Kwema?
Kwanini Captain Tesha alitoka mbele ya kadamnasi na kuzungumza mambo mazito vile huku akitaja baadhi ya wanasiasa kuwa wazuiliwe kukimbia nchi?
Kwanini Captain Tesha alionya polisi watakazuia waandamanaji kuwa watakuja kuulizwa hapo baadaye?
Lengo lake hasa la kutoka hadharani ni lipi?
Ikiwa (labda) kuna mpango wa coup d'etat why atoke hadharani kumpa faida ya kujipanga huyu aliyeko madarakani?
Amefanya hivyo kwa lengo gani hasa na ni ipi target yake katika hilo?
Kwasababu umetamani kujifunza wacha ujibiwe kwa heshima
Kimsingi hiyo ni miongoni mwa mbinu chache zenye nia njema.
Kimedani inatambuliwa kama (conscientious disobedience) yaani uvunjwaji wa sheria kwa makusudi au hutambuliwa pia kama Principled Ins disobedience .
Pengine unaweza kuwa na swali la nyongeza, je! Siyo kosa kisheria?
Ufafanuzi, kwa muktadha wa kijeshi nidhamu na utii au kwakifupi tuite (chain of command) ndio msingi wa utendaji.
Kuvunja sheria hizi ni hatari na adhabu zake huwa nzito ,hata kifo wakati mwingine.
Lakini kisichofahamika na wengi nikwamba hata mwanajeshi ana wajibu wa Kikatiba na wa Kimataifa wa kukataa amri zisizo za kisheria, Kwa mfano, amri ya kutekeleza mauaji ya kimbari au mateso.
Najitahidi kufafanua kwa ufupisho sana ili tusipoteane.
Nini hasa lengo husika ?
Lengo husika hapo huwa ni kupeleka ujumbe kwa serikali, hatua hiyo inaweza kuitwa Whistleblowing (Kupiga Kengele ya tahadhari kwa watawala wakisiasa).
Na hapo muhusika nilazima ajijite kwenye key issues kuielekeza serikali husika maeneo ambayo kwa upande wa Jeshi inatamani kuona yakifanyiwa kazi, hapo wanaweza kugusa maeneo mbalimbali mfano yanayohusu pengine ufisadi, uonevu wa haki za raia na makosa mengine makubwa makubwa ndani ya taasisi yake kwa madhumuni ya kuitaka serikali au umma kujua na kuchukua hatua.
Twende harakaharaka.
Nikuwekee mifano michache ninayoikumbuka .
Unaweza kuingia Google na ukatafuta kisa cha mwamba sana Daniel Ellsberg nadhani hii iliwahi kuandika kwenye (Pentagon Papers) saga la mwamba huyu aliwahi kuchapisha hati za siri za serikali ya Marekani zilizoonyesha ukweli kuhusu Vita vya Vietnam na kuzimwaga hadharani ,lengo alitamani tu kumjulisha Umma ujue ili tuanze kupiga kelele na serikali iweze kuchukua hatua ya kuyarekebisha hayo makosa waliyotuhimiwa nayo.
Lakini pia kunamwingine aliitwa Chelse Manning if am not mistaken
Huyu bwana nae alitumia nafasi yake kama mwanajeshi wa Marekani kupeleka faili nyingine za siri kwa WikiLeaks, aliziona zinamapungufu makubwa kwenye eneo la ukiukwaji wa haki za binadamu.
Kwa uchache niishie hapo .