzi? Wale jamaa ni malimbukeni wa mapenzi at least kwa wanaume, pia ni ving'ang'anizi mno ukimzingua anakuu na panga.
 
Back
Top Bottom