Waswahili wengi hawaaminiki kwenye ajira

Waswahili wengi hawaaminiki kwenye ajira

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Nitatolea mfano halisi ambao nimekutana nao mimi:-

Kuna kijana mmoja alijitangaza mtandaoni anatafuta kazi, amehitimu mwaka juzi kwenye mambo ya IT.

Katika kumuhoji kweli, ikaonekana ana shida ya kazi kweli kwa sababu ata kula yake ilikuwa ni ya shida.

Nikaumiza kichwa, nikaona huyu atanifaa kwenye eneo fulani katika shughuli zangu, nimuweke pale huku akijishikiza lakini pia anapata kipato kwa kiasi fulani.

Ikabidi nimtumie nauli kule alikokuwa mpaka ofisi ilipo, nikampangishia vyumba viwili, pamoja na kuhakikiha ofisi inamuhudumia chakula kuanzia asubuhi mpaka cha usiku. Muhimu afanye kazi kwa utulivu.

Kweli alikuwa anafanya kazi kwa bidii, mpaka nikaona huyu ndio kijana niliyekuwa nikimtafuta. Kichwani nikawa nampangia malengo ya muda mrefu, ikiwepo namna ya kumboreshea maisha yake kwa sababu nilijua kwa spidi yake ile huko mbeleni nitaanza kupata faida.

Baada tu ya kumpatia mshahara wa mwezi mmoja, siku ya nne akanitumia ujumbe usiku wa saa nane, ya kuwa anaelekea mkoani baba yake ni mgonjwa yuko hoi anaenda kumuuguza kwa hiyo yuko safarini.

Nikaitafakari ule ujumbe,nikajiuliza kwa nini anitumie muda huu wa usiku, na mimi nilikuwa niko mbali, pia hakutoa taarifa kwa msimamizi wake.

Asubuhi nampigia simu zangu, hapokei; kesho yake nampigia simu hapokei tena, ndipo akanitumia ujumbe yuko hospitalini anamuuguza baba yake, ila nikimpigia simu hapokei.

Ndipo nikamwambia dada mmoja awasiliane naye kwa namba ambayo haitambui, akapokea vizuri na akaongea; ndipo nikajua huyu ameacha kazi kiuswahili bila kufuata utaratibu.

Mbaya zaidi, makazi yake nilikuwa nimeshalipia miezi mitatu achilia mbali gharama zingine.

Kwa ujumla alifanya ofisi yangu iyumbe kwa muda; ila nikawa nimejifunza watafuta ajira asa hawa wakiswahili sio watu wakuwaamini sana,ndio maana wengi hawaajiriki.​
 
Ulianza haraka kumpangishia labda hata mshahara haukuwa kivile kwa ujuzi wake

Pole, ila nawe inabidi kweli jitafakari kama employer na kujirekebisha. Usionyeshe unatumia mtu na akunyenyekee kisa unamtoa kwenye maisha dunia kwa mshahara kama mtumwa. Nimeongeza tu hili

Lingine inaonekana hata references za wowote haukuchukua au hata namba za next of kin wake na kuhakiki

Ahsante ni funzo kwa wengi, ila hawa wa mmoja wawili wafanyakazi muhimu kujua wanapotoka makwao...

Naongezea.. Hii ikija kwenye wizi mtu unabeba familia yake hadi ajitokeze muhusika
 
Back
Top Bottom