Wizara ya Ardhi
Govt Institution
- May 14, 2024
- 306
- 165
Wataalamu wa Ardhi Mkoani Singida wameendelea kunolewa katika matumizi ya mfumo wa e-Ardhi, hatua inayolenga kuwawezesha kutoa huduma bora na za kidijitali kwa wananchi.
Matumizi ya mfumo huo yanatarajiwa kurahisisha upatikanaji huduma za ardhi, kupunguza usumbufu kwa wananchi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.
Mafunzo hayo yameendelea leo, Septemba 15, 2026, ikiwa ni siku ya pili, ambapo wataalamu hao wameuelezea mfumo huo wa e- Ardhi kuwa watautendea haki kupitia mafunzo wanayoyapata.
Kwa mujibu wa wataalamu hao, matumizi ya mfumo huo yatachangia zaidi kuboresha huduma wanazozitoa kwa wananchi.