Waswahili wengi hawaaminiki kwenye ajira

Waswahili wengi hawaaminiki kwenye ajira

Nitatolea mfano halisi ambao nimekutana nao mimi:-

Kuna kijana mmoja alijitangaza mtandaoni anatafuta kazi, amehitimu mwaka juzi kwenye mambo ya IT.

Katika kumuhoji kweli, ikaonekana ana shida ya kazi kweli kwa sababu ata kula yake ilikuwa ni ya shida.

Nikaumiza kichwa, nikaona huyu atanifaa kwenye eneo fulani katika shughuli zangu, nimuweke pale huku akijishikiza lakini pia anapata kipato kwa kiasi fulani.

Ikabidi nimtumie nauli kule alikokuwa mpaka ofisi ilipo, nikampangishia vyumba viwili, pamoja na kuhakikiha ofisi inamuhudumia chakula kuanzia asubuhi mpaka cha usiku. Muhimu afanye kazi kwa utulivu.

Kweli alikuwa anafanya kazi kwa bidii, mpaka nikaona huyu ndio kijana niliyekuwa nikimtafuta. Kichwani nikawa nampangia malengo ya muda mrefu, ikiwepo namna ya kumboreshea maisha yake kwa sababu nilijua kwa spidi yake ile huko mbeleni nitaanza kupata faida.

Baada tu ya kumpatia mshahara wa mwezi mmoja, siku ya nne akanitumia ujumbe usiku wa saa nane, ya kuwa anaelekea mkoani baba yake ni mgonjwa yuko hoi anaenda kumuuguza kwa hiyo yuko safarini.

Nikaitafakari ule ujumbe,nikajiuliza kwa nini anitumie muda huu wa usiku, na mimi nilikuwa niko mbali, pia hakutoa taarifa kwa msimamizi wake.

Asubuhi nampigia simu zangu, hapokei; kesho yake nampigia simu hapokei tena, ndipo akanitumia ujumbe yuko hospitalini anamuuguza baba yake, ila nikimpigia simu hapokei.

Ndipo nikamwambia dada mmoja awasiliane naye kwa namba ambayo haitambui, akapokea vizuri na akaongea; ndipo nikajua huyu ameacha kazi kiuswahili bila kufuata utaratibu.

Mbaya zaidi, makazi yake nilikuwa nimeshalipia miezi mitatu achilia mbali gharama zingine.

Kwa ujumla alifanya ofisi yangu iyumbe kwa muda; ila nikawa nimejifunza watafuta ajira asa hawa wakiswahili sio watu wakuwaamini sana,ndio maana wengi hawaajiriki.​
Mkuu hata ccm waliahatuona jinsi tulivyo ndio maana wanajipigia tu wao na familia zao.

Sisi waswahili hatuna maana.
 
Sasa ulitaka huyo kijana akae hapo forever?

Ni muda wake wakuondoka.

Unapomsaidia mtu usitegemee kwamba atakaa na wewe milele.

Na yeye ana plan zake kichwani.
Shida zake ziliisha ndani ya Mwezi Mmoja?

Huyo alikuwa na demu sasa ile kupata laki tatu kwa pamoja akachachawa😂😂
 
Sasa bora ata angekaa miezi mitatu angalau atengeneze cv, sasa mwezi mmoja mbio
Unaajiri Mdada abakuja analia shida, akishapata ajira baada ya mieI miwili tu anakwambia ana mimba. Hapo anataka apatw Excuses za kazi, muda wa kazi na routines zingine.

Hadi unajiuliza hivi hawa waswahili wana akili kweli?
 
Tatizo kubwa ni uvumilivu, lakini ndio hivyo kila mtu na kichwa chake
Wanashinda kwenyw Bongo Fleva wanadanganyana Bora ni Enjoy, maisha mafupi ni simple......Thay think it is real life.

Mafanikio yoyote yanahitaji uvumilivu.

dogo ulimpa mazingira mazuri sana ya kazi.
 
nakuwa na amani nikiingia ofisini au hata dukani nikikutana mtu ambaye sio mswahili mwenzangu,....
 
Nitatolea mfano halisi ambao nimekutana nao mimi:-

Kuna kijana mmoja alijitangaza mtandaoni anatafuta kazi, amehitimu mwaka juzi kwenye mambo ya IT.

Katika kumuhoji kweli, ikaonekana ana shida ya kazi kweli kwa sababu ata kula yake ilikuwa ni ya shida.

Nikaumiza kichwa, nikaona huyu atanifaa kwenye eneo fulani katika shughuli zangu, nimuweke pale huku akijishikiza lakini pia anapata kipato kwa kiasi fulani.

