KERO Wataalamu wa Maabala tuliofanya Mitihani ya Leseni mwezi Machi tunaumizwa na Ucheleweshwaji wa Matokeo, HLPC KULIKONI?

KERO Wataalamu wa Maabala tuliofanya Mitihani ya Leseni mwezi Machi tunaumizwa na Ucheleweshwaji wa Matokeo, HLPC KULIKONI?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sisi wataalamu wa maabara(certificate hadi degree) nchini Tanzania ambao tulifanya Mtihani wa Leseni kuanzia march 15 hadi april 01(certificate hadi degree) tumecheleweshewa kupewa matokeo kwa zaidi ya miezi miwili sasa, hali ambayo inatukosesha fursa nyingi ikiwemo ajira zinazotangazwa.

Matokeo yalipaswa kutolewa ndani ya mwezi mmoja, changamoto ni kuwa Baraza la wataalamu wa maabara(HLPC) ambao ndio wahusika wa kila kitu hawasemi chochote, kibaya zaidi kwa taaluma yetu huwezi fanya chochote bila kuwa na leseni, kwani tukipata matokeo ndio tunatakiwa kuomba leseni.

Pia passmark hasa za mitihani ya vitendo(practical) zipo juu sana 70% wakati theory ni 60%, wakati chuoni ilikuwa 50%.
 
Umeshaliwa kichwa si namba ya FRL/HLPC/2026/0123


Wewe utafanya pepa hara mara 10
 
Wahitimu wa taaluma ya udaktari tunapenda kuwasilisha hoja kuhusu changamoto inayojitokeza katika mchakato wa upatikanaji wa leseni za udaktari nchini.

Kumekuwa na malalamiko kwamba Baraza la Madaktari Tanzania huchukua muda mrefu zaidi ya ilivyotarajiwa kutoa matokeo ya mitihani kwa wahitimu waliomaliza mafunzo ya utarajali na kufanya mitihani yao ya kitaaluma. Hali hii husababisha kuchelewa kwa upatikanaji wa leseni za kazi, jambo linalowakwamisha wahitimu kuanza kujipatia kipato na kutoa huduma kwa jamii.

Kwa mujibu wa utaratibu unaotarajiwa, matokeo na mchakato wa utoaji leseni ungeweza kukamilika ndani ya muda mfupi, kwa mfano mwezi mmoja baada ya mitihani kufanyika. Hata hivyo, kumekuwa na ucheleweshaji wa muda mrefu, ambapo baadhi ya wahitimu waliomaliza mitihani yao miezi kadhaa iliyopita bado hawajapata majibu au leseni zao. Hali hii imepelekea baadhi yao kukosa fursa muhimu za ajira na maendeleo ya kitaaluma.

Kutokana na hali hiyo, kunahitajika ufafanuzi na mapitio ya mchakato huu ili kuhakikisha unafanyika kwa ufanisi na kwa wakati, ili kuondoa changamoto zinazowakabili wahitimu wa udaktari.

Tunaomba mamlaka husika zilifanyie tathmini suala hili ili kuboresha mfumo wa usimamizi wa mitihani na utoaji wa leseni, kwa lengo la kuongeza ufanisi na kurahisisha wahitimu kuingia katika soko la ajira kwa wakati.

Tunasisitiza umuhimu wa uwazi, uwajibikaji na uharakishaji wa huduma hizi muhimu kwa maendeleo ya sekta ya afya nchini.
 
Wataalamu wa Maabara tuliofanya Mitihani ya Leseni mwezi Machi tunaumizwa na Ucheleweshwaji wa Matokeo, HLPC KULIKONI?

Nilitumia jukwaa hili kutoa KERO ya kucheleweshwa matokeo. Pia kupiga simu kwenye Ofisi ya HLPC, wanasema shida sio wao bali ni viongozi.

Tunaomba jukwaa la JF mtusaidie kupaza sauti maana media ni Muhimili wa 4 kama lilivyo bunge nk.

Kada ya afya huwezi kufanya kazi bila kuwa na Leseni hai. Hivyo toka tufanye mtihani tupo mtaani bila ya kufanya kazi.

Pia, Serikali mwezi huu imetangaza nafasi za kazi kwa Certificate. Itakuwa ngumu kuomba maana hatuna leseni na kufanya mitihani ya usahili mpaka leseni hai. Pia, kuna fursa kwenye Hospital binafsi ila bila leseni kazi huwezi kupata.

Sambamba na hilo, Alama za ufaulu zipo juu sana kuliko alama za ufaulu tukiwa chuoni.

Naomba kuwasilisha.
IMG-20260618-WA0007.jpg

IMG-20260613-WA0014.jpg
 
Back
Top Bottom