Waswahili wengi hawaaminiki kwenye ajira

Waswahili wengi hawaaminiki kwenye ajira

Ulianza haraka kumpangishia labda hata mshahara haukuwa kivile kwa ujuzi wake

Pole, ila nawe inabidi kweli jitafakari kama employer na kujirekebisha. Usionyeshe unatumia mtu na akunyenyekee kisa unamtoa kwenye maisha dunia kwa mshahara kama mtumwa. Nimeongeza tu hili

Lingine inaonekana hata references za wowote haukuchukua au hata namba za next of kin wake na kuhakiki

Ahsante ni funzo kwa wengi, ila hawa wa mmoja wawili wafanyakazi muhimu kujua wanapotoka makwao...

Naongezea.. Hii ikija kwenye wizi mtu unabeba familia yake hadi ajitokeze muhusika
Nilichukulia positive tu, kwenye kampuni wapo wanaoingia na kutoka pia
 
Kwa kweli vijana ni changamoto Sana kwenye uaminifu....... unaweza kuwa kwenye nafasi nzuri ya kumsaidia mtu lakini ukifikiria uzito wa kumbebea dhamana unaamua bora kuacha maana unaweza kujiletea matatizo.....

Mimi nilishawahi kumuita fundi kibaruani kwangu ili naye apate ridhiki....jioni baada ya kumaliza kazi anataka kutoka walinzi wanapekua begi wanakuta ameiba viatu.....

Kwa kweli niliona aibu sana......
 
Kwa mtu professional na mwenye akili timamu, anajua maana ya smooth transition kwenye ajira.

Pia anafahamu kua kuacha kazi ni haki ya mtu ila lazima lifanyike kwa namna ambayo anayeacha na anayeachwa wote wawe salama kwa maana ya wako aware kwa kupeana taarifa iwe informal au formal lakini IFAHAMIKE.

Unayedhani kua ukilipwa pesa ndogo ndo kigezo ukurupuke kama.ngiri kichakani jua wazi mawazo yako si ya kitaalamu unajiwazia tu.
 
Na tumfanye mtu kwa mfano wetu........

Hapa God ndo alikosea maana binadam ni nusu God huwez kumfuga kama mbuzi mpaka umuwekee sheria kali sana.......na bado atazivunjaaaaa
Hakuna namna, ukimuonea huruma yeye anakuona fursa
 
Back
Top Bottom