Tetesi: Wataalam wa Kenya washindwa kutetea mradi wa bomba la mafuta

unanitaka

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2014
Posts
2,178
Reaction score
1,045
Habari zilizotufikia hivi punde kutoka Uganda katika kikao cha Makatibu Wakuu wa Kenya, Uganda na Tanzania kujadili mradi wa Bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda.

Kikao hicho kiliisha Saa 6:30 mchana bila makubaliano baada ya wajumbe wa Kenya kukataa kusaini makubaliano ambayo mapendekezo yote yanataka Mradi huo upite Hoima Uganda hadi Bandari ya Tanga (Tanzania).

Mtoa taarifa ametutaarifu Kuwa maoni ya Uganda kwenye Mradi huu nanukuu "Recommendations and firm conclusions of the Govt of Uganda is as follow:-

(1) The Tanzania Route provides the most economic and robust option for transportation of Uganda's crude oil because of the various advantages it has over the Routes through Kenya.

(2) The Kaabale-Tanga route promotes the development of an integrated regional pipeline project for oilfields of Kenya, S Sudan, DRC, Tanzania, Rwanda and Burundi'

Baada ya Uganda kutoa taarifa hiyo kulizuka mjadala kutoka kwa Katibu Mkuu wa Kenya na wataalam wake wakihoji kutokubaliana na majumuisho yakiofanywa na Serikali ya Uganda. Kikao kikiahirishwa bila Kuwa na mwafaka na Sasa kasi hiyo wameachiwa mawaziri wa Sekta husika katika kikao kitakachofanyika Saa 10 Jioni.

Habari tulizopata kutoka Ndani ya kikao hicho zinaeleza Serikali ya Uganda imekasirishwa na utaratibu unaotumiwa na Kenya ambapo kila kikao wanachoitwa wanashindwa na Watanzania lakini wanagoma kukubali matokeo ya wataalam na kuanzisha mjadala upya. Wajumbe wa Uganda walisikika wakisema 'Tumechoka na hawa watu, tulianza nao hii project miaka miwili iliyopita lakini hatujamaliza na hadi Leo wanaleta njia mpya ambayo haijafanyiwa tathimini, watuache tuendelee Kama wameshindwa"

Kauli hizo za wajumbe wa Uganda zinaonyesha kukubali Moja Kwa Moja Mradi huu upite Tanzania na kikao Cha Mawaziri kinaweza kikawa kifusi zaidi Kama Kenya watashindwa kukubali basi hatua ya Mwisho ni mkutano wa Marais watatu wa Kenya, Uganda na Tanzania baadae mwezi huu.
 
Tatizo ni nini hasa? Financiers ni kina nani maana nategemea mwenye mradi na wenye pesa kuwa na majibu ya huu mvutano..... otherwise mradi huu unakuwa financed na E.A. Community.... kweli mi sielewi kabisa kwa nini kuwe na huu mvutano.....
 
Huu sasa utani! Kwani kuna mafuta ya kenya yatapitia Tz? Au kuna makubaliano walishafanya miaka ya nyuma?
 
Tatizo ni nini hasa? Financiers ni kina nani maana nategemea mwenye mradi na wenye pesa kuwa na majibu ya huu mvutano..... otherwise mradi huu unakuwa financed na E.A. Community.... kweli mi sielewi kabisa kwa nini kuwe na huu mvutano.....
Financiers ni kampuni ya Total ya Ufaransa na walishasema kuwa kutokana na sababu za kiusalama bomba hilio lipitie Tanazania badala ya Kenya.

We waache Kenya wajishebedue lakini Bomba litapita Tanga.
 
Hao jamaa wa kenya wanajua hawawezi pangua hoja zilizopo mezani so hawataki sign ionekane ni wao wamesanabisha. But inajulikana swala hili tulisha shinda.
 
Haya mambo nlijua yameisha mana total wao wanavutiwa zaidi Tz sasa ina inakuwaje???
 
Financial ni kampuni ya Total ya Ufaransa na walishasema kuwa kutokana na sababu za kiusalama bomba hilio lipitie Tanazania badala ya Kenya.

We waache Kenya wajishebedue lakini Bomba litapita Tanga.
Financier. ..
 
