Waswahili wengi hawaaminiki kwenye ajira

Nilikuwa najiuliza, kwa nini makampuni makubwa yanaajiri wahindi; ila kwa sasa nimekuja kupata jibu.
 
Nadhani pia labda tatizo la ujana
 
Hawo watu wanaharibia vijana wengine kupata kazi/ajira,maana kila atakaekuja unawaza yale yale ya huyo alieondoka gafla.ni bora kuwa na mikataba ya kazi,hata kama ni mlinzi wa geti,mkataba utambana yeye pamoja na wewe mwajiri.
 
Inawezekana ikawa hivyo, kwa sababu alikuwa akipokea 350, amelipiwa kwa kukaa, na anakula bure kuanzia asubuhi mpaka jioni
Hata sio mshahala mdogo
Kuna mafala wanapenda sana kuwachukua wafanyakazi wa wenzao kwa kuwalaghai

Mfano mtu akiona una STUDIO kali ya photoshot na video recording ama tigopesa imechangamka anadhani na yeye akifungua atakula maokoto kama wewe

Sasa hapo hao mafala ndo umshawishi atoke ataenda kumuazishia nyingine atamlipa vizuri
Tena utakuata inaongezeka laki tu
Sasa kinachowatokeaga badae huwa nacheka
Wakirudi
wanadhani kuwa biashara ukianza tu un apata faida kumbe mtu biashara unaweza endesha mwaka mnzima bira faida tena wakati mwingine unaingiza na pesa yako ya mshahara au ziada 7bu unajua kuwa unawekeza baada mwaka au miaka 2 ndo upate faida
Sasa wengi udhani wakianzisha faida itakuja kama walivyoplan kwenye karatasi matokeo yakiwa tofauti ugomvi unaanza BIASHARA inakufa then wanabaki kuwa hawana ajira

Mkuu jambo nzuri ajakuibia ilo la kumshukuru MUNGU
Next time ukiajiri mtu mchukulie kuwa ni mfanyakazi term and condition ziende hvyohvyo ukishamchukilia kam ndugu na kisha ukaanza kumpa matumaini kuwa piga kazi kwa bidii baadae mambo yatakuwa manzuri kwa hawa wafanyakazi wa kibongi haswa wakiume tena akiona yeye ndo kiungo muhimu lazimu akutende tu
 
Kwa mazingira hayo, hakuna haja ya kuoneana huruma kwenye ajira
Mambo ya kuoneana huruma kwenye ajira yapo Afrika tu, Kwa vile ajira ni ngumu kupatikana.

Na hii kitu ndio inawafanya mabosi wengi wa kiafrika, kujikuta wao ndio kila kitu hata kujiona bila wao, wewe huwezi kuishi.

Kumbe sivyo, Kwa nchi zilizo endelea mtu anaacha kazi leo kesho anapata kazi nyingine.

Na hiyo ni kawaida.

Kila mtu ana plan zake.
 
Hawo watu wanaharibia vijana wengine kupata kazi/ajira,maana kila atakaekuja unawaza yale yale ya huyo alieondoka gafla.ni bora kuwa na mikataba ya kazi,hata kama ni mlinzi wa geti,mkataba utambana yeye pamoja na wewe mwajiri.
Kupitia alivyoondoka kuna kitu nimejifunza
 
Kuna kitu nimejifunza hapa mkuu
 
Kabla hujawekeza chochote kwa mtu, Tambua kwamba hata huyo mtu ana plan zake kichwani.

Sasa usitarajie kwamba huyo mtu atafanya kazi na wewe milele yote.

Kuna muda utafika na yeye atahitaji kuondoka.
Huko sahihi huwezi kukaa sehemu milele. Ukiondoka kwa kufuata utaratibu sio tatizo. Tatizo nikuondoka kiuni.
 
Maisha kuna nyakati hayana kanuni rasmi Sana,ila kwakiasi kikubwa unapaswa kuwa MTU WA kuondoa sintofahamu hasa kwenye sehemu zenye maslahi

Vijana wengi Wana vitu vingi kichwani Hali inayopelekea busara kutumika kidogo kwenye maamuzi mengi.

Kuna jamaa alikuwa sehemu a anafanya kazi inawamiliki wawili lakini anafosi mishe ikatokea imetiki kazi idara ya mtume Mathayo,akamfungukia boss WA kwanza kuwa nimepata kitengo boss mmoja akafurahi na kumpa Baraka,bosi WA pili hakuridhia akaminya mchuzi WA mwezi mmoja.

Enewei Kila MTU anaona vitu na kuchukua uamuzi wake kadiri ya Uhuru wake.
 
Uko sahihi kwa 💯. Hawa vijana wanalia njaa kutwa kucha lakini ili reality ni pasua kichwa sana ukiamua kuwabeba. Hawabebeki. Fanya utaratibu ingiza wahindi mkuu hutajutia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…