Ikabidi nimtumie nauli kule alikokuwa mpaka ofisi ilipo, nikampangishia vyumba viwili, pamoja na kuhakikiha ofisi inamuhudumia chakula kuanzia asubuhi mpaka cha usiku. Muhimu afanye kazi kwa utulivu.

Kweli alikuwa anafanya kazi kwa bidii, mpaka nikaona huyu ndio kijana niliyekuwa nikimtafuta. Kichwani nikawa nampangia malengo ya muda mrefu, ikiwepo namna ya kumboreshea maisha yake kwa sababu nilijua kwa spidi yake ile huko mbeleni nitaanza kupata faida.

Baada tu ya kumpatia mshahara wa mwezi mmoja, siku ya nne akanitumia ujumbe usiku wa saa nane, ya kuwa anaelekea mkoani baba yake ni mgonjwa yuko hoi anaenda kumuuguza kwa hiyo yuko safarini.

Nikaitafakari ule ujumbe,nikajiuliza kwa nini anitumie muda huu wa usiku, na mimi nilikuwa niko mbali, pia hakutoa taarifa kwa msimamizi wake.

Asubuhi nampigia simu zangu, hapokei; kesho yake nampigia simu hapokei tena, ndipo akanitumia ujumbe yuko hospitalini anamuuguza baba yake, ila nikimpigia simu hapokei.

Ndipo nikamwambia dada mmoja awasiliane naye kwa namba ambayo haitambui, akapokea vizuri na akaongea; ndipo nikajua huyu ameacha kazi kiuswahili bila kufuata utaratibu.

Mbaya zaidi, makazi yake nilikuwa nimeshalipia miezi mitatu achilia mbali gharama zingine.

Kwa ujumla alifanya ofisi yangu iyumbe kwa muda; ila nikawa nimejifunza watafuta ajira asa hawa wakiswahili sio watu wakuwaamini sana,ndio maana wengi hawaajiriki.​
Wenzako tumezoea! Kuamka asubuhi unakuta Wafanyakazi wako kadhaa wamekublock ni kawaida. Ndiyo maana tunahakikisha tunaajiri na wa akiba ili (wa)akiindoka katika Idara nyeti, taasisi isiyumbe! Ni gharama maana unalipia NSSF, PAYE, WCF etc
 
Ulianza haraka kumpangishia labda hata mshahara haukuwa kivile kwa ujuzi wake

Pole, ila nawe inabidi kweli jitafakari kama employer na kujirekebisha. Usionyeshe unatumia mtu na akunyenyekee kisa unamtoa kwenye maisha dunia kwa mshahara kama mtumwa. Nimeongeza tu hili

Lingine inaonekana hata references za wowote haukuchukua au hata namba za next of kin wake na kuhakiki

Ahsante ni funzo kwa wengi, ila hawa wa mmoja wawili wafanyakazi muhimu kujua wanapotoka makwao...

Naongezea.. Hii ikija kwenye wizi mtu unabeba familia yake hadi ajitokeze muhusika
Ukweli ni kuwa mtu anaondoka kutokana na maslahi. Ila kinachoumiza sisi waajiri ni jinsi ya kuacha kazi. Kawaida unampatia taarifa mwajiri iwe masaa 48 au mwezi etc. Mikataba inambana tu mwajiri si mwajiriwa.
 
Bora wewe mkuu hakukuibia. Waswahili siyo waaminifu, ukiwaajiri wanakurudisha nyuma.

Wenye mitaji ya kudunduliza tuna wasiwasi sana na vijana wa kazi wasiturudishe nyuma tuanze upya tena kutafuta mtaji.

Wenzetu mlioajiri, mnawadhibiti vipi vijana wa kazi wasiwaibie?. Kudhibiti kijana wa kazi ni ngumu sana
 
Kuna lingine nimelipambania kwa mwajiri wangu flani wa zamani mhindi mpaka likapata kazi,mshahara 1.1m limefanya kazi miezi mitatu likaanza uvivu mara halitumi reports za watu,siku limeaga kuwa mzee wake huko Bush anaumwa linaenda kuuguza huku nyuma likawa lishawaambia wenzake eti limechoka na kazi hivyo halitorudi..sasa hivi linanijia na story eti kama nina ramani yoyote nilistue na wakati nililipa ramani likaharibu na kunitia aibu juu.
Since then nikajifunza sitokaa nimpigie mtanzania mwenzangu pande sehemu yoyote ile.
 
Back
Top Bottom