Hii sio kweli kwa 100%.
Serikali haikufuta ada za utalii kulipwa kwa dola, bali serikali ilifuta utaratibu wa kulazimisha malipo mbali mbali hapa nchini kuwa kwa dola.
Serikali inahitaji mnoo dola kutoka nje ziingie nchini (ili ikienda nje kufanya malipo izitumie) na serikali kwa sasa haitaki kutoa dola zake kuzunguka humu humu nchini hivyo ndio hilo dhumuni la kufanya hivyo.
Mpaka leo hii na saa hii watalii kutoka nje wanalipa kwa dola. Na hilo ni rahisi kwao na habari njema zaidi kwa serikali
Mwisho kabisa, kushuka kwa dola dhidi ya shilingi ni suala la mpito na halina uhusiano wa moja kwa moja na hatua za serikali. Kitaalamu tunasema it is a nature phenomenon of the graph!