Ama kweli wabongo ni watu dhaifu sana kwenye masuala ya biashara za kimataifa. Hili la bomba limedhihirisha mpo hafifu sana, mna timu ambayo inafaa ipewe darasa kuhusu negotiations. Yaani ingekua sisi Wakenya ndio tuna hizo advantage mlizo nazo, hata hatungekua tunajadili chochote. Ni dhahiri kwamba
- Mzungu wa Total ameshaweka tayari pesa za ujenzi wa bomba, wakati sisi tunategemea kukopa
- Tanzania imetoa ardhi bure, wakati sisi tunategemea kununua
- Mkondo wa Tanzania ndio mfupi, wakati sisi kwetu ni umbali sana tena maeneo kame
- Tanzania inayo bandari tayari, wakati sisi hata bandari hatujaanza kujenga
- Tanzania haina tishio la ugaidi, wakati sisi tunachezea mabomu
- Serikali ya Tanzania imefaulu kuwatuliza watu wake kisiasa, wakati sisi tumewahi kung'oa reli inayokwenda Uganda
- Juzi tumeona kwa taarifa Tanzania imeamua kutotoza ada yoyote wala kodi, wakati sisi tumesisitiza lazima Museveni alipie
Yaani naweza andika kurasa nyingi sana kwanini bomba lipitie Tanzania. Ingekua sisi Wakenya ndio tuna advantages zote hizo, hii ni kazi ya kufanywa na mtu mmoja, hata hatungetumia timu kama jinsi Watanzania wamejazana kule Kampala. Mtu mmoja tu kama mimi binafsi naweza kumaliza mchezo.
Watanzania mtazidi kubaki kuwa watu hafifu sana. Mnatia huruma kuona eti mnashabikia wakati hapa hata hapafai kuwa na ushindani.
Franco Zetta unanitaka Crocodiletooth Vyamavingi Susuma BONGE BONGE mwanawao Doto Dotto rais wako zinj
HEKIMA KWANZA Sibonike kkenzki kadoda11