mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Kwa lugha rahisi, mfamasia ni mtaalamu wa madawa! kazi yake inahusisha kutengeneza, kuchanganya, kutunza na kufikisha dawa kwa wagonjwa zikiwa salama. Ndiye anayeweza kuya-handle madawa na anajua vizuri kwa undani mode of action ya madawa. Daktari/MD ni mtaalamu wa tiba! kazi yake ni kutibu watu , anajua ni dawa ipi inafaa mgonjwa yupi, lakini, si mtaalamu wa kui-handle na kuitunza hiyo dawa, na hata mode of action ya hiyo dawa si lazima aijue kwa undani!!. Nurse ni mtaalamu wa kuuguza! kazi yake ni kuuguza wagonjwa na kuwandle wagonjwa katika kipindi wanachokuwa wanatibiwa. Ndiye anayefuatilia hali ya mgonjwa jinsi anavyoendelea!
Utaona kuwa kila mtaalamu ana majukumu yake ya kumtosha yaliyomgharimu miaka isiyopungua 5 kuhitimu kwa ngazi ya shahada!! Kwenye masomo yao kuna baadhi ya kozi wanazisoma wote!! Kwa hiyo hakuna ambaye ni mshamba kabisa kwa eneo laa mwenzake na hapo ndipo tatizo linapoanzia!! Kwa kuwa kila mmoja anajua baadhi ya majukumu ya mwenzake anaweza kujaribiwa kuona kuwa anaweza kuyafanya mwenyewe!! Kwa mfano Daktari anaweza kuona anaweza kuendesha pharmacy kwa kuwa kuna vitu anavijua kuhusu madawa wakati SI KWELI!! Hali kadhalika mfamasia kuna vitu vingi anavijua kuhusu tiba kwa mujibu wa masomo yake na kwa mujibu wa uzoefu na siku hizi kuna ku-google!!. Kwa hiyo naye anaweza kuona anaweza kumtibu mgonjwa wakati SI KWELI!! Pia Nurse yeye pia kwa mujibu wa masomo yake na uzoefu wake na ku-google naye pia anajua mambo mengi sana ya kifamasia na kidaktari. Kwa hiyo nurse naye anaweza kuona anaweza kufanya majukumu ya mfamasia au ya daktari wakati SI KWELI. Afya zetu ni jambo TAKATIFU, lazima zishugfhulikiwe na mtaalamu husika kwenye eneo husika!!
Wataalamu wetu hawa waheshimiane, wasihasimiane, wasiingiliane na watimize majukumu yao kwa mujibu wa Sheria na kwa mujibu wa taaluma zao!! Ni ukosefu wa maadili daktari kuingilia majukumu ya mfamasia, hali kadhalika ni ukosefu wa maadili mfamasia kuingilia majukumu ya daktari. Kwa bahati nzuri madaktari na wafamasia huwa hawaingilii majukumu ya NURSE!! nafikiri ni kwa sababu ni magumu sana na hayaambatani na maslahi wakiyaingilia. Ila nurses huweza kujaribiwa kuingilia majukumu ya daktari na ya mfamasia hasa akiwa kwenye pharmacy!!
PENDEKEZO: Kuwe na adhabu kubwa sana kwa mtaalamu atakayeingilia majukumu ya taaluma isiyo yake kwa kuwa kwa kufanya hivyo atakuwa anahatarisha afya zetu.