Wataalamu wa Biashara nauliza Comfort Iringa ilikufaje wakati ilikuwa na wateja abiria wa mabasi?

Wataalamu wa Biashara nauliza Comfort Iringa ilikufaje wakati ilikuwa na wateja abiria wa mabasi?

Jina lilibadilishwa baada ya mnunuzi mpya, labda kifupi nilikua nao karibu, kuna mambo sio ya kuweka mtandaoni, Elinino hiyo ya 1993 Mwinyi alikuwa bado Rais na ilikua mwezi March alikagua mafuriko yale Dar es Salaam kwa Helkopta na RC alikuwa Kanali Anatory, Tarimo, kule Mtwara kulisombwa daraja kubwa la Chipite linalounganisha mnazi mmoja na Masasi, nahisi ulikua bado kiumri
We jamaa unaishi dunia yako. Mwaka 1993 sanasana kulikuwa ukame ambao haujawahi kutokea. Tukawa na mgawo wa umeme mkali kabisa kwa kuwa mabwawa yote karibu yalipungua maji.

kakolaki kumbuka unabishana na watu wenye kunbukumbu kuliko wewe
 
Mmiliki alikuwa akiitwa Anderson Nyato, Iringa tukimwita Mwanyato, alikuwa mfanyabiashara wa usafiri wa mabasi yakiitwa Comfort, alisaidiwa kuendesha biashara na mdogo wake Joshua (aliyekuwa mume wa Mkuu wa mkoa wa sasa wa Dodoma) wote ni marehemu kwa sasa, baada ya biashara ya mabasi kuchanganya, kumbuka yalikua ya mikopo, akapata wazo la kukopa milioni 700 kwa ajili ya kufungua Kitonga Comfort Hotel, hiyo ulikua mwaka 1993, na ilifunguliwa na mkuu wa mkoa Iringa wakati huo Marehemu Major General Herman Lupogo, nilihudhuria ufunguzi tukiwa vijana na weekend tujivinjari pale. Mkasa wa kwanza ilikuwa kusombwa swimming pool na mvua za Elinino 1993. Tatizo kubwa ilikua management na kujaza ndugu, hotel ikaanza kuyumba, niliwahi kumshauri laiti angejenga ndani ya Mikumi national Park asingekosa wateja mpaka wanyama waishe mbugani, was too late, benki wakaipiga mnada kupitia rafiki yake Seth Motto (Majembe Auction Mart), mabasi na nyumba yake binafsi pale Field Force ikakumbwa pia
Moja ya factor niliyoifanya ni kufungua kampuni ili kuepuka haya.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Comfort kitonga ...like any other husslers ...alikuwa na backup ya business zake ambayo ilikuwa mishe za hatar......jamaaa anguko lake alivamiwa na majambazi ambao walikuwa n masela wake alio wa snitch au kuwazulum.....hvooo alilazimishwa kusaini paper za kubadili ownership...yaa assets zake ikiwepo hotel yake ....baada yaa hapo jamaaa ali freeze forever...na mwshon mtakumbuka hotel ilibadilika jna ...kabla hajaja mpizan AL JAZEERA.... hii ili kuwa ndo .THE LAST NAIL IN COMFORT COFFIN...
Uongo wa hali ya juu.
 
N
Hapoa BONGO ukiiga biashara unaweza firisika
Mfano kma unaona SHABIBY ana mabus kibao
Il ukiambiwa Utajiri wake upo sehemu nyingine utakataa
Iga wewe sasa uanzishe bussines kama hiyo utakufa kifo cha mende kma SUMMY za mbeya
hawa wanakuwa na biashara nyingine za magendo hutumia vitega uchumi kama hvyo kutakatisha fedha sasa zile deal zikifika inakuwa ngumu kuendesha BIASHARA isiyo na faida

Nb-: hiyo SHABIBY nimetoa mfano tu ili nieleweke haisuiani msije mkampopoa mzee wa watu yeye anasema wakt yupo na miaka 20 tayari anamuliki mabus je wewe kijana una miaka 30 unamiliki nini smartphone au
Namiliki boda boda used kila siku Kwa fundi
 
Ni sahihi kwani wazazi hatuwashirikishi watoto wetu kuhusu biashara tufanyazo..?
Yaani hata mimi sielewi kwa kweli
Hili ni tatizo kubwa mno kwa wafanyabiashara ngozi nyeusi tofauti na wenzetu weupe.Serikali itangaze kuwa ni tatizo la kitaifa
 
Yaani hata mimi sielewi kwa kweli
Hili ni tatizo kubwa mno kwa wafanyabiashara ngozi nyeusi tofauti na wenzetu weupe.Serikali itangaze kuwa ni tatizo la kitaifa
Tatizo ni kukosekana kwa uaminifu kwa watoto wetu. Pia kukosekana kwa utulivu kwa baadhi ya watoto wetu.

Unaweza mshirikisha yeye akaanza kuhonga kutokana na biashara ya Baba.
 
Tatizo ni kukosekana kwa uaminifu kwa watoto wetu. Pia kukosekana kwa utulivu kwa baadhi ya watoto wetu.

Unaweza mshirikisha yeye akaanza kuhonga kutokana na biashara ya Baba.
Kwani wenzetu wahindi,waarabu na wapemba wanafanyaje hadi watoto wao wanakuwa waamijifu na kuwa na utulivu kwenye biashara na nidhamu ya matumizi ya pesa za biashara? Hadi ngozi nyeusi tushindwe kuiga?
 
Elnino ilikuwa mwaka 1998 labda hiyo 1993 ilikuwa mafuriko mengine.

2005 nilipita na BUS la KILIMANJARO hapo comfort na kula , nilikuwa naelekea Mbeya.
Mpaka mwaka 2014 hiyo hotel ilikuwa inafanya kazi japo kwa kusua sua

Hizi picha niliipiga mimi mwenyewe tar 28/11/2014, hata hayo mabasi kwa sasa yote hayapo. Deluxe aliziuza na kuacha biashara ya mabasi ruti ya Iringa - Dar, Mcaraghan amefariki dunia miezi michache iliyopita, ila nae basi lake lilianza kwenda vijijini ndani ndani huko.
 

Attachments

  • IMG_20141128_100812.jpg
    IMG_20141128_100812.jpg
    464.8 KB · Views: 5
  • IMG_20141128_100843.jpg
    IMG_20141128_100843.jpg
    447.8 KB · Views: 6
Mpaka mwaka 2014 hiyo hotel ilikuwa inafanya kazi japo kwa kusua sua

Hizi picha niliipiga mimi mwenyewe tar 28/11/2014, hata hayo mabasi kwa sasa yote hayapo. Deluxe aliziuza na kuacha biashara ya mabasi ruti ya Iringa - Dar, Mcaraghan amefariki dunia miezi michache iliyopita, ila nae basi lake lilianza kwenda vijijini ndani ndani huko.
Hii deluxe naikumbuka sana. Nishapanda nayo kwenda Iringa. Mpaka around 2015 ilikuwa inafanya kazi japo ilikuwa imechoka kweli. Nakumbuka abiria walikuwa wanalalamika kulishwa chips za juzi!
 
Back
Top Bottom