Mmiliki alikuwa akiitwa Anderson Nyato, Iringa tukimwita Mwanyato, alikuwa mfanyabiashara wa usafiri wa mabasi yakiitwa Comfort, alisaidiwa kuendesha biashara na mdogo wake Joshua (aliyekuwa mume wa Mkuu wa mkoa wa sasa wa Dodoma) wote ni marehemu kwa sasa, baada ya biashara ya mabasi kuchanganya, kumbuka yalikua ya mikopo, akapata wazo la kukopa milioni 700 kwa ajili ya kufungua Kitonga Comfort Hotel, hiyo ulikua mwaka 1993, na ilifunguliwa na mkuu wa mkoa Iringa wakati huo Marehemu Major General Herman Lupogo, nilihudhuria ufunguzi tukiwa vijana na weekend tujivinjari pale. Mkasa wa kwanza ilikuwa kusombwa swimming pool na mvua za Elinino 1993. Tatizo kubwa ilikua management na kujaza ndugu, hotel ikaanza kuyumba, niliwahi kumshauri laiti angejenga ndani ya Mikumi national Park asingekosa wateja mpaka wanyama waishe mbugani, was too late, benki wakaipiga mnada kupitia rafiki yake Seth Motto (Majembe Auction Mart), mabasi na nyumba yake binafsi pale Field Force ikakumbwa pia