Kama vipi waweke mpira kwapani waende wakaendeleze kilimo cha mirungi kwao. Hakuna ujomba kwenye international trade, leta hoja kama ziko poa unapewa dili sio kumbwela mbwela na kuzira kusaini. Zama zimebadilika bwashee msubirini Kikwete
 
Ukiungalia huu mradi kiuchumi na kisiasa, Tanzanian route is more advantageous than Kenyan. Hili bomba likipita Tanzania, Rwanda na Burundi nao watanufaika maana itakuwa rahisi kujiunganisha na hilo bomba wakati ambapo likipita Kenya, ni Sudan Kusini pekee ndio watafaidika.

Kenya wangewashawishi Sudan Kusini wajenge bomba la mafuta kupitia Kenya hadi Lamu. Kuwa na mabomba mawili yenye njia tofauti ni faida zaidi kwa EAC kuliko hilo moja ambalo Kenya wanalazimisha lipite kwao.

Vv
 
Habari zilizotufikia hivi punde kutoka Uganda katika kikao cha Makatibu Wakuu wa Kenya, Uganda na Tanzania kujadili mradi wa Bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda.

Kikao hicho kiliisha Saa 6:30 mchana bila makubaliano baada ya wajumbe wa Kenya kukataa kusaini makubaliano ambayo mapendekezo yote yanataka Mradi huo upite Hoima Uganda hadi Bandari ya Tanga (Tanzania).

Mtoa taarifa ametutaarifu Kuwa maoni ya Uganda kwenye Mradi huu nanukuu "Recommendations and firm conclusions of the Govt of Uganda is as follow:-

(1) The Tanzania Route provides the most economic and robust option for transportation of Uganda's crude oil because of the various advantages it has over the Routes through Kenya.

(2) The Kaabale-Tanga route promotes the development of an integrated regional pipeline project for oilfields of Kenya, S Sudan, DRC, Tanzania, Rwanda and Burundi'

Baada ya Uganda kutoa taarifa hiyo kulizuka mjadala kutoka kwa Katibu Mkuu wa Kenya na wataalam wake wakihoji kutokubaliana na majumuisho yakiofanywa na Serikali ya Uganda. Kikao kikiahirishwa bila Kuwa na mwafaka na Sasa kasi hiyo wameachiwa mawaziri wa Sekta husika katika kikao kitakachofanyika Saa 10 Jioni.

Habari tulizopata kutoka Ndani ya kikao hicho zinaeleza Serikali ya Uganda imekasirishwa na utaratibu unaotumiwa na Kenya ambapo kila kikao wanachoitwa wanashindwa na Watanzania lakini wanagoma kukubali matokeo ya wataalam na kuanzisha mjadala upya. Wajumbe wa Uganda walisikika wakisema 'Tumechoka na hawa watu, tulianza nao hii project miaka miwili iliyopita lakini hatujamaliza na hadi Leo wanaleta njia mpya ambayo haijafanyiwa tathimini, watuache tuendelee Kama wameshindwa"

Kauli hizo za wajumbe wa Uganda zinaonyesha kukubali Moja Kwa Moja Mradi huu upite Tanzania na kikao Cha Mawaziri kinaweza kikawa kifusi zaidi Kama Kenya watashindwa kukubali basi hatua ya Mwisho ni mkutano wa Marais watatu wa Kenya, Uganda na Tanzania baadae mwezi huu.
noli noli noli noli, M7 katufanya watoto,
 
Mi kinachonishangaza ni kuwa hao manyangau kwani wasiposaini kuna shida gani? Kwani wanatoa hela ya kufanya huu mradi?

Warudi zao unyang'auni wenye project waendeleze yao.
 
Mwenye Mradi kashaamua Bomba lipite Tanzania tatizo ni nini? Hawa jamaa wana lao jambo sio bure ngoja tusubiri
 
If this trend continues, EAC will not last longer like the former one.

It is said that Kenya and Idd Amin were the reason of the disintegration of the former EAC.

Vv
 
Hehehe kweli sisi manyangau ndio wenye EAC yaani hadi sasa bado mnakaa vikao mkituskiliza wakati nilidhani mlishafanya maamuzi.
Hadi mtupigie magoti muombe ndio tutaachia.

Yaani ardhi yenu, pesa ashatoa mzungu, Museveni ashaafanya maamuzi ya Tanga lakini bado mnatutgemea tutie saini. Sisi ndio baba wa EAC sasa mama ndio yupi kati yenu.
 
Back
Top Bottom