Wanaweza kujenga Refinery Rwanda na kurefusha bomba hadi Burundi na East DRC. Kwao itakuwa economic viable maana ni karibu zaidi na source ya visima vya mafuta kuliko kuagiza mafuta yaliyosafishwa kutoka Uarabuni.
Vv
Mkuu Vyamavingi
Katika dunia ya sasa inayo endeshwa kwa nguvu za uchumi kigezo kikubwa kinacho zingatiwa ni FAIDA. Na Faida hupatikana baada ya kutenga gharama.
Umbali wa kutoka kwenye visima vya mafuta vilivyopo Uganda (Lake Albert) hadi kufika mpaka wa Rwanda ni zaidi ya 330kms (180°South) bado hujafika Kigali.
Na umbali wa kutoka kwenye hivyo visima hadi kufika Tanzania wilaya ya Bukoba Vijijini mkabala na Kigali ni 380kms (175°South) na kutoka hapo hadi Kigali ni 90 kms (270°West).
Kwa mantiki hiyo Rwanda watakuwa watu wa ajabu kuamua kujenga bomba lao kutokea kwenye hivyo visima.