Wataalamu wa Biashara nauliza Comfort Iringa ilikufaje wakati ilikuwa na wateja abiria wa mabasi?

Wataalamu wa Biashara nauliza Comfort Iringa ilikufaje wakati ilikuwa na wateja abiria wa mabasi?

Tatizo la confort hotel ilikuwa ni kuuza vyakula visivyo na ubora,bei juu, na vilivyolala, unauziwa chips zilizolala,halafu hazipashwi, unauziwa chips za viazi vibovu( vimefikia stage ya kuwa mbegu,vinakuwa na ukijani flan hivi halafu haviivi) vyenye uchungu. Nyama ya kuku iliyovunda. Na uchafu wa mazingira. Hata al jazeera ni kwa sababu tu hajapata mpizani,ila akipatikana wa kuweka hotel ya ukweli kama njia ya kaskazin pale anafunga. Liverpool alifunga hivyo hivyo sababu ya huduma mbovu akakosa wateja,sasa hivi alivyoikarabati na kuboresha huduma wateja wamerudi
 
Biashara tuige Wahindi na Waarabu,Baba,Mama na watoto wote mnakuwa ni biashara yenu na mnwajibika,sisi ngozi nyeusi ukipata pesa unaongeza wanawake na kila kitu unataka ukishikilie wewe maana huoni yupi anastahili,siku ukiondoka kila kitu kinakwenda...
Mama hajui namba ya siri ya ac ya baba ya bank.. Ngoz nyeusi tuna roho mbaya vibaya mno
 
Wataalamu wa Biashara nauliza Comfort Hotel, kitonga Iringa ilikufaje wakati ilikuwa na wateja abiria wa mabasi?
Alipofariki mwenye maono na mmiliki Andeson Mwanyato, ndugu zake waliobaki walishindwa kuendeleza uwekezaji wake mzuri. Hata mabasi yake yote yakaisha. Ila bado ni eneo mwafaka sana kwa biashara kama unaweza kununua na kuliendeleza.
 
Mmiliki alikuwa akiitwa Anderson Nyato, Iringa tukimwita Mwanyato, alikuwa mfanyabiashara wa usafiri wa mabasi yakiitwa Comfort, alisaidiwa kuendesha biashara na mdogo wake Joshua (aliyekuwa mume wa Mkuu wa mkoa wa sasa wa Dodoma) wote ni marehemu kwa sasa, baada ya biashara ya mabasi kuchanganya, kumbuka yalikua ya mikopo, akapata wazo la kukopa milioni 700 kwa ajili ya kufungua Kitonga Comfort Hotel, hiyo ulikua mwaka 1993, na ilifunguliwa na mkuu wa mkoa Iringa wakati huo Marehemu Major General Herman Lupogo, nilihudhuria ufunguzi tukiwa vijana na weekend tujivinjari pale. Mkasa wa kwanza ilikuwa kusombwa swimming pool na mvua za Elinino 1993. Tatizo kubwa ilikua management na kujaza ndugu, hotel ikaanza kuyumba, niliwahi kumshauri laiti angejenga ndani ya Mikumi national Park asingekosa wateja mpaka wanyama waishe mbugani, was too late, benki wakaipiga mnada kupitia rafiki yake Seth Motto (Majembe Auction Mart), mabasi na nyumba yake binafsi pale Field Force ikakumbwa pia
Nilikuwa najuana naye sana Anderson Mwanyato niliwahi kumpa ushauri wa kibiashara. Alikuwa msikivu na mtulivu ila alipenda kufanya aonavyo yeye na alikuwa na ujasiri wa kuthubutu.
 
Jina lilibadilishwa baada ya mnunuzi mpya, labda kifupi nilikua nao karibu, kuna mambo sio ya kuweka mtandaoni, Elinino hiyo ya 1993 Mwinyi alikuwa bado Rais na ilikua mwezi March alikagua mafuriko yale Dar es Salaam kwa Helkopta na RC alikuwa Kanali Anatory, Tarimo, kule Mtwara kulisombwa daraja kubwa la Chipite linalounganisha mnazi mmoja na Masasi, nahisi ulikua bado kiumri
Daraja la Chipite kijiji cha Nangoo, nimepita sana maeneo hayo
 
Jina lilibadilishwa baada ya mnunuzi mpya, labda kifupi nilikua nao karibu, kuna mambo sio ya kuweka mtandaoni, Elinino hiyo ya 1993 Mwinyi alikuwa bado Rais na ilikua mwezi March alikagua mafuriko yale Dar es Salaam kwa Helkopta na RC alikuwa Kanali Anatory, Tarimo, kule Mtwara kulisombwa daraja kubwa la Chipite linalounganisha mnazi mmoja na Masasi, nahisi ulikua bado kiumri
Shikamoo
 
Weka rekodi zako sawa mkuu, mwaka 1998 ndio kulikuwa na mvua za El Nino na balaa kubwa lilikuwa ni kuzolewa kwa basi la No Challenge Tanga...
 
Back
Top Bottom