Wataalamu wa rangi za nyumba naomba msaada wenu kabla hapajakuchašŸ™

Wataalamu wa rangi za nyumba naomba msaada wenu kabla hapajakuchašŸ™

prida

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2026
Posts
1,297
Reaction score
2,596
Eti wakuu hiyo rangi hapo kwenye picha ni ya kupaka ndani au nje ya nyumba.?

Eti ni kweli kwamba rangi ikiwa na neno EMULSION haifai kupaka nje ya nyumba?

Kama rangi hii ni ya nje,je ni miongoni mwa rangi bora?

Kama sio,naomba mapendekezo ya rangi bora za kupaka nje.

Nyumba ilishapakwa rangi nataka kuirudia tu.

ASANTENI
Screenshot_20260612_215829_Gallery.jpg
 
Ina faa bila shaka yoyote maadamu tu fundi azingatie kanuni maana umesema una rudia kupaka .

Na pia hii ni moja ya rangi bora sana kwa kuta za nje.
 
Eti wakuu hiyo rangi hapo kwenye picha ni ya kupaka ndani au nje ya nyumba.?

Eti ni kweli kwamba rangi ikiwa na neno EMULSUON haifai kupaka nje ya nyumba?

Kama rangi hii ni ya nje,je ni miongoni mwa rangi bora?

Kama sio,naomba mapendekezo ya rangi bora za kupaka nje.

Nyumba ilishapakwa rangi nataka kuirudia tu.

ASANTENIView attachment 3606550
Hio ni rangi ya nje. Mafundi hawajui Kiingereza wakisikia emulsion wanajua ni rangi ya ndani tu.
 
Hio ni rangi ya nje. Mafundi hawajui Kiingereza wakisikia emulsion wanajua ni rangi ya ndani tu.
Zilikuja kama zawadi ila fundi akanambia ukiona rangi imeandukwa hili neno "masheni"(emulsion) ni rangi ya mqji huwezi kuipaka nje.

Hata hivyo leo zimeanza kutumika baada ya muongozo wako na wa mkuu pendaeli.

AsantenišŸ™šŸ™
 
Kumbe Kuna rangi ya ndani ya nyumba na Kuna rangi ya nje ya nyumba? Nilikuwa sijui.
Nje inapakwa rangi maalum ambayo inaweza kuvumilia na kukinga nyumba dhidi ya maji maji,jua etc yaani inavumilia hali ya hewa yoyote bila kuharibika. Ndani inapakwa rangi ya kawaida hata ya maji.
 
Emulsion ipake wakati iliyopakwa awali ni Emulsion

Usije kupaka hiyo takataka wakati ulitangulia kupaka silk

Ila jambo la msingi

Kama uliskim nyumba na ukapiga msasa hakikisha kama ulioamua kutumia emulsion anza kupaka moja kwa moja usiweke primer

Ni rangi nzuri kwa ndani inaruhusu ukuta kupumua
 
Back
Top Bottom